Wanachama UN wapiga kura mzozo wa Urusi - Ukraine

Wanachama UN wapiga kura mzozo wa Urusi - Ukraine

Ninaamini una uelewa wa kutosha. Usisikilize habari za vijiweni. Ukraine amefanya nini dhidi ya Russia? Nimekaa kidogo Urusi, Ukraine, Poland, na zaidi nchi za Magharibi.

Hivi unafahamu kuwa si mara ya kwanza Russia kuivamia Ukraine, na kufanya mauaji? Kwenye ule uvamizi wa mwanzo, Ukraine hakuwa member wa NATO wala EU.

Ukifuatilia, utajua wazi kuwa mataifa yale yaliyokuwa chini ya USSR, yalijitenga na Russia bila Russia kutaka. Baada ya kujitenga, Urusi ilitaka iendelee kuwa na mamlaka juu yake, na kuyaamlia nani awe Rais, nani awe rafiki yao, na nani awe adui wao. Katika members wote waliokuwa chini ya USSR, ukiiacha Russia, ni Ukraine ndiyo iliyo na potentials nyingi kuliko mwingine yeyote. Hali hii haimpi Mrusi amani. Na Ukraine baada ya kuumizwa na Urusi safari iliyopita, imekuwa ikihangaika sana kuingia NATO ili ipate hakikisho la kutoingiliwa na Urusi. Jambo ambalo Urusi haitaki. Urusi imekuwa ikitaka kuimega sehemu ya Ukraine ili kupunguza nguvu ya Ukraine. Na imefanya hivyo kwa kupandikiza makundi yanayotaka kujitenga na Ukraine, mashariki ya Ukraine.

Maisha ya raia wa Ukraine yanazidi kupotea, lakini lengo la Urusi halitafanikiwa. Marekani, China, pamoja na nguvu zote, waliishindwa Vietnam, ndivyo itakavyokuwa kwa Urusi.

Kwahiyo..!?
 
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepiga kura kwa wingi ya kuunga mkono azimio la kuitaka Urusi kusimamisha mara moja mashambulizi nchinUkraine na kuyaondoa majeshi yake yote, Mataifa 141 yameunga mkono azimio hilo dhidi ya matano ambayo yamepinga, kura hiyo iliyoitwa uvamizi dhidi ya Ukraine ilipigwa katika kikao cha dharura cha UNGA.

Je China ni ndumilakuwili??
Kwanini Eritria imejitoa ufahamu hivyo
 
Mzee kichwa cha habari ni cha uongo
35 zimepiga kura lakini zikawa neutral. Wewe ni mbumbumbu.
 
Safi sana, kuna vitaifa vichache vimeogopa, ila wengi wameunga mkono, anguko la Urusi limefika muda wake, Putin aliingia kwenye kumi na nane, na bado atakoma.
 
Safi sana, kuna vitaifa vichache vimeogopa, ila wengi wameunga mkono, anguko la Urusi limefika muda wake, Putin aliingia kwenye kumi na nane, na bado atakoma.
Vimeogopa au vimekataa kuwa bendera fuata upepo?
 
Hiyo spirit ingeendela kwa angalau miongo 2 au 3. Mtazamo wetu ungebadilika sana kuelekea jinsi tunavyojiona. Tunajiona dhaifu, maskini, vipofu na duni ndiyo maana "wale" wanafaidika na mtazamo huo. Ukiwa na mtazamo wa kujiamini, nani atakuamini. Ukijiona dhaifu nani atakufanya hodari. Ukijiona duni, nani atakuona unafaa na uko vizuri. Ukijidharau na atakuheshimu. Kila kitu kinaanza na wewe.

Akina china wanaweza, ni baada ya kuwa na mtazamo chanya kujielekea. Siku zote wanasema kwani wao waweze wana nini na sisi tushindwe tuna nini. Hawako kama watoto wa mama huyu ambao wanabaguliwa kule kwenye vita. Ambao mtazamo ni sisi ni wanyonge. Sisi ni wakushindwa tu siku zote.

Kila kitu kinaanza na wewe. Chukua hatua. Hayati JKNyerere aliwahi kusema, "hatubishi kwamba nyie mmepiga hatua ya kimaendeleo kutuzidi, lkn hilo haliwezi kuwa sababu ya kupuuza utu wetu na haki zetu". Hatuna pesa kama nyie, lkn tuna utu kama ninyi. That is dignity. Kujitambua utu wetu.
 
Wanafiki utawajua tu. Hakuna adui mbaya kama rafiki anayeshindwa kukutetea wakati unataabishwa. Anakuchekea mkiwa kwenye furaha, hasa anapokuwa na shida. Siku unasemwa vibaya, ama unashambuliwa na adui kwa namna yoyote anabunda!. Ni hatari sana kuwa na rafiki wa namna hiyo.
 
Hiyo spirit ingeendela kwa angalau miongo 2 au 3. Mtazamo wetu ungebadilika sana kuelekea jinsi tunavyojiona. Tunajiona dhaifu, maskini, vipofu na duni ndiyo maana "wale" wanafaidika na mtazamo huo. Ukiwa na mtazamo wa kujiamini, nani atakuamini. Ukijiona dhaifu nani atakufanya hodari. Ukijiona duni, nani atakuona unafaa na uko vizuri. Ukijidharau na atakuheshimu. Kila kitu kinaanza na wewe. Akina china wanaweza, ni baada ya kuwa na mtazamo chanya kujielekea. Siku zote wanasema kwani wao waweze wana nini na sisi tushindwe tuna nini. Hawako kama watoto wa mama huyu ambao wanabaguliwa kule kwenye vita. Ambao mtazamo ni sisi ni wanyonge. Sisi ni wakushindwa tu siku zote.
Kila kitu kinaanza na wewe. Chukua hatua. Hayati JKNyerere aliwahi kusema, "hatubishi kwamba nyie mmepiga hatua ya kimaendeleo kutuzidi, lkn hilo haliwezi kuwa sababu ya kupuuza utu wetu na haki zetu". Hatuna pesa kama nyie, lkn tuna utu kama ninyi. That is dignity. Kujitambua utu wetu.

Unasomeka mkuu. Tuliokimbia kura tuna ujasiri gani uliobakia?

IMG_20220303_145225_837.jpg

Au kwani Ndugai alikuwa kipi kakosea?

Zama za kina Nyerere kwenye usukani hazipo tena.
 
Mbona Marekani anapoanzisha matimbwili yake huwa hawapigi Kura..? Sisi tupo neutral hatutaki kuegamia sehemu moja wasituchoshe.
Ukapiga usipige wewe huzidishi chochote na hizo nchi ambazo hazikufungamana upande wowote zote kwa jumla tunasema ni vibaraka wa russia wacha tuone nguvu ya nchi 141
 
Ukapiga usipige wewe huzidishi chochote na hizo nchi ambazo hazikufungamana upande wowote zote kwa jumla tunasema ni vibaraka wa russia wacha tuone nguvu ya nchi 141
Tulia wewe
 
Ukapiga usipige wewe huzidishi chochote na hizo nchi ambazo hazikufungamana upande wowote zote kwa jumla tunasema ni vibaraka wa russia wacha tuone nguvu ya nchi 141
Tatizo wewe ni mshamba. Hilo azimio siyo la kisheria. Halina action plan yoyote. Baada ya kupiga kura ndio imeishia hapo mzee.

Hilo ni azimio la kuiomba Russia iache kuwapiga Ukraine. Unajua ombi linaweza kukubaliwa au kukataliwa.
 
Kumepigwa kura UN kuhusiana na nani ni nani kwenye uvamizi wa Ukraine.

Upande wa Russia kuna North Korea, Syria, Belarus na Eritrea.

View attachment 2137041

Kwa mujibu wa Tutu na bwana Martin Luther yumkini na sisi tumewakilisha:

View attachment 2137035

Source: NPR Cookie Consent and Choices
===

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wamekutana kwa dharura na kupiga kura za misimamo yao juu ya mzozo wa Russia-Ukraine unaoendelea kutikisa dunia.

Kura hizo ni mahsusi na ni azimio la kukemea vikali mashambuliz ya kibabe yanayoendelea kufanywa na Urusi dhidi ya Taifa la Ukraine, ambapo licha ya jitihada za usuluhishi kuanzishwa, bado vita hivyo vimeonekana kushika hatamu.

Hatua hii ni shinikizo baada ya Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy kuomba msaada wa kimataifa zaidi ya maramoja kwa lengo la kudhibiti vita hivyo ambavyo nchi yake imeonekana kuathirika zaidi ya mbabe wake Urusi kadiri siku zinavyosogea.

Nchi 141 kati ya 193 za UN zilipiga kura ya kuilaani vikali Russia na kuridhia kuwekewa vikwazo mbalimbali vya kimaendeleo na uchumi wake duniani kote.

Nchi tano hazikukubaliana na uamuzi huu; wao waliisapoti Urusi. Kati ya nchi hizo ni washirika wa Urusi ambao ni Belarus, Korea ya Kaskazini, Eritrea na Syria.

Nchi 35 hazikufungamana na upande wowote. Miongoni mwao ni nchi ya China ambaye ni rafiki mkubwa wa Urusi pamoja na Uganda.
Nchi 11 hazikushiriki (kupiga kura) kabisa.

Rais Zelenskyy wa Ukraine alishukuru nchi wanachama kwa kushiriki katika kura hizo, hasa zile zilizopiga kura za kulaani Urusi.
Vita vyao sisi hatufungamani na upande wowote ule. Non Alignment Movement (NAM) asili yetu toka zamani
 
Tatizo wewe ni mshamba. Hilo azimio siyo la kisheria. Halina action plan yoyote. Baada ya kupiga kura ndio imeishia hapo mzee.

Hilo ni azimio la kuiomba Russia iache kuwapiga Ukraine. Unajua ombi linaweza kukubaliwa au kukataliwa.
Mshamba mmako, Narudia lengo la hiyo kura ni kujuwa mnafiki ni nani na nani kama nchi yako ulipiga kuisaport russia jiandae na vikwazo respectively
 
Mshamba mmako, Narudia lengo la hiyo kura ni kujuwa mnafiki ni nani na nani kama nchi yako ulipiga kuisaport russia jiandae na vikwazo respectively
Jina tu ulilotumia linaonesha wewe low thinker. Je, una umri wa miaka mingapi!?
Wamewekewa vikwazo Zimbabwe na jamaa wanadunda tu. Wewe ni mshamba. Umuwekee vikwazo kwa kupiga kura!?!!

YOU ARE STUPID
 
Jina tu ulilotumia linaonesha wewe low thinker. Je, una umri wa miaka mingapi!?
Wamewekewa vikwazo Zimbabwe na jamaa wanadunda tu. Wewe ni mshamba. Umuwekee vikwazo kwa kupiga kura!?!!

YOU ARE STUPID
Waulize zimbabwe bei ya chapati 1 ni shilingi ngapi, lazima watakwambia ni shilingi elfu nane kwa chapati moja., tunasubiri hayo pia kwa russia baada ya mwezi toka sasa
 
Waulize zimbabwe bei ya chapati 1 ni shilingi ngapi, lazima watakwambia ni shilingi elfu nane kwa chapati moja., tunasubiri hayo pia kwa russia baada ya mwezi toka sasa
Mzee kwa maelezo haya wewe umezaliwa miaka ya 1990s wewe bado kinda.
 
Back
Top Bottom