Mkuu umenifundisha kitu hapa. Huyu mtu anayeitwa faizafoxy ni wa ku-ignore aeleweki kabisa! Sijui nyerere au wakatoliki walimfanyia ubaya gani hadi anaonekana kuchanganyikiwa kuhusu mambo yao yasiyomhusu badala ya kupambana na hali yake huko aliko kwenye u-islam?Ningekujibu ila ngoja niku-Ignore
Samurai...
Ili kunifanya nielewe hebu niwekee hapa sentensi ambayo nimeandika hivyo niweze kukujibu.
Sasa hapa ndipo palipowavutia wasomaji wengi kusoma kuwa Nyerere si aliyekuwa na ''blue print'' ya TANU bali kaikuta kwa Abdul na Abdul kapokea harakati zile kutoka kwa baba yake.
Prof...Hii hapa phrase inayofanana na hiyo aliyosemea mdau SamuraiJack. Nadhani kwa kuwa wewe ni mwandishi basi utaelewa.
Please my dude can you demystify that hidden part of independence struggle history?Hili halisemwi kwamba Kuna mtu hakutaka historia ya mchakato wa ukombozi wa nchi yetu iwe bayana kwa nia ya "monopolising his prestige"
Mwalimu was classmate of my father in Tabora, of course, Mwalimu has indeed done good things for this country but one of his attitude at the school as my father narrated makes me nervous, it was the underlying attitude which made some of the independence struggle history be hidden.
Utakataaje kuwa sio Lucy Lameck ili hali humjui ni nani? Mimi nakuhakikishia kuwa ndiye kwani Lucy na Titi Mohamed walikuwa mstali wa mbele kwa mambo ya siasa wakati huo!!! Muulize Juma Mwapachu anaweza kukusaidia kwa hili!!! Pengine hata balozi Paul Rupia anaweza kuwa na msaada hapa.
Nipo kijijini. Usisahau hilo.Una shauri nini, au unashauri nini! Unaandika kama umetoka kijijini jana?!
= mstari
Halafu wewe bwana au sijui ni bibi (utaniwia radhi nashindwa ku "identify gender" kwa ID yako) ni hodari sana tena sana, umetuletea historia nnzuri sana ya wakati huo na ya uhakika kabisa, imesambaratisha kabisa ya huyu Mzee Mohamed Said sijui amwitoa wapi.Usinionee huruma kwani mimi sio wa kuhurumiwa na mtu kama wewe. Mohamed unaweza kuandika kitabu kikajaa upuuzi na mwingine akaandika paragraph moja ikawa imeja busara na substance kwahiyo ujue kwamba quantity does not always mean acceptance!! Ujifunze kuwa mvumilivu na kukubali pale hoja zako zinapohojiwa.
Halafu wewe bwana au sijui ni bibi (utaniwia radhi nashindwa ku "identify gender" kwa ID yako) ni hodari sana tena sana, umetuletea historia nnzuri sana ya wakati huo na ya uhakika kabisa, imesambaratisha kabisa ya huyu Mzee Mohamed Said sijui amwitoa wapi.
Yako ni murua kabisa.
Lakini siioni iko wapi kwa sasa! Naomba iweke tena.
Inaelekea Sheikh Mohamed Said hapendi wazo la peer review kwani amejiaminisha kuwa kile anachoamini yeye ndio sahihi!! Nimejaribu hata kumpa references za watu ambao wangeweza kumsaidia akapata uhakika wa picha ile lakini bado anang'ang'ania kile anachoamini yeye. Daisy alikuwa mtoto mdogo sana wakati wa haraketi za marehemu baba yeke lakini kuna baba yake mdogo aitwae Abbas ambale pia alikuwa mwanasiasa wakati huo,yeye anaweza kuwa na kumbukumbu sahihi kuliko mwanae.
Zaidi ya hayo sio wakina mama wa Kiislam peke yao ndio walijishuhulisha na siasa za TANU iwe Dar es Salaam [ mfano huyo mama aliyevaa sketi kwenye hiyo picha ] hata huko bara. Ntakupa mfano mmoja ninaoufahamu sana ni kule Nyanda za juu kusini ambako vinara wanawake wa siasa enzi za TANU walikuwa mama BINTI MATOLA na mama BINTI MWASHAMBWA. Kama ilivyokuwa, mmoja alikwa muislam na mwingine alikuwa misheni! Hata baada ya kuundwa UWT wakina mama wa madhehebu mbali mbali walichaganyika.
Yupo mwingine anakaa Kata ya Majengo, anaitwa Mama Mwaipasi. Huyu ni Mmoja wa Wanachama wa TANU wa awali kabisa Mkoa wa Mbeya na ni Mkristo.
Ndinani,Mama mwaipasi amekuja nyuma sana ya hao Binti Matola na Binti Mwashambwa!! Wilfrem Mwakitwange ndio muanzilishi wa Tanu hapo Mbeya ; wakina Mzee Enos Mwangoka wamekuja nyuma yake.
Si ndio maana nikakwambia historia uliyotuletea wewe ni "bab kubwa" na haipo "biased" kabisa.Mimi ninachokifanya ni kutoa maoni yangu juu ya yale Sheikh Mohamed Said anayoandika , kwani kwa bahati nzuri mwenyezi Mungu amenipendelea wakati wa miaka hiyo ya TAA na TANU nilikuwa na akili zangu timamu hivyo ninayoandika kumuhoji Mohamed ni mambo ninayouhakika nayo!! Ndio maana huwa namtajia hata majina ya watu wa zamani walio hai ambao angeweza ku cross check nao pale panapokuwa na utata!
In actual fact nakubaliana na mambo mengi sana anayoandika Mohamed juu ya historia ya TANU tatizo ni pale anapoleta biases dhahili kwenye narration zake!!
Tupe bwana historia yake, hakuna nyaraka, picha na alikuwa na harakati zipi? Lete vitu bwana, kuwa.Mkristo pekee haitoshi. Si unaona Mohamed Said akiandika anatupa na nini walikifanya?Yupo mwingine anakaa Kata ya Majengo, anaitwa Mama Mwaipasi. Huyu ni Mmoja wa Wanachama wa TANU wa awali kabisa Mkoa wa Mbeya na ni Mkristo.
Maalim Faiza,Si ndio maana nikakwambia historia uliyotuletea wewe ni "bab kubwa" na haipo "biased" kabisa.
Halafu tupe kile kipande cha wazee wako walishiriki vipi katika kudai uhuru, na "roles" walizo "play" kabla ya Uhuru, maana ulibahatika na ulipendelea na Mwenyeezi Mungu (kama ulivyotujulisha juu hapo) kuwa wakati huo tayari ulikuwa una akili (bahati mbaya bwana umesahau kutueleza wakati upi) lakini huyu mohamed said analeta ya wazee wake toka kabla ya 1920s na wewe unayo ya wakati huo au upi? Funguka bwana. Tupe bwana. Na hiyo ya kuwa na akili bwana kisayansi ni "heredity" achana na huyo na u "bias" wake kakazania "wazee wangu wazee wangu". Tupe kidogo. Hata kama wazee wako walikua upande wa pili wa shillingi wewe lete tu usione haya.
Nasema upande wa pili, kwani lazima kama kuna "waliodai uhuru" basi kuna "waliodaiwa uhuru" na kuna waliokuwa upande wa wadai uhuru na kuna waliokuwa upande wa wadaiwa uhuru.
Sisi wazaliwa na wakulia Kariakoo bwana tunafahamu upande mmoja tu wa wadai uhuru na kule mission quarter tunafahamu kuwa ulikuwa upande wa wadaiwa uhuru bwana. Tunafahamu kuwa wote ya wasio Waislam walikuwa wasomi na wenye akili sana kwa hiyo walipewa kazi na wadaiwa uhuru na wengi wao wakawa upande wa wadaiwa uhuru wakiogopa maslahi yao.
Hata kama wewe ni wa upande huo wa walioogopa, tupe tu bwana/bibi Ndinani kwani lazima kuna pande mbili (heads na tails).
Wewe ni vitu adimu kabisa bwana, maana utakuwa unayajua ya "tails" siyo huyu anatuketea "heads" tu. Lete elimu bwana isiyokuwa "biased" isipotee bure ukazikwa nayo. Si unaona kina Sykes wamewaachia watoto nyaraka sasa ni kumbukumbu nzuri sana, hata wewe umeshauri arudi kwa Abbas Sykes akaulize! Au siyo bwana? Hivi wewe hauna wakumuuliza upande huo wa.pili ukatuletea hayi mamb9 bwana ili tumuweke sawa huyu Mohamed Said? Lazima na wewe utakuwa na mengi yako na ya wazee wa upande wako waliyoyaacha bwana. Haiwezekani wazee wa kariakoo na gerezani wasio wasomi kama hawa wa Mohamed Said wawe na nyaraka na mapicha na kumbukumbu. Na wasomi kama wewe na wazee wako msiwe na chochote cha kulipa taifa la leo kama kumbukumbu njema bwana.
Au umeleta bwana na sisi hatujaviona bwana?
Ndinani,
Miaka miwili iliyopita niliandika makala hii katika blog yangu ambayo ni fupi nikiomba mwenye taarifa ya mama huyu mzalendo atuandikie tupate kumfahamu ili tumuadhimishe pamoja na wapigania uhuru wengine:
BI. FATIMA MATOLA MAMA MPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA ASIYEJULIKANAMohamed Said Historia, Siasa na Maendeleo Tanzania October 14, 2017 0
Hapo chini ni nyumba ya Bi. Fatima Matola mwanachama wa TANU mazalendo aliyepigania uhuru wa Tanganyika.
Baba wa Taifa alikuwa akifikia nyumba hii wakati wa kupigania uhuru.
Nani keshapata kusikia jina hili la Bi. Fatima Matola?
Kuna hotuba ya Baba wa Taifa anasema kuwa safari yake ya kwanza baada ya kuundwa TANU mwaka wa 1954 alikwenda Mbeya.
Lakini Nyaraka za Sykes zinaonyesha kuwa safari ya kwanza ya Baba wa Taifa ilikuwa Mororgoro akifuatana na Zuberi Mtemvu.
Kuna barua ya tarehe 15 Agosti, 1954 mwezi mmoja tu baada ya kuundwa TANU kutoka kwa Mtemvu akimwandikia Ally Sykes, Mtemvu akieleza matatizo waliyoyapata yeye na Nyerere Morogoro katika kuitangaza TANU.
Hii ndiyo safari ya kwanza ya Baba wa Taifa katika kuitangaza TANU na safari ya pili ilikuwa Lindi.
Ikiwa safari hii ya Mbeya kwa namna yoyote ilikuwa ndiyo ya kwanza basi Baba wa Taifa alifikia nyumbani kwa Bi. Fatima Matola ambae nyumba yake ndiyo hiyo hapo chini kwenye picha.
Kuna mtu yeyote anaemfahamu shujaa huyu wa ukombozi atupe historia yake?
BI. FATIMA MATOLA MAMA MPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA ASIYEJULIKANA
Hapo chini ni nyumba ya Bi. Fatima Matola mwanachama wa TANU mazalendo aliyepigania uhuru wa Tanganyika. Baba wa Taifa alikuwa akifi...mohamedsaidsalum.blogspot.com
Unaweza kuingià hapo chini kwa taarifa zaidi:
Umuhimu wa kumbukumbu na nyaraka za Sykes katika kuijua historia ya Mwalimu Nyerere, TAA na TANU 1
UMUHIMU WA KUMBUKUMBU NA NYARAKA ZA SYKES KATIKA KUIJUA HISTORIA YA MWALIMU NYERERE, TAA NA TANU 1 Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika hotuba yake maarufu ya kuwaaga wazee wa Dar es Dar es Salaam aliyotoa Ukumbi wa Diamond mwaka wa 1985 alisema yeye alipelekwa nyumbani kwa...www.jamiiforums.com
Mohamed Said, mimi ninaheshimu sana kumbukumbu zako, maana unatuelimisha wengi.Dutu,
Wala hujakosea.
Ilikuwa si rahisi kuwatoa uani wanawake wa Kiislam miaka ile ukawaleta Mnazi Mmoja hadharani kwenye mikutano ya TANU.
Fundimchundo,Mohamed Said, mimi ninaheshimu sana kumbukumbu zako, maana unatuelimisha wengi.
Tatizo langu ni udini.
Tena Uislam.
Sijawahi kuona, humu JF, mtu au watu wakitambulishwa kama Wakristu.
Na kama wangetambulishwa hivyo, kwangu ingekuwa ni ukakasi ule ule.
Lengo lako la kutambulisha watu kama Waislam ni kuficha 'kabila' zao?
Wewe, Mohamed Said, ni kabila gani?
Lucy Lameck alikuwa mama wa Kichaga toka Moshi; Mohamed Said ni kabila gani toka wapi?
Au wewe ni mmoja wa wale wanaoona aibu kutaja makabila yao, kutokana na historia yao?
Ukristu na Uislam hauwezi kuwa 'identity' yetu sisi Waafrika.
Mohamed Said, mimi ninaheshimu sana kumbukumbu zako, maana unatuelimisha wengi.
Tatizo langu ni udini.
Tena Uislam.
Sijawahi kuona, humu JF, mtu au watu wakitambulishwa kama Wakristu.
Na kama wangetambulishwa hivyo, kwangu ingekuwa ni ukakasi ule ule.
Lengo lako la kutambulisha watu kama Waislam ni kuficha 'kabila' zao?
Wewe, Mohamed Said, ni kabila gani?
Lucy Lameck alikuwa mama wa Kichaga toka Moshi; Mohamed Said ni kabila gani toka wapi?
Au wewe ni mmoja wa wale wanaoona aibu kutaja makabila yao, kutokana na historia yao?
Ukristu na Uislam hauwezi kuwa 'identity' yetu sisi Waafrika.