Wanajeshi wa Tanzania takribani 2000 walifyekwa na majeshi ya Idd Amin; huo ndio ulikuwa mwanzo wa vita ya Kagera

Wanajeshi wa Tanzania takribani 2000 walifyekwa na majeshi ya Idd Amin; huo ndio ulikuwa mwanzo wa vita ya Kagera

Hamna mtu asiyefanya makosa na hivyo hata Gadaffi alikuwa na makosa yake. katika kumtathmini kiongozi lazma ulinganishe mazuri na mabaya yake na kwa kuzingatia hilo hamna kiongozi kama Gadaffi barani Afrika na itachukua muda mrefu kupata kiongozi kama Gadaffi. he's the true African hero
Unajua jinsi Gaddafi alivyoua wananchi wake mwenyewe?
 
Babake wa taifa amekufa na siri nyingi
 
Mkuu hata mimi uwa napata ukakasi kuamini aliyosema mwalimu kwamba "tumepoteza vijana 395 na raia wasiopungua 1500" kwa nature ya ile vita watu wengi na askari walipotea, ukiangalia strength ya tanzania kulikuwa na askari "troops" wasiopungua 150'000~250'000, (hapa chukua na UNLA ya Mseveni plus wale askari kutoka Mozambique, China na Cuba) wakt waganda awakuwa na zaidi ya askari 70'000 ukijumlisha na Libya zaidi ya 500, na bado vita ilipiganwa zaidi ya miezi 10 mpk ushindi kupatika

Hapa nahisi yafuatayo......

1. Uenda idadi hii 395 ni idadi ya askari waliokufa vitani na sio idadi ya wale mgambo,JKT,UNLA,polisi na washirika kwani mwanzon zile platoons zaidi ya 10 zilizotaka kuvuka mto kupitia mitumbwi zilimiminiwa mizinga na kupotea kabisa kiasi cha kamanda wake kuondolewa mstari wa mbele na daraja kuvunjwa rasmi

2. Hii vita ilkuwa ngumu kweli kweli kutoka na kupiganwa kipindi cha masika na ile misitu minene na mapoli ya Uganda kiasi cha kupoteza askari wengi sana

3. Vita hii wakati mwingine ulihitajika uzalendo kwan kizana waganda walikuwa mbali kivifaa kuna wakati vita ilichachamaa esp katika utekaji wa mbalala na entebbe kiasi cha askari frontline ku retreat bila mpangilio wengin walkimbia mpk bukoba mjini mpk kupelekea msuguri kuonelea askari wote wavuke daraja kisha livunjwe ili wasipate pa kupitia na kazi ya kujijenga upya kuchukua wiki tatu

5. Uenda kuna stori inafichwa makusudi na kwa mtu ambaye ana ubongo ili ni muhimu zaidi na ufanywa makusudi
Naungana na ww mkuu.. Nimewahi kukisoma kitabu cha siri cha vita ya Uganda... Kilikuwa kimeandikwa kwa lugha ya tarakimu... Mfano Neno kama basi liliandikwa 52III2 ...aisee kile kitabu hakijaficha kitu chochote, wameelezea jinsi tulivyopigwa pale mpkani.. Tulipoteza mgambo na waalimu wa shule za msingi zaidi ya 2000 , maana walipewa mafunzo ya wk 3 tu... Migambo na waalimu ndo walitangulizwa mstari wa mbele... Mwalimu nyerere ile Vita alilazimishwa na makamanda waliokuwa ktk hvyo vikosi uchwara vya waalimu na migambo.. Baada ya kusaini nyerere akaenda kutangazia hiyo Vita ktk mji wa songea.. Aisee anayebisha acha abishe tu lkn tulipigwa mnoo japo baada ya hapo tulijitahidi kwa msaada wa bomu stera lililofumua mlima ambao ulikuwa machinjio ya wanajeshi wetu... Baada ya kuufumua ule mlima ndo tukapata nafuu ya kusonga mbele... Watu hawajiulizi kwnn mtangazaji Ben kiko alirudishwa dar, alikuwa anatangaza kana kwamba anatangaza mpira wa simba na yanga... Bomu la stera tulisaidiwa na wachina.. Lile Bomu liligeuza mlima na kuwa tambalale askari wengi wa Idd amin waliishia pale... Na kingine akina mseven walitusaidia sana kutuonyesha sehemu muhimu za kupiga... Ukisoma kile kitabu ndo utajua jinsi gani vita ilikuwa ngumu kwetu.. Tulikuwa na vifaru vya minyororo wakat Amin yy alikuwa na vifaru vyenye matairi na vina speed kubwa kuliko vyetu... Tulipoteza wanajeshi wengi mnoo kwa umalaya pia... Wanajeshi wa Uganda waliwatumia wanawake kama chambo kuwaua wanajeshi wetu... Anyway anayebisha kuwa hatukupoteza wanajeshi anahitaji kusamehewa tu maana hajui kitu
 
Hili jambo ni kweli nilishawahi kusimuliwa na Mjomba wangu ambae alikuwa kwenye vita hivyo.ata kuwawa Kwa Mtt Wa nyerere ambaye alikuwa rubani ni kweli kabisa
 
Kwa hali hii jeshi letu lilikuwa na viazi wengi sana.
 
Habari kwenu jukwaani.

Kuna simuluzi BBC Radio wanatujuza historia iliyofichwa. Mwanzoni mwa vita vya Kagera ni kuwa baada ya Amini kufanya uvamizi wake, Tanzania ilitanguliza kikosi cha wanajeshi 2000 mstari wa mbele na chote kilifyekwa na majeshi ya Amin.

Baada ya hapo jeshi letu lilijipanga upya na kusonga mbele hadi Kampala na Jinja ambapo Idd Amin alitimkia Libya na baadae Saudi Arabia.

Hii historia sijiwahi kuisikia, nilijua tulipigana bila upinzani mkali na hatukupoteza askari wengi kiasi hiki kwa mpigo mmoja.

Msimuliaji pia anadai jeshi la Uganda lilikuwa limegawanyika sana kwani baadhi hawakumtaka Amin aendelee kuongoza Uganda na hivyo kulisaidia jeshi letu lililojipanga upya kushinda vita hivyo.

Viva JWTZ.

VITA VYA KAGERA!
Kama jinsi vilivyofahamika Vita vya Kagera (1978-1979). Vita vya Takkribani Mwaka Mmoja na Miezi Kadhaa,viliingiza Tanzania katika hali mbaya ya kiuchumi ambayo iliharibu ustawi wa Taifa letu kwa kiasi kikubwa sana!
Nisichoshe watu naomba na mie nitoe dondoo (Zilizoleteleza Vita) nilizojifunza kutokana na Vita hivi kama ifuatavyo:-
  • Ni vita ambavyo Nyerere alijaribu kuviepuka kidiplomasia lakini vilishindikana kabisa; Alienda OAU akawaomba walaani vitendo vya Alhaji, Field Marshal,Black Hitler,CBE The Life President of Uganda. IDD AMIN anavyovifanya vya Uvamizi na tishio la Vita dhidi ya TZ,Mashirika mbalimbali ya kimataifa yalikaa kimya juu ya ombi la Nyerere Kuwataka Wapaze sauti isikike duniani - Aliomba tu Jumuiya za Kimataifa ZIMRAANI AMIN na UZUSHI WAKE DHIDI YA TZ.

  • OCD wa Bukoba Hans Pope (Chotara wa kijerumani) aliuwa( alikuwa kwenye doria mpakani) na Maiti yake kutembezwa Kampala, na Nchi ya Uganda kutangazia kuwa Nyerere alikuwa anajiandaa na vita na tayari alishaleta Askari wa Kichina TZ.(uzushi).
  • Amin alidai eneo la mto kagera ni ardhi ya Uganda.(uzushi)
  • Comrade Cho Enlai (Waziri wa Ulinzi na Mambo ya Nje ya china) alimpigia simu Nyerere akamwambia usipigane vita na Uganda;Amin amejipanga na anasubiri uingie mkenge akutandike.
  • IDD AMIN alikuwa ameahidiwa siraha nzito mbalimbali na nchi kadhaa za nje (Uingereza,Urusi pamoja na Israel).
  • Idd Amin alifanikiwa kupata siraha nyingi toka urusi na Libya.Hivyo Amin alikuwa amepania Kupigana Vita.
  • Wakati huo Uganda ilikuwa ikitawaliwa kama DEEP STATE - Yaani Vyombo vya ulinzi na Usalama ndio vilitawala Uganda na mitaa yake.
  • SRB (State Research bureau) shirika la Ujasusi la Uganda lilishika hatamu ya ushauri na uongozi wa Nchi chini ya Amin,likitesa na Kuua raia na watu waliodhaniwa kuwa ni adui wa Amin.
  • Frank Terpil dalali mbaya sana aliyemtafutia Kila kitu alichokitaka Amin toka Ulaya na marekani,Huyu jamaa alikuwa kiungo kiovu katika siasa za Uganda kwa wakati ule.(siraha,magari ya kifahari na vitu vingine vya starehe).
  • inasemekana Wanafunzi Saba toka UDSM waliuwawa kinyama Uganda walipokuwa wamekwenda Field Katika Shirika la Mawasiliano la Afrika Mashariki(East African telecominication headquarter ilikuwa Uganda kabla ya shirikisho kuvunjika 1977).
  • Waziri Mkazi wa nchini Uganda wa TZ ndg. Ahmed Shekilango alikufa Ghafla baada tu ya kuongea na Nyerere kuhusu jambo ambalo mpaka leo hatujui ilikuwa ni nini na alitaka kuja kuonana na mwl. kumweleza nini?
  • Wakati huo Milton Obote akipata hifadhi ya ukimbizi nchini Tz,Uganda ilitaka sana Obote arudishwe Uganda kwa Amini(extradition) Kitu ambacho TZ ilikataa kata kata chini ya Waziri wa mambo ya Nje Dr. John S. Malecela.Ndugu Malecela alimuapia Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Joshua W. Kibedi (shemeji wa Amin) akamwambia kuwa hata yeye anaweza kuwa mkimbizi wakati wowote ule hivyo hajui anachoomba kwa TZ,Kwani Ukimbizi ni Haki ya kiraia. Kweli baada ya miezi michache Kibedi alikimbia Uganda.
  • Somalia nchini ya"Dikteta" Siad Bare alikuwa msuluhishi wa Mgogoro kati ya Uganda na Tz.
  • Askofu Mkuu wa Anglican nchini Uganda auawa kinyama - Bishop Janan Luwum (inasemekana aliuwawa na Amin kwa mkono wake mwenyewe - Janan Alikemea Vitendo vya Kidikteta hadharani Amin hakupendezwa na hilo)
  • Wakati chokochoko hizi zinaendelea hapa nchini mambo hayakuwa Shwari sana,jeshi letu pendwa lilikuwa Kusini mwa Tz kusaidia harakati za Ukombozi hasa Mozambique(1970s).
  • Nyerere alitafakari sana akakonda mno!Aliiona Uganda inataka kuwa nchi ya Ajabu -Udikteta sio Kitu kizuri - Nyerere akaapa kwamba hataruhusu Uganda Martyr (historia inaeleza vizuri sana juu ya hili)Ingine itokee Uganda akafunga kwa maombi kanisani siku tatu,akainuka na Maneno - NIA,UWEZO NA SABABU.
  • Tanzania ikaingia Vitani rasmi Mwaka 1978 ( Inasemekana ni kwa taarifa za Kijasusi zilizokusanywa na Mashushushu wetu huko na kwa Maelezo binafsi ya baadhi ya Maaskari wa JW waliomjua Amin vizuri(General Msuguli).
  • Vita ni Vita tu - casultes of war huwa hazitamaniki kabisa sio kwa upande wowote ule.
  • Inasemekana takriban US Dollars 508,000/- zilipotea kutokana na Vita hivyo! ni Zaidi ya hela ambazo hata wafadhili wa nje wasingeweza kutupa sisi kirahisi rahisi.
  • Idadi ya waliopoteza maisha(Askari) Vyanzo nilivyopitia vinadai si chini ya Askari 300.
  • Baadhi ya Makanda waliotutoa Kimasomaso ni Lt.Col. Ben Msuya (Huyu Jamaa hakuna askari hata mmoja aliyekufa kwenye Battalion yake) Alipokuwa Uganda alivaa Rain boot Nyeupe na Mkuki - aliongoza kuteka kituo cha redio Uganda.
  • Abdalla Twalipo,Yusuph Himid,Herman Lupogo,Nshimani,Roland Chacha,Major Musuguli,Tumainieli Kiwelu,Mirisho Sarakikya,Walden,Marwa,Silas Mayunga,James Luhanga na wengineo wengi.
  • Natunaimini nimeelezea kidogo na mimi hapo.Asante
War may sometimes be a necessary evil. But no matter how necessary, it is always an evil, never a good. We will not learn how to live together in peace by killing each other's children.- Jimmy Carter.
 
Nitajie kiongozi wa Afrika ambaye hajaua mwananchi wake yoyote, tuanzie hapo kwanza.
Kama viongozi wote wa Afrika wanaua wananchi wao, hiyo ni sababu zaidi ya kukemea kiongozi yeyote wa Afrika anayeua wananchi wake, akiwamo Gaddafi.

Two wrongs do not make a right.

Magufuli akitaka kukuua wewe leo kwa sababu Kagame kaua Wanyarwanda utafurahi na kukubali na kusema hakuna kiongozi wa Afrika ambaye hajaua wananchi wake?
 
Ok, sikumaanisha mauaji yanakubalika ninachomaanisha mimi hamna kiongozi aliye perfect na haitakuja kutokea. Hivyo basi kiongozi bora lazma mazuri yake yafunike mabaya yake thats the logic. Kama kuna kiongozi aliye perfect naomba unitajie labda mimi siifahamu dunia vizuri
 
Sasa una hakika gani Gaddafi mazuri yake yamefunika mabaya yake?

Mtu akikuua wewe kuna mazuri yake yatakayofunika mauaji yake kukuua wewe?
 
Huu ni uchochezi Tanzania atujawai kufiwa na mwanajeshi hata mmoja acheni uchochezi awamu ya tano huyu mzee tutamtumia Uhamiaji kwanza na TRA
 
Habari kwenu jukwaani.

Kuna simuluzi BBC Radio wanatujuza historia iliyofichwa. Mwanzoni mwa vita vya Kagera ni kuwa baada ya Amini kufanya uvamizi wake, Tanzania ilitanguliza kikosi cha wanajeshi 2000 mstari wa mbele na chote kilifyekwa na majeshi ya Amin.

Baada ya hapo jeshi letu lilijipanga upya na kusonga mbele hadi Kampala na Jinja ambapo Idd Amin alitimkia Libya na baadae Saudi Arabia.

Hii historia sijiwahi kuisikia, nilijua tulipigana bila upinzani mkali na hatukupoteza askari wengi kiasi hiki kwa mpigo mmoja.

Msimuliaji pia anadai jeshi la Uganda lilikuwa limegawanyika sana kwani baadhi hawakumtaka Amin aendelee kuongoza Uganda na hivyo kulisaidia jeshi letu lililojipanga upya kushinda vita hivyo.

Viva JWTZ.
VIJANA WA BRIGADIER HIMID ....lakini hawakufika idadi hiyo ??wengi walikimbilia Bukoba mjini kuliko waliokufa
 
Habari kwenu jukwaani.

Kuna simuluzi BBC Radio wanatujuza historia iliyofichwa. Mwanzoni mwa vita vya Kagera ni kuwa baada ya Amini kufanya uvamizi wake, Tanzania ilitanguliza kikosi cha wanajeshi 2000 mstari wa mbele na chote kilifyekwa na majeshi ya Amin.

Baada ya hapo jeshi letu lilijipanga upya na kusonga mbele hadi Kampala na Jinja ambapo Idd Amin alitimkia Libya na baadae Saudi Arabia.

Hii historia sijiwahi kuisikia, nilijua tulipigana bila upinzani mkali na hatukupoteza askari wengi kiasi hiki kwa mpigo mmoja.

Msimuliaji pia anadai jeshi la Uganda lilikuwa limegawanyika sana kwani baadhi hawakumtaka Amin aendelee kuongoza Uganda na hivyo kulisaidia jeshi letu lililojipanga upya kushinda vita hivyo.

Viva JWTZ.
Uongo uongo uongozi[emoji12]
 
Hiyo simulizi haina ukweri wowote,Kwa kipindi kile 1979 kama Tanzania ingepoteza asikari 2000 ndo ingekuwa mwanzo wa kushindwa vita,naiman miaka hiyo JWTZ ilikuwa na asikari wachache sana,japo hata Jeshi la mgambo lilishiriki katika Ops hiyo
 
Baada ya wanajeshi kurudi vitani nyerere aliwashukuru kwa mchango wao wakulitetea taifa ila ilitoa angalizo moja Kali sanaa" YALE YOTE MLIYOFANYA AU KUYAONA NI MARUFUKU KUYAONGELEA KATIKA JAMII AU VYOMBO VYA HABARI" akatoa mabasi kwaajili ya kuwarudisha wanajeshi hao kwao.jamii ya miaka hiyo walikuwa watiifu sanaa kwa mamlaka zao tofauti na sasa kwani kuna mambo mengi sanaa ya kinyama yalifanyika vitani.1972
 
Habari kwenu jukwaani.

Kuna simuluzi BBC Radio wanatujuza historia iliyofichwa. Mwanzoni mwa vita vya Kagera ni kuwa baada ya Amini kufanya uvamizi wake, Tanzania ilitanguliza kikosi cha wanajeshi 2000 mstari wa mbele na chote kilifyekwa na majeshi ya Amin.

Baada ya hapo jeshi letu lilijipanga upya na kusonga mbele hadi Kampala na Jinja ambapo Idd Amin alitimkia Libya na baadae Saudi Arabia.

Hii historia sijiwahi kuisikia, nilijua tulipigana bila upinzani mkali na hatukupoteza askari wengi kiasi hiki kwa mpigo mmoja.

Msimuliaji pia anadai jeshi la Uganda lilikuwa limegawanyika sana kwani baadhi hawakumtaka Amin aendelee kuongoza Uganda na hivyo kulisaidia jeshi letu lililojipanga upya kushinda vita hivyo.

Viva JWTZ.
hamna unachokijua kwa taaluma yangu ndogo ya JKT watu 2000 ni kama vikosi viwili.heuwezi poteza wanajeshi wote hao kwa mara moja.kama sisi tulipoteza 2000 basi adui ni 10000
 
Back
Top Bottom