Waliofukuzwa CHADEMA waanza kupewa vyeo Bungeni, Grace Tendega awa Mwenyekiti wa LAAC

Waliofukuzwa CHADEMA waanza kupewa vyeo Bungeni, Grace Tendega awa Mwenyekiti wa LAAC

Grace Tendega, mmoja wa Wasaliti waliojiteua na kuapishwa na Ndugai kuwa wabunge wa viti maalum kutoka Chadema, leo ametunukiwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa ( LAAC )

Bado haijafahamika kama aliomba nafasi hiyo au amepewa bure.

Bali swali kubwa ni hili , ni yupi mwingine atayekikwaa cheo cha bure miongoni mwa wasaliti waliosalia ?
 
huku mtaani maisha ni magumu sana hivyo bora tu kukomaa na maisha yetu, kuliko kufuatilia bunge ambalo kimsingi ukiangalia ni kama hatuna katiba ya nchi bali tunaenda tu kwa utashi wa watu flani mwenye maamuzi na siyo katiba ya nchi tena
 
% cdm ilizopata kwenye uchaguzi mnaosema ni batili ndio zimeipa wabunge wa kuteuliwa na ruzuku cdm,but ruzuku mnachukua wabunge amuwataki
Kamati kuu ya chadema ituambie kuhusu ruzuku endapo itaingia kwenye akaunti yao. Wasiposema tutaiona kwenye taarifa za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali.
 
Grace Tendega, mmoja wa Wasaliti waliojiteua na kuapishwa na Ndugai kuwa wabunge wa viti maalum kutoka Chadema, leo ametunukiwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa ( LAAC )

Bado haijafahamika kama aliomba nafasi hiyo au amepewa bure.

Bali swali kubwa ni hili , ni yupi mwingine atayekikwaa cheo cha bure miongoni mwa wasaliti waliosalia ?
Wabunge wanawake waliona mbali, Yaani wengine wacheze comedy ya kukimbia nchi na familia zao ili walipiwe maisha yao na familia zao wao walale njaa
 
CHADEMA inasema kwamba uchaguzi haukuwa halali na Mwenyekiti na Makamu walitoa tamko kabisa.
Sasa kwanini Chama kichukue ruzuku zinazotoka na matokeo ya uchaguzi ambao siyo halali ???
Hizo pesa siyo za watawala, ni za wananchi wote. Ni afadhali wachukue kwa ajili ya kusaidia kuimarisha chama.

Ukikuta nyani wanaiba mahindi shambani kwako ukasusa shamba lote, tija yake ni nini?

Cdm walisusia ule uchaguzi wa hovyo wa S/Mitaa wa 2019, je, kulikuwa na manufaa yoyote kwa wananchi?
 
Back
Top Bottom