Wanachama UN wapiga kura mzozo wa Urusi - Ukraine

Wanachama UN wapiga kura mzozo wa Urusi - Ukraine

Kumepigwa kura UN kuhusiana na nani ni nani kwenye uvamizi wa Ukraine.

Upande wa Russia kuna North Korea, Syria, Belarus na Eritrea.

View attachment 2137041

Kwa mujibu wa Tutu na bwana Martin Luther yumkini na sisi tumewakilisha:

View attachment 2137034

View attachment 2137035

Source: NPR Cookie Consent and Choices
Kulikuwa na kura ya kupigia Israel itsmbuliwe Kama nchi swala ambalo ni kinyume na taratibu za UN.. hawa wasituone si ma lofa bhana

Hii vita lawama zote ni kwa Mmarekani.. Kama kawaida yake anachonganisha alafu anakaa pembeni
 
Kulikuwa na kura ya kupigia Israel itsmbuliwe Kama nchi swala ambalo ni kinyume na taratibu za UN.. hawa wasituone si ma lofa bhana

Hii vita lawama zote ni kwa Mmarekani.. Kama kawaida yake anachonganisha alafu anakaa pembeni

Kwa hiyo kwa mawazo yako kwa kura yetu hii ya turufu tumemkomoa sasa Mmarekani?

Hatusomeki vyema pale kweli?

IMG_20220302_115525_094.jpg
 
Geneva, Uswisi (Jumatano, Machi 2, 2022)

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wamekutana kwa dharura na kupiga kura za misimamo yao juu ya mzozo wa Russia-Ukraine unaoendelea kutikisa dunia.

Kura hizo ni mahsusi na ni azimio la kukemea vikali mashambuliz ya kibabe yanayoendelea kufanywa na Urusi dhidi ya Taifa la Ukraine, ambapo licha ya jitihada za usuluhishi kuanzishwa, bado vita hivyo vimeonekana kushika hatamu.

Hatua hii ni shinikizo baada ya Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy kuomba msaada wa kimataifa zaidi ya maramoja kwa lengo la kudhibiti vita hivyo ambavyo nchi yake imeonekana kuathirika zaidi ya mbabe wake Urusi kadiri siku zinavyosogea.

Nchi 141 kati ya 193 za UN zilipiga kura ya kuilaani vikali Russia na kuridhia kuwekewa vikwazo mbalimbali vya kimaendeleo na uchumi wake duniani kote.

Nchi tano hazikukubaliana na uamuzi huu; wao waliisapoti Urusi. Kati ya nchi hizo ni washirika wa Urusi ambao ni Belarus, Korea ya Kaskazini, Eritrea na Syria.

Nchi 35 hazikufungamana na upande wowote. Miongoni mwao ni nchi ya China ambaye ni rafiki mkubwa wa Urusi pamoja na Uganda.

Nchi 11 hazikushiriki (kupiga kura) kabisa.

Rais Zelenskyy wa Ukraine alishukuru nchi wanachama kwa kushiriki katika kura hizo, hasa zile zilizopiga kura za kulaani Urusi.

DISCLAIMER: Katika ufuatiliaji wangu, sijaona nafasi ya Tanzania, ijapokuwa nimeona katika mitandao ya kijamii watu wakieleza kuwa Tanzania haikushabikia upande wowote.
 
Yasije kutukuta yaliyowakuta South Sudan🐒

 
Mbona marekani anapoanzisha matimbwili yake huwa hawapigi Kura..?
Sisi tupo neutral hatutaki kuegamia sehemu moja wasituchoshe.
... msome Archbishop Tutu and Rev. King Jr. hapo juu about what does neutrality or silence mean in such a situation (of injustice)!
 
Mbona unasimama na Israel dhidi ya Palestina na waarabu wengine wakati Marekani yuko nyuma ya Israel?!
Binafsi Mmarekani asingekua nyuma ya Ukraine ningesimama na Ukraine. Siwezi side na Ukraine wakati najua vita ni ya mmarekani.

Mungu mbariki mChina japo ana maudhi yake amejua kumkwamisha mmarekani kwenye mambo mengi ya uonevu
 
Kama nchi hatufungamani na upande wowote, ila wananchi mmojammoja wana maoni yao

Mungu Ibariki Tanzania

Mungu wabadilishe viongozi wa Russia na Ukraine mioyo yao watafute Suluhu nje ya vita
... in a situation of injustice; we can't say we are neutral or silent!
 
Baada ya corona kupotezewa na wanokulipa Naona umekuja Kwa mada mpya 😆😆
 
... msome Archbishop Tutu and Rev. King Jr. hapo juu about what does neutrality or silence mean in such a situation (of injustice)!
Hatuwezi kufanya maamuzi kisa tu kina fulani walisema nini!.. kukaa kimya nayo ni maamuzi.
 
Oppressor Ni nani Sasa katika mgogoro huu?!
If an elephant has its foot on the tail of a mouse and you say that you are neutral, the mouse will not appreciate your neutrality.” - Archbishop Tutu. Kwenye hili sakata bado hujaweza kutofautisha elephant na mouse?
 
Kama nchi hatufungamani na upande wowote, ila wananchi mmojammoja wana maoni yao

Mungu Ibariki Tanzania

Mungu wabadilishe viongozi wa Russia na Ukraine mioyo yao watafute Suluhu nje ya vita
Mungu ibariki pia chadema
 
Ni upuuzi mkubwa kwa Tanzania kushindwa kupiga kura kwa jambo lililo wazi ka hili. Ni aibu kubwa!!

Tanzania ya Mwalimu, haikuwahi kuwa na kigugumizi katika suala lolote linalohusu haki. Tulikemea kwa haki kuvunjwa, na tukapiga kura dhidi ya Israel pale Israel ilipowaua raia wakati wanawashambulia wapiganaji wa kipalestina, licha ya kwamba israel ilikuwa imetufanyia mambo mengi: kutujengea UDSM, mafunzo ya JKT, mafunzo ya makamanda wetu, na hata miradi ya kilimo.

Tusifikiri tupo salama sana kwa kujifanya popo. Tutasuswa na wote.
 
If an elephant has its foot on the tail of a mouse and you say that you are neutral, the mouse will not appreciate your neutrality.” - Archbishop Tutu. Kwenye hili sakata bado hujaweza kutofautisha elephant na mouse?

Akiweza kutofautisha usiache kutupatia mrejesho mkuu
 
Binafsi Mmarekani asingekua nyuma ya Ukraine ningesimama na Ukraine

Mungu mbariki mChina japo ana maudhi yake amajua kumkwamisha mmarekani kwenye mambo mengi ya uonevu
Kwa hiyo kwa sababu tu Marekani yupo nyuma ya Ukraine, ni heri kwako waendelee kuuliwa?
 
Back
Top Bottom