Sema ukweli buana. Huyo mrusi kamvamia Ukraine bila Ukraine mwenyewe kumchokonoa??
Ukraine wameingizwa mkenge na America
Na sasa America wenyewe wametulizwa na Putin haswa baada ya Kim na China kuwa wakweli
Mungu saidia marais wa Ukraine na Russia wapate mioyo ya huruma kwa watu wao na ufahamu wa kuwajua maadui zao
Ninaamini una uelewa wa kutosha. Usisikilize habari za vijiweni. Ukraine amefanya nini dhidi ya Russia? Nimekaa kidogo Urusi, Ukraine, Poland, na zaidi nchi za Magharibi.
Hivi unafahamu kuwa si mara ya kwanza Russia kuivamia Ukraine, na kufanya mauaji? Kwenye ule uvamizi wa mwanzo, Ukraine hakuwa member wa NATO wala EU.
Ukifuatilia, utajua wazi kuwa mataifa yale yaliyokuwa chini ya USSR, yalijitenga na Russia bila Russia kutaka. Baada ya kujitenga, Urusi ilitaka iendelee kuwa na mamlaka juu yake, na kuyaamlia nani awe Rais, nani awe rafiki yao, na nani awe adui wao. Katika members wote waliokuwa chini ya USSR, ukiiacha Russia, ni Ukraine ndiyo iliyo na potentials nyingi kuliko mwingine yeyote. Hali hii haimpi Mrusi amani. Na Ukraine baada ya kuumizwa na Urusi safari iliyopita, imekuwa ikihangaika sana kuingia NATO ili ipate hakikisho la kutoingiliwa na Urusi. Jambo ambalo Urusi haitaki. Urusi imekuwa ikitaka kuimega sehemu ya Ukraine ili kupunguza nguvu ya Ukraine. Na imefanya hivyo kwa kupandikiza makundi yanayotaka kujitenga na Ukraine, mashariki ya Ukraine.
Maisha ya raia wa Ukraine yanazidi kupotea, lakini lengo la Urusi halitafanikiwa. Marekani, China, pamoja na nguvu zote, waliishindwa Vietnam, ndivyo itakavyokuwa kwa Urusi.