Wanafunzi wachoma moto pikipiki ya mwalimu, wafyeka shamba kisa adhabu ya kukutwa na simu shuleni

Wanafunzi wachoma moto pikipiki ya mwalimu, wafyeka shamba kisa adhabu ya kukutwa na simu shuleni

Ukisoma hii habari utahisi wanafunzi ndio wakorofi, mimi mpwa wangu anasoma pale form six na alinielezea A to Z ya nini kilichotokea.

Mimi mvivu sana kuandika lakini kifupi ni kwamba huyo mwanafunzi aliyesemekana kakutwa na simu, haikuwa ya kwake... Huyo mwalimu aliyechomewa pikipiki ndio alikuwa anamuadhibu kijana ili aseme simu iko wapi... Kifupi ni kwamba Mwalimu alimchapa vibaya mwanafunzi mpaka akazidiwa. Walimu wakaogopa kumpeleka hospitali kwa sababu hakukuwa na pf3.

Kituoni waliogopa maana wangetoa maelezo gani ili waeleweke. Ndipo ikabidi wamrudushe shule wakampa dawa ili atulize maumivu. Jioni mwanafunzi hali yake ikawa mbaya zaidi ndipo wanafunzi wengine wakaanza kushinikiza apelekwe hospitalini. Kukawa na mvutano kati ya waalimu na wanafunzi.

Yule mwalimu aliyetoa adhabu akawa anawatukana wanafunzi na kuwajibu jeuri. Wanafunzi wakapandisha hasira na mvutano ukawa mkubwa, Mwalimu mkuu alipata taarifa na kufika eneo la tukio. Akajaribu kuwasihi wanafunzi watawanyike atashughulikia lakini wanafunzi tayari walishapandisha hasira na chuki dhidi ya yule mwalimu, kwani inasemekana yule mwalimu amekuwa na tabia ya kupiga wanafunzi hovyo bila utaratibu na kuwatukana matusi.

Hiki ndio chanzo mpaka huyo mwalimu kuchomewa pikipiki na kufyekewa shamba lake. Haya ni maelezo mafupi tu ya nini hasa kilichotokea.
Walimu wengi ni hamnazo, stress za mishahara yao kiduchu wanamalizia kwa wanafunzi, wanakera sana msieeeew zao. Ndo maan wengi wako maskini wa kutupwa. Khaaaaah
 
Juzi kuna mwenyekiti wa chama cha walimu(cwt) wilaya nikamsikia anamsimulia mwenzie(kiongozi wa ccm) '' yaani nikamla .... kimasihara....''

Nikajua tayari uzi umeshafanya yake.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Heheh pamoja sikubaliani na utovu wa nidhamu Ila Hawa vijana ndio wa enzi zetu. Mwalimu akitaka kutoa adhabu alikuwa anajikagua mara mbili mbili maana anajua tukitoroka na tikakutana nae mtaani ajue ameumia.

Waliacha hadi kutufundisha eti tumekuwa watukutu na tukapasua almost wote wa mwisho alikuwa na 2.12 A level huyo ndio failure.

Ila Sasa tumeshakuwa watu wazima lakini mie Kama ni mwanangu hapo najua nimezaa dume sio Hawa wavaa kata K anakuja kuoa anapigwa makofi na mwanamke na anashangilia tu.
Umezaa jambazi badae linakuja kuwa jizi
Angekuwa na akili timamu angekinukisha bila kuacha alama
 
Hii comment watu hasa walimu wataipita kama hawaioni... Kiufupi huyo mwalimu hajaanza leo, mwalimu huyo anaukatili by nature kabisa na ninahisi ana matatizo kisaikolojia hadi huwa anakuwa hivyo

Wakati tupo sisi kipindi hicho alikua na visa kama hivi vingi na alikuwa ananusurika sana kupata hivi vipigo kutokana na matendo yake haya

hatukatai bylaws zetu za mashuleni zilizopitwa na wakati haziruhusu Wanafunzi kumiliki simu ila mwalimu huyu alikua anatake advantage ya hiyo sheria kwa maslahi yake binafsi.. alikua akipata taarifa kutoka kwa maspy wake ambao aliwaruhusu kumiliki simu ili kumpa taarifa kuhusiana na simu zilizopo mabwenini basi anakuja anachukua then anaenda ziuza kama ni iPhone au simu ambazo ni ngumu kubypass password bas atakupa kipigo hadi utoe password au umpe hela akurudishie simu yako

Hili ni fundisho kwa walimu wengine ambao wanafanya vitendo kama hivi vya Dhulma kwa kujifichia kwenye kivuli cha utaratibu na sheria za shule
Walimu wengi huwa wana huo mtindo wa kuchukua simu za wanafunzi na kuziuza nje. Wala sio kwamba wanazihifadhi sehemu ili baadae muhusika arejeshewe. Khaaah
 
hahahahahah yaani umeokoteza vi link uchwara kuja kunipinga hapa ni kiasi Gani unaonesha wewe ni zuzu first class wenzako Huko shule zimeunganishwa na Mifumo ya IT wewe unaniletea Link za mwaka 2003 Huko na Leo tupo 2022
Kiufupi endelea kujidanganya na kuleta ujuaji!
Ndugu kubali wewe ni mjinga tena mjinga sana,Tanzania hadi leo tunatumia katiba ya 1977 sasa eti wewe act ya mwaka 2003 unajifanya huielewi,

Swala Shule kuunganishwa na mifumo ya ki computer ni jambo moja na wanafunzi kutumia simu shuleni ni jambo jingine kama hata hilo imeshindwa kulitofautisha basi wewe ni tatizo sana
 
Kwa nini wa wanafunzi wa shule za sekondari hawaruhusiwi kuwa na simu shuleni?!
Kama hadi sasa hujui kwanini simu haziruhusiwi kwa wanafunzi wa sekondari basi wewe bado mdogo sana kifikra.

Na hiyo si kwa tanzania pekee bali mataifa mengi sana hawaruhusu hilo.
 
Jibu sasa kwa nini simu haziruhusiwi hata kwa wanafunzi watu wazima wa sekondari wa A-Level ili ukuze fikra zangu
Kama hadi sasa hujui kwanini simu haziruhusiwi kwa wanafunzi wa sekondari basi wewe bado mdogo sana kifikra.

Na hiyo si kwa tanzania pekee bali mataifa mengi sana hawaruhusu hilo.
 
aina hii ya wanafunzi ilipigwa fimbo za matako na chalamila,halafu wazazi wakachangishwa gharama kesi ikaisha.
wenye mtindio wa akili wakaloloma kwamba ni uonezi,sasa nategemea sheria ichukue mkondo wake,wafukuzwe shule,na gaharama zilipwe.
Naongezea; Na wakufungwa wafungwe.
 
Sheria za kipumbavu tu watu wapo smart world nyie mnaendelea kushikilia masheria ya kikoloni zama hizi wanafunzi wa secondary waruhusiwe kumiliki smart phone ziwasaidiek masomo Yao nchi nyingi tu hasa za Asia mfano Philippine,Hongkong,Thailand watoto wa sekondary kumiliki Simu ni kitu Cha kawaida tu Tena Zina msaada mkubwa sana huko ndiko kinakotoka kizazi Cha smart world wanajua Kila kitu wale sisi huku kijana wa Miaka 17 hajui hata kuwasha computer Wala hajui google ni Nini
Halafu ndio utegemee mageuzi ya kisasa Kwa Jamii kalagha bhaho
Tutaendeshwa na wachina na wahindi mpaka kiama!
Ndugu; Kila jambo na wakati wake. Wakati wa kuruhusu ukifika wataruhusiwa ila sio sasa. Hata wewe wakati halali wa kushiriki "tendo" ulipofika uliruhusiwa tena kwa sherehe. Lakini mwanzoni ulikuwa unakatazwa (japokuwa inawezekana ulikuwa unaiba-iba kwa kificho na tahadhari). Hebu pata picha ilivyo ck hizi. kwa mfano na iko hivyo; unakuta Watu wawili wanaofahamiana na wapo njiani wanaeleka kumoja lakini badala ya kuongea na kubadilishana mawazo utakuta kila mmoja kainamia cm kivyake huku wanatembea.... eti wana-chat na mtu fulani ambaye hayuko hapo. Ss pata picha ya mwanafunzi na simu yake akiwa darasani nini kitaendelea? na Mwalimu yupo ubaoni anafundisha.
Simu(smart phones) zinawaharibu sana watu(Vijana hata Wazee) e.g. kuangalia picha, Kucheza kamari, michezo mbalimbali n.k. bila kusahau utapeli mwingi.Kwa wanafunzi mambo hayo yanaathiri masomo yake. Kwani akisubiri amalize masomo kuna shida gani???
Wakiruhusiwa ; tukumbuke watakao wawezesha ni wazazi au walezi. Lakini Sio wote wana uwezo (Kifedha) kununua simu kwa mtoto au watoto wake lakini pia
kutakuwepo na matabaka ya wanafunzi e.g. wenye Smart phones na wale wenye vitochi - kitu ambacho huenda kitachochea Wizi, Unyanyapaa au hata Ushoga.
Kwa Mwanafunzi ni bora awe na msemo huu kama kauli mbiu yake: "Phones are not Oxygen that u cannot live without" . Full stop! akate miaka yake 4 O-level na 2A-level. Chuoni ni habari nyingine.
 
Mwenge Secondary kuna O Level? Huyo mwanafunzi aliyeadhibiwa n wa kidato cha 6.

Ila walimu wengine waache unoko na ukuda, japo sitetei kitendo kilichofanywa na wanafunzi hao. Msieeew
Pia usisahau kuwaambia wadogo zenu wasome kanuni za shule kwa Faida yao
 
Pia usisahau kuwaambia wadogo zenu wasome kanuni za shule kwa Faida yao
Najazia: Kwenye fomu ya Maelekezo ya kujiunga; ipo sehemu ya mzazi/mlezi kuweka saini kuonesha kwamba anathibitisha na atahakikisha kwamba atatoa Ushirikiano na Uongozi wa shule na Wizara kwa ujumla katika malezi ya mwanae.
Mara nyingi huwa hawazisomi au wakizisoma hawazielewi.
 
Najazia: Kwenye fomu ya Maelekezo ya kujiunga; ipo sehemu ya mzazi/mlezi kuweka saini kuonesha kwamba anathibitisha na atahakikisha kwamba atatoa Ushirikiano na Uongozi wa shule na Wizara kwa ujumla katika malezi ya mwanae.
Mara nyingi huwa hawazisomi au wakizisoma hawazielewi.
Tunafeli kwa kutokufanyia kazi maandishi huenda sawa zinaweza kuwa sheria zilizopitwa na Wakati Lakin hazijabadilishwa bado

Kutokutiii utotoni hata ukubwani tutachukulia poa hivi visheria vidogovidogo watu wanashuka na wewe jumla lawama Kwa shetani
 
Tunafeli kwa kutokufanyia kazi maandishi huenda sawa zinaweza kuwa sheria zilizopitwa na Wakati Lakin hazijabadilishwa bado

Kutokutiii utotoni hata ukubwani tutachukulia poa hivi visheria vidogovidogo watu wanashuka na wewe jumla lawama Kwa shetani
👍
 
Ndugu kubali wewe ni mjinga tena mjinga sana,Tanzania hadi leo tunatumia katiba ya 1977 sasa eti wewe act ya mwaka 2003 unajifanya huielewi,

Swala Shule kuunganishwa na mifumo ya ki computer ni jambo moja na wanafunzi kutumia simu shuleni ni jambo jingine kama hata hilo imeshindwa kulitofautisha basi wewe ni tatizo sana
wewe pia inaonekana ni mjinga sana Tena inawezekana ni wale first class,unadhani hizo simu nazozungumzia Mimi ni vitoch vya kuchatia?
Hapa nazungumzia simu zenye devices za internet Ili kuwezesha masomo kiurahisi tatizo lako una fikra za kizamani sana,
Ninao mfano hai wa mdogo Wangu aliyepo mkoani
Yupo kidato Cha 4 now na alianza kumipiki simu yupo kidato Cha pili
Dogo alikua slow Kwenye masomo yake mpaka Kuna muda alitaka aache shule ila alivyojua kutumia smart phone alianza kujifunza vitu vingi vya faida Kwenye masomo kitu kilicho mfanya awe updated sana na Dunia
Hua anakili kabisa Bila simu Kwa nature ya shule za kata zilivyo asingetoboa
Hata Mimi Kuna muda hua najilaumu Kwanini nilikua nyuma ya wakati endepo ningeanza kumiliki device Yenye internet kipindi nasoma ingenisaidia sana
Maana baada ya kuhitimu kidato Cha nne ndani ya miezi michache niliyokua kitaa na simu janja nilijifunza mambo makubwa na chanya ndani ya muda mfupi sana ambayo hata Wewe najua huyajui na huo ukubwa wako!

Grow up dude Dunia ipo Kwenye mabadiliko wewe endelea kutetea ujinga!

Hovyo kabisa halafu Ndio fikra kama zako zisaidie kuifikia Tanzania ya maendeleo ya science na Teknolojia Kwa Akili kama hizo thubutu

Endelea na Marufuku Kwa Kila kitu Cha faida wakati wenzenu wapo hatua mia Moja mbele Yenu!
Shwain!
 
Ila haya mambo ya simu kwa Wanafunzi serikali inabidi waangalie tena sababu za kuwakataza simu wanafunzi. Things have changed.... waweke utaratibu rasmi tu wa matumizi ya simu hasa katika shule za boarding kwa A-level.



Mwaka 2012 tulishawahi fanya kama hao wanafunzi ilikua Iyunga Tech Mbeya ofisi ya Mwalimu wa Nidhamu tuliijaza maji na nyumba yake ikapigwa mawe usiku kucha. Kisa ilikua issue hii hii ya simu.

Ila yule Mwalimu alikua Snitch sana.
 
Ila haya mambo ya simu kwa Wanafunzi serikali inabidi waangalie tena sababu za kuwakataza simu wanafunzi. Things have changed.... waweke utaratibu rasmi tu wa matumizi ya simu hasa katika shule za boarding kwa A-level.



Mwaka 2012 tulishawahi fanya kama hao wanafunzi ilikua Iyunga Tech Mbeya ofisi ya Mwalimu wa Nidhamu tuliijaza maji na nyumba yake ikapigwa mawe usiku kucha. Kisa ilikua issue hii hii ya simu.

Ila yule Mwalimu alikua Snitch sana.
Pamoja na Usnitch wake lkn Mchango wake kwako kukubalika na jamii ni mkubwa,asingekuwa snitch inawezekana leo hii ungekuwa mtu wa hovyo sana.
 
Back
Top Bottom