Waliosoma shule za kata na kuumbuliwa na kiingereza tukutane hapa

Kiingereza kimenifanya nikakosa fursa nying sana

Kudadek mwalimu baba wa taifa hili kutuletea kiswaz
Usimlaumu huyo mtu, wazazi wako je? Shule ya msingi nilisoma enzi zake, ila haikunizuia nikiwa shule ya msingi kujua Kiingereza. Nyumbani kulikuwa na kamusi na vitabu vya hadithi vya Kiingereza, wachilia mbali unaweza upate neno moja au mawili kwa kumsikia au kumuuliza Baba au Mama.
 
Ni kiingereza hakitupendi watanzania? Hapana la hasha.

Ni sera zetu tu. Ooh lugha ya kikoloni, oo mbona China, Urusi na Ujerumani hivi na vile wanapita humo humo wameridhika sana.

Shule ya msingi darasa la sita na la saba niliyo soma haikuwa ya kata lakinl no chini ya usimamizi wa serikali.

Sikuwa na kamusi, lakino nilianzisha daftari langu natembea nalo saa 18/24/7 nilikuwa na hasira za kupitiliza kiingereza kinipende(msemo wetu mitaani)

Nikiona neno kwenye gazeti, au kitabu chochoye au tangazo katika ubao mfano NOTICE au DANGER (tukitamka dangeri) naandika katika ukurasa husika katika mfululizo wa A-Z kisha namuuliza baba au mama au mtu mzima yoyote, ajabu siyo mwalimu.

Darasa la saba tulifundishwa na mwalimu kutoka mfumo wa UPE.
Hakijui, hadi wanafunzi tulikuwa tunamcheka baada ya kipindi.

Akiingia na kitabu anaamrisha watoto tusome aya moja moja, hahahanui, harekebishi, ni sisi kukanyaga kanyaga hadi dakika arobani ziishe.

Nilichaguliwa kwenda sekondari. ilikuwa pia jitihada za baba kunotafutia wanafunzi ws sekondari wakati wa likizo kutupiga brashi mimi na dada yangu.

Nadhani bahati maswali ya kuchagua na kuoanisha pamoja na sala za mama zilisaidia. Ile siku tulippelekwa chumba cha mtihani kwa gari. Na kufungua kinywa kilikuwa kina mayai, enzi hizo wala mayai siyo wote. Katika darasa zima nilichaguliwa pekee, wilaya nzima 17.

Sekondari, kutafsiri notice nlitumia kamusi rasmi ilikuwa vituko maana maana ilizidi kunivuruga. Fikiria imeandikwa action and reaction are equal and opposite. Au biology is a branch of sience which is dealing with leaving things....nk

Haikuwa rahisi, nashukuru mwanafunzi form two aliona jitihada zangu mbinu alizo nipa ni pamoja na kuazima vitabu maktaba. Enzi hizo mwalimu wetu wa somo alitokea Dernmark akiwa mke wa mtaalamu katika chuo cha uvuvi.

Huyu naye alivutiwa na kiherehere changu katika kiingereza. Alinitia moyo nakunichagiza kuazima vitabu vyake vingi na alivitoa Kenya kujibu maswali darasani.

Form three na four mwalimu wa literature alikuwa ni Mganda. Kila wakati wa kipindi lazima niulizzwe chocho. Kwa mnao kumbuka Songs of Lawino, Weep not child., My dera bottle, No longer at easy nk hatari sana.

Shule olevel na A levell zilikuwa na matangazo Speak English only, lakini hakuna aliyesimamia hiyo kanuni.

Hata hivyo walimu wate darasani waliwasilisha mada kwa kiingereza. Masomo kwaa lugha ya Kiswahili ilikuwa no Kiswahili chenyewe na siasa.

Wale walioamua kukodoa macho na kufumba midomo kwa miaka minne, walivuna walicho panda.

Siku hizi naambiwa na wanangu huko vyuo vikuu kuna wakufunzi ni kumwaga Kiswahili mtupu, kisa wanafunzi hawana msingi bora.

Ukisikiliza hoja za wabunge wetu ni kama watu wa mitaani eti hii siyo lugha yetu, vijana huko nje hivyohivyo, na kila aina ya matusi, nani katuroga?

Hao watangazaji vijana katika vyombo vya habari wana haribu Kiswahili kila siku, wengine wamehitimu vyuo vikuu, penye R anaweka L, mara lisaa vurugu tupu.

Namudu Kiingereza kwa jitihada binafsi zaidi ya 60%. Katika miaka mitano ya kwanza utumishi wa umma nilisoma vitabu zaidi ya 300 na majarida yasiyo pungua 100.

Wito, serikali zetu kwa wakati wote, kuna mahali pa kuanzia. Kiswahili kipewe uzito wake lakini siyo dhambi hata mkulima alie ishia darasa la sita ikiwa ana mudu lugha ya Kiingereza.

Hii habari ya kusema mbunge ajue kusoma na kuandika Kiswahil lakini dereva wake angalau ahitimu form four nani mnawaogopa hapo.

Happa nisipotukanwa itakuwa ajabu sana na sikaribishi matusi.

Mungu ibariki Jamhuri ya Mmungano wa Tanzania.

AMEN.
 
Mwalimu mkuu alikuwa anatoa mawaidha pale paredi kuhusu wanafunzi waliojamiiana katika stoo ya shule akaaendelea na mwaidha (kwa kiingereza) alipofika mishoni akasema "Is there anyone who comment sex here at school apart from these two partners" nilinyoosha mkono kwa kudhani kuwa mwalimu alisema "leo aliyewahi saa kumi na mbili asubuhI ni nani shuleni kati yenu nyote"

Kilichonikuta sikuelezi baada ya knyoosha mkono.

holoholo Mbaga Jr Nomadix
Inasikitisha sana mkuu 😂
 
Mpaka namaliza la saba nlikua naweza kuhesabu ONE mpaka TEN tu nikifika kwenye eleven na twelve nazisahau kabisa af et leo mpumbavu anashouts shule za kulipia ni umasikini manina mwanangu hasomi kayumba abadani
 
Ni kiingereza hakitupendi watanzania? Hapana la hasha.

Ni sera zetu tu. Ooh lugha ya kikoloni, oo mbona China, Urusi na Ujerumani hivi na vile wanapita humo humo wameridhika sana.

Shule ya msingi darasa la sita na la saba niliyo soma haikuwa ya kata lakinl no chini ya usimamizi wa serikali.

Sikuwa na kamusi, lakino nilianzisha daftari langu natembea nalo saa 18/24/7 nilikuwa na hasira za kupitiliza kiingereza kinipende(msemo wetu mitaani)

Nikiona neno kwenye gazeti, au kitabu chochoye au tangazo katika ubao mfano NOTICE au DANGER (tukitamka dangeri) naandika katika ukurasa husika katika mfululizo wa A-Z kisha namuuliza baba au mama au mtu mzima yoyote, ajabu siyo mwalimu.

Darasa la saba tulifundishwa na mwalimu kutoka mfumo wa UPE.
Hakijui, hadi wanafunzi tulikuwa tunamcheka baada ya kipindi.

Akiingia na kitabu anaamrisha watoto tusome aya moja moja, hahahanui, harekebishi, ni sisi kukanyaga kanyaga hadi dakika arobani ziishe.

Nilichaguliwa kwenda sekondari. ilikuwa pia jitihada za baba kunotafutia wanafunzi ws sekondari wakati wa likizo kutupiga brashi mimi na dada yangu.

Nadhani bahati maswali ya kuchagua na kuoanisha pamoja na sala za mama zilisaidia. Ile siku tulippelekwa chumba cha mtihani kwa gari. Na kufungua kinywa kilikuwa kina mayai, enzi hizo wala mayai siyo wote. Katika darasa zima nilichaguliwa pekee, wilaya nzima 17.

Sekondari, kutafsiri notice nlitumia kamusi rasmi ilikuwa vituko maana maana ilizidi kunivuruga. Fikiria imeandikwa action and reaction are equal and opposite. Au biology is a branch of sience which is dealing with leaving things....nk

Haikuwa rahisi, nashukuru mwanafunzi form two aliona jitihada zangu mbinu alizo nipa ni pamoja na kuazima vitabu maktaba. Enzi hizo mwalimu wetu wa somo alitokea Dernmark akiwa mke wa mtaalamu katika chuo cha uvuvi.

Huyu naye alivutiwa na kiherehere changu katika kiingereza. Alinitia moyo nakunichagiza kuazima vitabu vyake vingi na alivitoa Kenya kujibu maswali darasani.

Form three na four mwalimu wa literature alikuwa ni Mganda. Kila wakati wa kipindi lazima niulizzwe chocho. Kwa mnao kumbuka Songs of Lawino, Weep not child., My dera bottle, No longer at easy nk hatari sana.

Shule olevel na A levell zilikuwa na matangazo Speak English only, lakini hakuna aliyesimamia hiyo kanuni.

Hata hivyo walimu wate darasani waliwasilisha mada kwa kiingereza. Masomo kwaa lugha ya Kiswahili ilikuwa no Kiswahili chenyewe na siasa.

Wale walioamua kukodoa macho na kufumba midomo kwa miaka minne, walivuna walicho panda.

Siku hizi naambiwa na wanangu huko vyuo vikuu kuna wakufunzi ni kumwaga Kiswahili mtupu, kisa wanafunzi hawana msingi bora.

Ukisikiliza hoja za wabunge wetu ni kama watu wa mitaani eti hii siyo lugha yetu, vijana huko nje hivyohivyo, na kila aina ya matusi, nani katuroga?

Hao watangazaji vijana katika vyombo vya habari wana haribu Kiswahili kila siku, wengine wamehitimu vyuo vikuu, penye R anaweka L, mara lisaa vurugu tupu.

Namudu Kiingereza kwa jitihada binafsi zaidi ya 60%. Katika miaka mitano ya kwanza utumishi wa umma nilisoma vitabu zaidi ya 300 na majarida yasiyo pungua 100.

Wito, serikali zetu kwa wakati wote, kuna mahali pa kuanzia. Kiswahili kipewe uzito wake lakini siyo dhambi hata mkulima alie ishia darasa la sita ikiwa ana mudu lugha ya Kiingereza.

Hii habari ya kusema mbunge ajue kusoma na kuandika Kiswahil lakini dereva wake angalau ahitimu form four nani mnawaogopa hapo.

Happa nisipotukanwa itakuwa ajabu sana na sikaribishi matusi.

Mungu ibariki Jamhuri ya Mmungano wa Tanzania.

AMEN.
Safi sana mkuu, penye nia pana njia.

Jitihada jitihada jitihada!
 
Mbona kasheshe wakati nipo Sec ,home Shy .Hili neno "Tobacco" lilinitoa jasho ,kila nikilisoma najikuta nimesoma Tombako.
 
Hovering brother uko poa?
Nipo brother Monetary doctor . Nashukuru sana kunialika hapa. Vipi Hali Yako ?
.
.
.
High school enzi hiyo tunapiga story na Mwl wa bioz. Kwenye story zake akaongelea umuhimu wa vyakula kundi la 'wanga'. Sikuamini jamaa mmoja alisimama na kuuliza 'wanga' ndio Nini na vyakula vya 'wanga' ndio vipi.

Ilikua ajabu kidogo kwa level Ile ukilinganisha Mdau aliuliza swali kwa Swahili language.
 
Nilipokuwa form One baadhi ya maneno nilikuwa naya-assume (najitengenezea) maana zake katika fikra zangu kwa sababu kiingereza lilikuwa hakipandi. Yafuatayo ni baadhi ya maneno ya kiingereza na maana nilizokuwa nilizoziunda kwa Kiswahili.

Let - Lete.
Pudenda - mpira unadunda.
Cook - kuku.
Sex - sita.
Common - pombe aina ya komon.
Come late - njoo ulete.
Lazy -mwizi.

Nitaongeza maneno mengine kadri nitakavyokumbuka. Kama umeshapitia hali kama yangu tuambie kama hujapitia kama Monetary doctor na Mshangazi dot com hongera.

Yote kwa yote kiingereza siyo kipimo cha akili.
Mimi nilikua na oxford dictionary ya English _ English ni hatare Sanaa 😊 😅

Mimi kimombo changu kinazungumzika na kipo Cha kiwango Cha SGR.

Kiingereza ni kuamua kujifunza na kusoma na kuandika na kumsikiliza na kukiongea ukiwa na phrase 100 + wewe automatically kiingereza kinakujaga chenyewe kabisa kabisa yaan.
 
Hongera mkuu. Ngoja nami niichukue hatua ili niwe totally fluent.
 
Back
Top Bottom