Bhujegwe
Senior Member
- Nov 23, 2013
- 135
- 191
Kuna taarifa kuwa Wanafunzi 22 wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari ya Shinyanga maarufu kama Shybush, wamefukuzwa shule na kuzuiwa kufanya mtihani wa kidato cha sita unaotarajiwa kuanza mapema mwezi wa tano.
Taarifa zaidi zinadai kuwa sababu kubwa ni fujo iliyotokea shuleni hapo mwezi March ambapo wanafunzi waliharibu gari la Mwalimu,na hivyo kupelekea bodi ya shule hiyo kukutana na kuamua wanafunzi hao wachukuliwe hatua hiyo.
Sambamba na hao,pia wapo wengine zaidi ya 30 ambao walirejeshwa makwao na wataruhusiwa kufanya mitihani yao wakitokea makwao.
Binafsi niwaombe wataalamu wa sheria wanisaidie ufafanuzi wa juu ya "Waraka wa Elimu No. 13" uliotumiwa na bodi ya shule hiyo kuondoa haki ya vijana hao kufanya mtihani na kupelekea vilio na majonzi kwa wazazi na walezi.