Wanafunzi 22 wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Shinyanga kuzuiwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita 2021

Bhujegwe

Senior Member
Joined
Nov 23, 2013
Posts
135
Reaction score
191
Kuna taarifa kuwa Wanafunzi 22 wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari ya Shinyanga maarufu kama Shybush, wamefukuzwa shule na kuzuiwa kufanya mtihani wa kidato cha sita unaotarajiwa kuanza mapema mwezi wa tano.

Taarifa zaidi zinadai kuwa sababu kubwa ni fujo iliyotokea shuleni hapo mwezi March ambapo wanafunzi waliharibu gari la Mwalimu,na hivyo kupelekea bodi ya shule hiyo kukutana na kuamua wanafunzi hao wachukuliwe hatua hiyo.

Sambamba na hao,pia wapo wengine zaidi ya 30 ambao walirejeshwa makwao na wataruhusiwa kufanya mitihani yao wakitokea makwao.

Binafsi niwaombe wataalamu wa sheria wanisaidie ufafanuzi wa juu ya "Waraka wa Elimu No. 13" uliotumiwa na bodi ya shule hiyo kuondoa haki ya vijana hao kufanya mtihani na kupelekea vilio na majonzi kwa wazazi na walezi.
 
Nilikua mkorofi shuleni, nilikua nahamasisha migomo lakini baadae nilikuja kugundua kua ule ni ujinga na najuta sana ila nashukuru head master wangu kunihurumia hadi nikafanya mtihani na hadi leo niko huku na kazi yangu ya kuokota makopo na naipenda.

Utovu wa nidhamu shuleni hauna utetezi.

I feel sorry kwa hao watoto lakini ujinga na utovu wa nidhamu haukubaliki.
 
Duh!
Bro umeongea kwa hisia zote lkn unahitimisha kwa rungu la ajabu kiasi hicho. Uzuri umekiri nawe ulikuwa hivyo but hekima zikatumika kwako na ndiyo maana ulitoka. Ni vp huelekezi hiyo hekima kwa watoto wa wenziyo!!
 
Kisheria mwanafunzi akishasajiliwa ni lazima afanye mtihani awe mahabusu/magereza,hospitali au hajalipa Ada ya shule.Kama ni watovu wanidhamu na wamefukuzwa Shule wana haki ya kufanya mtihani.Awamu ya JPM ilibadili mambo mengi ngoja tuone.
 
Uongo
 
Huo waraka ulionao nenda nao kwa mwanasheria ili akufafanulie vizuri nadhani utakuwa umeelewa Cha kufanya ili usaidie warudi shuleni.
 
Kisheria mwanafunzi akishasajiliwa ni lazima afanye mtihani awe mahabusu/magereza,hospitali au hajalipa Ada ya shule.Kama ni watovu wanidhamu na wamefukuzwa Shule wana haki ya kufanya mtihani.Awamu ya JPM ilibadili mambo mengi ngoja tuone.
Mwanafunzi akishasajilwa kufanya mtihani lazima aufanye. Ni kanuni iliyowekwa na serikali miaka ya tisini ili kulinda haki za wanafunzi. Huko nyuma headmaster walijifanya Mungu watu na kuwazuia watahiniwa kwa baraka za bodi. Sasa hivi ikibidi wakati rufaa mara nyingi afisa elimu mkoa huwa ni watenda haki zaidi. Kama wakizubaa kanuni za life in the jungle zitatumika wazuiwe lakini nina imani mkuu wa shule atakayewazuia atabeba msalaba bodi ya shule itamruka arudi darasani uongozi ameshindwa.
 
Ndio iko hivyo mkuu enzi za Jk wakuu wa Shule na wenye Shule waliwekwa lupango kwa kuwazuia wanafunzi kufanya mtihani
 
Kisheria mwanafunzi akishasajiliwa ni lazima afanye mtihani awe mahabusu/magereza,hospitali au hajalipa Ada ya shule.Kama ni watovu wanidhamu na wamefukuzwa Shule wana haki ya kufanya mtihani.Awamu ya JPM ilibadili mambo

huwezi kulea wanafunzi wanao hatarisha amanj na usalama wa raia wengine eti kigezo tu lazima wafanye mtihani
Sina hakika
 
Nchi ina wanafunzi zaidi ya 30000 wanapiga paper wahangaike na 30??

Lazima ifikie mahali watu waheshimu mali za umaa
Wawapeleke mahakamani wahukumiwe mitihani watafanyia wakiwa jela au mahabusu.Sitetei uhalifu wa wanafunzi naangalia sheria na miongozo ya NECTA inasemaje
 
Back
Top Bottom