Umeme umesambazwa nchi nzima. Mazingira ya kufanya biashara yanazidi kuboreshwa kila kukicha.
ATCL inanunua ndege na zinafanya kazi ya kuonekana, mashirika yanaingiza gawio hazina, bandari imekuwa ya kisasa tofauti na miaka ya awamu ya kwanza, mengi yanafanyika na tija inaonekana.
Kilimo kinaingiziwa pesa nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mikubwa. Nchi ipo kwenye mchakato wa kusimama vyema tangu 2015.
Kuwategemea Nape na Makamba wafanye mambo machafu wakati wa uchaguzi ni kushindwa kuiona picha pana inayokuwa mbele ya macho yako.
Na wao kwa bahati mbaya wameishi wakiwa na fikra kwamba wanao umuhimu unapofika mwaka wa uchaguzi, ni mawazo fulani ya kipuuzi tu.