Wana JF narudia tena, haribu kabisa tiketi au karatasi yenye taarifa zako kamili

Hapo kitakachomuokoa labda simu imuoneshe alikuwa wapi wakati huo.
Manaa tukio limetokea saa 9 alfajiri, keshatoka kwenye kazi zake za uwakala. Na anasema baada ya kufunga alijifungia ndani mpaka kesho yake alipofungua tena kibanda chake.
Mimi na wewe hatujui, tuwaachie polisi
 
Nj

Hizi Huwa ni njia dhaifu na za kivivu kwa askari vipi kama vocha imewekwa siku mbili nyuma alafu tukio likatoke siku mbili MBELE?
Kuna jamaa alihusishwa na mauaji kisa yeye ndiye alikuwa wa mwisho kuongea na marehemu, kuna watoto walifungwa baada ya kuokota simu zilizotupwa na jambazi aliyetekeleza mauaji maala flani.
 
Hao police nao itakua ni wendawazimu tu kwamba wahalifu waache kufanya uhalifu wao uliowapelek hayo maeneo waanze kuhangaika na kutia vocha kwenye simu au sio ? 😄
 
Hao police nao itakua ni wendawazimu tu kwamba wahalifu waache kufanya uhalifu wao uliowapelek hayo maeneo waanze kuhangaika na kutia vocha kwenye simu au sio ? 😄
Hapana, hajamaanisha hivo.
Kamaanisha kuwa jambazi anaweza okota vocha yako iliyotumika akaja kuiacha sehemu alikofanyia uhalifu ili msala ukuangukie wewe na si wao kuweka vocha.
 
Hamna kesi hapo na hajazingiziwa.kapiga deal katambaa na watu wakamtafuta.
Hizo tkt huwezi kuforge nk qr code na pin ambazo ni wewe utamiliki.
Kutupa ni kupoteza ushahidi pia.
 
Rafiki yangu si mtu wa kujichanganya sana na watu. Iwe usiku au mchana, akiwa ndani hujui na wala akienda kibaruani hujui.

Hatujui kama kweli kahusika au lah!

Sisi tunajua ahusiki ila binadamu hubadilika.

Ila maadam iko mikononi mwa jeshi la polisi tutajua tu hatma yake na wahusika halisi.
 
Oya mwanangu usiniambie ulimuacha bila hata vibao huyo nyang'au
 
Hapana, hajamaanisha hivo.
Kamaanisha kuwa jambazi anaweza okota vocha yako iliyotumika akaja kuiacha sehemu alikofanyia uhalifu ili msala ukuangukie wewe na si wao kuweka vocha.
Nimemuelewa vyema tu ila iyo vocha haitoshelezi kuwa ni kithibitisho cha ushahidi kuwa kweli mwenye vocha ndio amehusika na uwo uhalifu,

Kwa akili ya kawaida tu mhalifu hana uwo muda wa kuhangaika na kutia vocha kwenye cm yake tena sehemu ambayo amefanyia uhalifu.

Sema kwa nchi zetu za africa izi polisi wetu wapo nyuma san kweny mambo ya upelelezi lolote linawezekana kwa wao 🤣🤣
 
Umewahi kuchunguza karatasi zinazotumika kama mifuko kufungia vitafunio au kwenye maduka ya Mangi?
 
Kabisa, na hapo mpaka kujinasua ujue muda ushaenda sana tu
 
Kweli kabisa, kwenye nchi zilizoendelea kwa sayansi na teknolojia kwenye Matumizi ya kazi za kijeshi, jambo kubwa la Kwanza kabisa kulitekeleza ingekuwa ni Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kisayansi wa kupima DNA kuhusiana na hiyo ticket iliyookotwa ili kutambua ni Watu gani hasa waliohusika katika kuishika hiyo tiketi iliyookotwa katika eneo la tukio (scene of crime)? Majibu yangepatikana ndani ya muda mfupi kabisa usiozidi saa moja.
Lakini kwa kuwa Jeshi la Polisi la nchi hii bado linafanya kazi zake kwa mtindo wa Ujima Kama vile bado tupo kwenye zama za mawe za kale, Basi matokeo ya uchunguzi wao utakuwa Kama ni matokeo ya kutoka kwa mganga wa kienyeji katika zoezi la kupiga 'ramli chonganishi.'
 
Umewahi kuchunguza karatasi zinazotumika kama mifuko kufungia vitafunio au kwenye maduka ya Mangi?
Yaani zina full details za watu.
hizi bahasha nyeupe za karatasi kariakoo kwenye maduka ya vipodozi yaani ni hatari
 
Kabisa, yaani hapo pona pona yake sijui itakuwaje
Wenzetu kesi ingekuwa imeisha chap!!!
 
Na anasema walihisi walimpata kupitia Facebook, (mutual friend mmoja akatafutwa kisha akawaelekeza kwake).
Polisi wanaingia kwenye mfumo wa mawasiliano na kuangalia namba hiyo inafanya manunuzi gani, mfano, kulipa bill za maji au manunuzi ya LUKU, halafu wanatafuta mamlaka sahihi labda TANESCO nk wanapata exact location ya ilipo LUKU ndio unakuta hao wametimba kwako hata kama ni chaka kiasi gani.
 
Na hapo unataka police wasikushuku 😂 kama muhusika hadi kuzima simu kwanini yeye asireport police waarifu wanamtafuta hata kituo kingine basi kama si kikara😂
 

Mazingira yamamuonyesha Kama mhalifu
 
Sijawahi kuchukua karatasi ya ticket Kwa sababu kwenye simu inatumwa na ikihitajika ofisini Kwa sababu ya refund nina print
 
Ohh, kumbe.
Basi sisi tukajua hawa mutual wametumika kumlengesha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…