Waliowahi kupotelewa na ndugu au mtu wa karibu mje mtupe experience

Kwa mtu aliyewah kupotelewa na ndugu au mtu wa karibu aje atoe experience. Nikiona mtu anatangaza kupotelewa na ndugu ua nashikwa na uchungu sana mpaka najiuliza nduguze hali ikoje.
Mwenyezi Mungu atuepushie na mitihani ya namna hii.

Polen Sana mliowahi patwa na mitihani ya namna hii
 
Aisee kuna shida ipo ndani msikilizeni. kila mtu anapenda kuwa karibu na ndugu zake ila sasa kuna mambo ya ndani ndio yanafanya mtu unachukua maamuzi magumu
Ni tabia zake tu za kilast born hakuna shida serious, hajishughulishi na chochote hata ukimuuliza tu "utakaa hivi hadi lini dogo si ufanye kazi" yani hili ni kosa kubwaaaa mnoooo la kutosha kumfanya atoroke kwamba ananyanyasika.
 
Jamani,fanya kurudi nyumbani au kuwa na mawasiliano nao.
Mimi nina ndugu yangu amepotea miaka zaidi ya kumi ,yaani inauma jamani
 
Kuna maswali huwezi kukwepa hasa kutoka kwa mama. Unawajua mama zetu...
Utaishia kumuonea huruma unajikuta unarudi😀
Mie pia huwa napenda kukaa mbali na ndugu tutembeleane tu mara chache chache ila walau nawasiliano yawepo.....kukaa nao karibu huwa sitaki mambo ni mengi. Kukerana kwingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…