MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 21,387
- 44,030
Lengo la maandamano ni watu kutoa maoni yao kwa kile wachoona wanastahili kukisemea. Ni namna moja ya wapo ya watu kuelezea hisia zao kwa mujibu wa katiba. Kuna maandamano kwa ajili ya kupinga au kupongeza jambo fulani. Maandamano hayahusishi uhalifu wowote.
Kwenye maandamano ya wiki iliyopita yalikuwa ya amani dakika za mwanzo lakini kadiri muda ulivyoenda yakageuka na kuwa uhalifu. Waandamanaji wakaanza kuharibu miundombinu na kuchoma mali za watu binafsi na umma. Ulikuwa uhalifu wa kutisha. Kwenye uhalifu lazima dola ichukue hatua dhidi ya wahalifu. Hatua zinazochukuliwa huendana na uzito wa uhalifu. Mwizi wa kuku hawezi kutendewa sawa na aliyeshika kidumu cha petroli na kuanza kuchoma kituo cha mafuta. Huyu wa kidumu cha petroli lazima atakutana na nguvu kubwa dhidi yake ikiwemo kupelekwa kuonana na mizimu ya kwao.
Binafsi ninawalaumu wanaharakati Mange, Maria, Lord Denning na Sativa kwa kuhamasisha uhalifu. Hawa watu wanne kabla na wakati wa maandamano walitumia muda mwingi sana kuhamasisha uhalifu. Damu zilizomwagika zitawalilia maisha yao yote.