LGE2024 Wana JF mmejiandikisha? hizi ni faida za kujiandikisha kupiga kura

LGE2024 Wana JF mmejiandikisha? hizi ni faida za kujiandikisha kupiga kura

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Faida ya Mtanzania kujiandikisha kupiga kura katika uchaguzi wa viongozi wa Serikali ya kitongoji, mtaa, na kijiji ni pamoja na:

1. Kuchagua viongozi bora: Inatoa nafasi ya kuchagua viongozi wenye uwezo wa kuleta maendeleo na kushughulikia maslahi ya jamii.

2. Kuhakikisha uwakilishi wa wananchi: Kupitia kura, wananchi wanapata viongozi wanaowawakilisha kwenye maamuzi yanayogusa maisha yao moja kwa moja.

3. Kuimarisha demokrasia: Kushiriki kwenye uchaguzi ni sehemu ya kutekeleza haki yako ya kikatiba na kuimarisha demokrasia nchini.

Ndugu zangu, wakati wa kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ni huu. Hii ni nafasi yetu ya kuhakikisha tunapata viongozi bora watakaosimamia maendeleo ya jamii zetu. Fanya uamuzi sahihi, jiandikishe leo ili ushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi ujao

Mnasubiri nini???
Kwenye kuimarisha democrasia siamini kwa kuwa upo uoga mwingi wa kupoteza nafasi zinazo aminiwa ni za chama fulani au za watu fulani kwa manufaa ya kundi fulani kwa malengo ya wachache wa taifa hili.Hivyo ipo haja ya mabadiliko makubwa kuondoa dhana hii ,vinginevyo hili ni bomu linalo subiri muda wake.
 
Inawezekana uoni .....letme remind you

Suala la amani

Ujenzi wa miundombinu

Uboreshaji wa elimu

Uboreshaji wa kilimo

All this ni faida za viongozi Bora waliochaguliwa



Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Miaka 63 ya Uhuru tunaongelea tiny and petty things. Elimu imeboreshwa kivipi? Adui ujinga ndiye ameesclate.
 
Back
Top Bottom