Waliomlazimisha Samia Suluhu kuwa Makamu na hatimaye Rais, walifanya makosa sana

Usiangalie kauli angalia matendo yake na utimizaji wa ahadi zake. Maneno yanaweza kuwa mepesi kwako, lakini tambua ni sehemu ya malezi yake, hakufundishwa kufokea wala kukebehi watu.

Tazama matendo yake, tazama lugha yake ilivyo na uwezo wake wa kukubalika kimataifa ulivyo. Tazama convincing power aliyonayo katika taasisi nyeti za kidunia. Tazama aina ya teuzi zake zinavyokuwa makini.


Jana umesainiwa mradi mkubwa wa gesi, nadhani unaelewa faida zake kwa taifa hili kwa miaka mingi ijayo.
 
Kati ya sifa muhimu ya kiongozi kwa taifa lenye watu waliojaa ubinafsi sababu ya uvivu wa kufikiri na kutenda lkn wanataka mambo mazuri..ni kukemea na kufoka, nchi yetu haihitaji mtu mwenye convincing power..amconvince nani kuja kufanya nini? Kwa hatua hii vitu vyote tunavyohitaji kwa maendeleo tunavyo..kinachotusumbua ni ulafi na ubinafsi..unaweza kusaini hata mikataba 100 kwa siku, lkn ni bure kama usimamizi wa rasilimali kwa mikataba hiyo ni mdogo au haupo kabisa..teuzi gani makini, miaka 60 baada ya uhuru unateua mtu/watu bila muhusika kuhojiwa kupima uwezo wake kwa nafasi anayoteuliwa, makaratasi ndiyo yanapima uwezo wa mtu..this s terrible! No wonder this nation is still poor! Acheni kusifia hata visivyohitaji kusifia..
 
Timu Jiwe mnaumia sana. ni muda wake sasa, mwacheni aupige mwingi kwanza💪💪
 
Labda amuombe Mungu kila anapokwenda kanisani au msikitini ili atushushie malaika aje awe rais wetu. Kwa maana hakuna binadamu mwenye kufaa kuwa rais kwa akili hizi za kitanzania.
Wewe kwa akili yako unaweza kuomba hivyo? au hata hujui maana ya uwepo wa malaika na Mungu anawatumia kufanya nini..watu kama nyinyi huwa natamani Mungu akufinye kidogo akili ikae sawa ujue vitu vya kusema kwa wengine..ndio maana wenye akili kama zako wanadai kufa kwa JPM Mungu alimuondoa eti kwa maumivu waliyokuwa wanapata wahalifu, wezi na wavivu wakati wa uongozi wake, watu wangapi walitwaliwa 2021 hata wenye rekodi za kutenda mema kwa kiwango cha juu kabisa km TB Joshua! Mungu ana ratiba yake tofauti kabisa na akili za binadamu..lakini jambo la kufahamu kwa kila binadamu ni hili, kila mtu chini ya jua ameletwa hapa duniani kwa kusudi, aliyemleta ndiye anajua ametimiza kusudi aliloletwa kufanya au bado! Badala ya kupoteza nguvu na muda kudhani Mungu anamuondoa usiyempenda ili ufurahi..tafuta kusudi linalofanya uendelee kuishi itakusaidia sana kwa maisha yako sasa na badae.
 
Kazi inakuja namna ya kumtambua rais mzuri.........kuna ambao kwao rais mzuri ni yule anaewashughurikia ipasavyo wapinzani
 

Uko sahihi ila popoma watakupinga
 
Ile takataka inapukuswa tu huko sasa hivi
 
Kazi inakuja namna ya kumtambua rais mzuri.........kuna ambao kwao rais mzuri ni yule anaewashughurikia ipasavyo wapinzani
...
Kazi inakuja namna ya kumtambua rais mzuri.........kuna ambao kwao rais mzuri ni yule anaewashughurikia ipasavyo wapinzani
... na wakati rais huyo mzuri anawashughulikia apasavyo wapinzani wao wanamlewesha na sifa za kijinga ili wapate ujira wao wa kufumbiwa macho wanapoFISADI nchi! 😅
 
Hawa marais tulionao ni kusudio la Mungu huyo huyo tunayemlalamikia kwanini hawa ni marais wetu.

Lowassa aliutafuta urais kwa miaka zaidi ya kumi, aliupata?. Wengi tu wanatafuta urais kwa kujipanga na kuwa na team imara nyuma yao, huwa wanaupata?.

Tuwe tunaridhika kuliko kulalamika, kana kwamba kila rais anayekuwa pale ikulu hafai chochote, tunakufuru mara nyingi tu kwa kujiona tuna haki kuliko kile tunachokipata.
 
Unateseka ukiwa chato au Burundi?
 
Utajuaje kama kiongozi fulani ni mpango wa Mungu au la, ikiwa wapo wachache wananufaika na wengi wanalalamika?

Kwangu mimi hayati JPM, ndiye alikuwa hasa kiongozi wa mpango wa Mungu. Maana tuliomba muda mrefu kupata kiongozi kama yeye. Mapungufu yake hayawezi kubatilisha mtazamo huo.
Ila huyu wa sasa, bado sijajua maono yake kwa watanzania, hasa kwa kauli na maamuzi yake!
Gharama za maisha ziko juu, kufukuzwa kwa machinga mjini, uwepo wa tozo za miamala ambazo hatujui matumizi yake,
Bila kusahau safari za mara kwa mara, sherehe za kitaifa zisizo na tija...
kwa kifupi wananchi wanaoitwa 'wa kawaida' hawamuelewi kabisa!
 
Sio kweli, wapo viongozi wengine ni zao la makosa ya binadamu be it kwa kufahamu au kutofahamu..kuna mazingira ambayo kiongozi anapopatikana dhahiri yanaonyesha kuna mkono wa Mungu, kiongozi apatikane kwa wizi wa kura na kuumiza watu bado useme ni mapenzi ya Mungu? hakuna kitu kama hicho..kiashiria kizuri kupima uongozi ulioridhiwa na Mungu angalia trend ya mambo ya asili, km misimu ya mvua, matukio ya maisha ya kila siku ya watu..mfano upendo, chuki, mauaji nk frequency ya mambo haya yatakuonyesha kuna baraka au laana kwa uongozi uliopo.
 
Siku ya uchaguzi mnalala mpaka saa nane mchana halafu mnauliza bila aibu kashinda nani?.

Lazima mlalamike mpaka siku ya kwenda kaburini kama akili ni hizi, kama uvivu wenu wa kushughulika na siasa ni wa kiwango hiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…