Wakuu niatanguliza salamu , baada ya Salamu naomba nitoe maelezo kidogo kuhusiana na nafasi ya spika wa bunge la Tanzania , halafu niingie kwenye mada.
Spika wa Bunge ndiye kiongozi wa Wabunge wote wa Tanzania , ndiye pia kiongozi wa Mhimili wa bunge , ambao una kazi ya kutunga sheria na kuisimamia serikali , kimsingi Spika ni mtu mzito , ambapo taarifa zinadai anaweza pia kuongoza nchi kwa kipindi fulani inapotokea sintofahamu yoyote kwenye nchi , Kwa maana hii Spika ni mtu muhimu
Baada ya utangulizi huo mfupi naomba sasa nianze kuwachambua Wagombea wa Nafasi hii kutoka ccm , chama chenye wabunge wote bungeni .
1. Mh Mwijaku
Huyu ni kijana wa mjini ambaye mtaji wake mkubwa ni mdomo wake , inasemekana ana elimu ya shahada kutoka UDSM , ni Mtangazaji wa redio ya clouds fm ya DSM kwenye kipindi cha Umbeya kiitwacho LEO TENA , ndani yake kuna kipengere kinachoitwa Heka Heka , wengi wanafahamu yanayojiri ndani ya kipindi hicho .
Mgombea huyu wa Uspika aliwahi kuwa mpiga debe wa timu ya soka ya Simba , ambako alitoa ahadi kabambe ya KUTEMBEA UCHI kwa umbali mrefu ikiwa Timu yake hiyo ingefungwa na Yanga , Simba ilifungwa na Yanga lakini kwa masikitiko Makubwa aligoma kutimiza ahadi yake ya KUSAULA hadharani .
Mgombea huyu anayepewa nafasi kubwa ya kuwa Spika wa bunge la Tanzania , kama anavyoonekana pichani
View attachment 2081040
Akiwa Mahakamani Kisutu , ambako alishitakiwa kwa kuweka picha za utupu/ngono mitandaoni , ambapo alirudishwa Rumande kwa kushindwa kulipa dhamana ya tsh laki 5 .
Note : Kazi ya kuchambua wasifu wa wagombea wengine inaendelea .
========
2.
3.
4.
5.