Ulikuwa wapi wewe na wana CHADEMA wote? Kwani hujaona Mbowe yupo peke yake na kubebwa tu nakwenda kupakiwa kwenye gari? Matapeli sana ninyi
Wewe mpuuzi una habari polisi walizingira nyumbani kwa Mbowe na kumbe hakuwemo humo.

Polisi wamezingira nyumbani kwa Lissu na wamemkamatia nyumbani kwake.

Kwakuwa una elimu ndogo na exposure yako ni ndogo ngoja nikuelimishe kuhusu Universal declaration of Human Rights hasa " article 13"

Everyone has the right to freedom of movement and residence within the borders of each state. Everyone has the right to leave any country, including his own, and to return to his country.
Nenda kajisomee hapo msururu wa sheria za kimataifa hao polisi wamevunja leo kumfurahisha Samia.

Sasa kama wewe unaunga mkono serikali inayokandamiza kisa unapewa $3 kumsifia Samia bado kama nchi mna safari ndefu.
 
Kwa hiyo na wewe ulilala kwa mbowe na hivyo kushindwa kuandamana? Wana CHADEMA wote mlilala kwa Mbowe na lissu? Kama mnajiamini kwanini hamkuandamana?
 
Mimi ningekuwa Mbowe ningeachana na siasa. Watu anaojitahidi kuwasaidia kujitambua katika kudai haki zao wala hawana habari, wanaendelea na shughuli zao.
Siku itafika watakapokuwa wamefikwa na maji ya pua na kuelekea kuzama, hakuna atakayewahimiza kujipigania wenyewe. Watajitokeza kudai haki zao kwa njia yoyote watakayoona inafaa.
 
Mbowe anapigaia Ruzuku na siyo Watanzania.
 
Kwa hiyo na wewe ulilala kwa mbowe na hivyo kushindwa kuandamana? Wana CHADEMA wote mlilala kwa Mbowe na lissu? Kama mnajiamini kwanini hamkuandamana?
Soma hoja zilizopo ujifunze.

Mbowe mwenyewe ndio kasema hakulala kwake au hukua na data za kuangalia video?

Mbowe gari zimezingira nyumba yake hata wanaopita barabara hiyo wanahojiwa na kukaguliwa , uko nyuma ya muda au unajitoa ufahamu?

Lissu kasems tangu jana usiku kuna gari 3 zimezingira nyumbani kwake , is that a police state?

Sasa kwenda kuwakamata watu majumbani mwao kuwa wameandamana ni sawa?,

Kwahiyo unataka kusema walikuwa wanaandamana sebuleni polisi ndio wakaenda kuwakamata kuwa wanaleta taharuki.

Tumia muda wako kusoma attachment niliyokupa , Kiingereza hakipandi au ?

Maana siamini muda mfupi tu huu umesoma article zote walizovunja polisi leo
 
Na wewe ulizuiliwa wapi? Wana CHADEMA wengine walizuiliwa wapi? Si mlisema mtaandamana hata wawepo Polisi? Imekuwaje mmekimbia na kumtelekeza Mbowe Peke yake?
 
Uongo lissu kashikwa,lema,familia mbowe na wengine acheni uongo
 
Na wewe ulizuiliwa wapi? Wana CHADEMA wengine walizuiliwa wapi? Si mlisema mtaandamana hata wawepo Polisi? Imekuwaje mmekimbia na kumtelekeza Mbowe Peke yake?
Onyesha post yoyote niliyosema nitaandamana humu.

Nasubiri .
 
Kwanini hamkwenda kuandamana? Si mlisema mtaandamana hata wawepo Polisi?
Nitie huko mie siko cgadema nimesema kura yangu na mpa Samia ya urais,ubunge act wazalendo udiwani ccm ,wenyeketi ,ccm so nitue huko ila penye haki nipo
 
Nitie huko mie siko cgadema nimesema kura yangu na mpa Samia ya urais,ubunge act wazalendo udiwani ccm ,wenyeketi ,ccm so nitue huko ila penye haki nipo
Hapo sawa nimekuelewa vyema kabisa .na hongera kwa maamuzi yako.
 
Mbowe anapigaia Ruzuku na siyo Watanzania.
Inawezekana ikawa kweli, mimi sina uhakika na hilo. Ila nyie mlioshika dola msijisahau na kuwapuuza wanyonge wanapolilia kupewa haki zao. Mkawaona hawana nguvu, wanaogopa kupigwa virungu na polisi na kufungwa jela. Kama mnataka kuendelea kuongoza dola kwa muda mrefu, basi watendeeni haki Watanzania. Wapeni stahiki zao, msiwabeze na kuwaumiza wale wanaowakosoa kwa haki.
 
1. 'Observation' yangu ilinipa picha tofauti na yako.
2. Mbele ya mtutu wa bunduki, kama mtu anashindwa kufanya jambo fulani kwa sababu anazuiwa na askari wenye silaha au wameziba njia huwezi kusema amesaliti au amegoma.
3. Hata hivyo, kwa wale waliojitokeza na kukamatwa - ni ishara kwamba si haba.
4. Labada kama ungechagua msamiati mwingine wa kutumia.
5. Ni unfortunate kutumia nguvu kubwa kiasi kile kuzuia wanasiasa wasio na silaha kuandamana kwa amani kuelezea hisia zao.
6. Kama polisi wenye silaha wangefanya hivyo kwa lengo la kuwasindikiza waandamanaji ili waandamane kwa amani bila bugudha, na kwa kufanya hivyo kama Wachadema wasingejitokeza kuandamana, hapo ndipo ungeweza kusema wamemsaliti au kumgomea mwekiti wao.
7. Je, unafikiri ingetokea siku ya uchaguzi polisi wakasema "atakaye kwenda kupiga kura huyo tunaye" halafu ikatokea siku chacke kabla na siku ya uchaguzi wenyewe makundi ya polisi wenye silaha wakatanda kwenye vituo mbali mbali vya kupiga kura wakiwakata watu wanaowahisi wanakwenda kupiga kura, katika mazingira hayo wapigakura wasipojitokeza, utaweza kusema wamesaliti kura yao na kugoma kwenda kupiga kura au utasemaje?
8. Bado sisi ni wachanga sana kwa demokrasia/kupigania haki zetu ingawaje miaka ya huko nyuma tulikuwa mfano kwa Afrika. Sifa hii tumejitahidi sana kuipunguza slowly, but steadly.
9. Kwa upande mwingine, kuwazoeza wananchi kuzoea silaha za moto hata mahali ambapo ni unnecessary is bad precedence.
 
Wameandamana polisi kwa kutumia Kodi zetu wanaCHADEMA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…