WanaJF tunaomuunga mkono Lissu sasa ni muda muafaka wa kumsaidia Lissu ashinde!

WanaJF tunaomuunga mkono Lissu sasa ni muda muafaka wa kumsaidia Lissu ashinde!

Ndugu wana JF, kwa miaka kibao tumepiga makelele humu juu ya udhalimu, ufisadi, uonevu, na incompentency ya serikali za CCM hususan hii ya awamu ya tano

Na kama mnavyojua, Sisi wanachama wa JF huenda ni watu ambao tumo katika kundi la watu wenye elimu na tuna upeo mkubwa wa mambo katika nchi.

Sasa ni jukumu letu kuchukua hatua katika kipindi hiki cha lala salama kusaidia kuuangusha mbuyu ambayo mizizi yake imekuwa ikifyonza hatima njema ya wana wa nchi hii na kuwaacha wakiwa hohe hahe

Sasa mwana JF, ni muda muafaka sasa wa kuingia front, kuchukua hatua na kumsaidia Lissu kushinda

1. Ongea na Familia yako, washawishi walio kwenye himaya yako wamchague Lissu

Kaa chini, waelezee hali yako ya kiuchumi, waelezee hali ya mwenendo wa haki katika nchi, kama una wanafunzi waelezee mustakbali wao kielimu hasa makato ya bodi ya mikopo, waeleze kuhusu athari za kutopandisha mishahara itakavyoathiri hata pensheni yako. Waombe watu wa familia yako wampigie kura Lissu aje aboreshe maisha yao

2. Wapigie simu ndugu, jamaa na marafiki huko kijijini kwenu, mijini na popote washawishi wampatie Lissu kura

Wanachama wa JF tupo wengi sana, Iwapo kila mmoja atamtafutia Lissu kura kumi tu basi CCM itakuwa na hali mbaya sana.

Hebu tuweke commitment, kila mtu aliyechoshwa na udhalimu wa serikali hii, awashawishi watu angalau kumi anaowamudu wampigie kura Lissu

Ndugu zangu, hii ishu siyo ya Lissu peke yake, hii ngoma ni yetu sote. CCM wametupuuza kiasi cha kutosha, wametunyanyasa kiasi cha kutosha, sasa tunataka mabadiriko, Sasa ni jukumu letu kusaidia hayo mabadiriko!
Tupu pamoja the game is over ...Lissu is the game changer, we have been waiting for the decades and the battle has been worn through lots of tears and blood. Hongera Tundu Lissu.
 
Lissu atashinda kwa kura nyingi sana huoni ccm wanavyoweweseka??
wameacha kushawishi watu wanajipanga namna ya kuiba kura
 
Wafuasi wa Lisu watapata tabu sana baada ya tarehe 28
Hata wewe utapata tabu pia ipo siku raia wote mtalia humu ndani mi nipo miaka mitano ni mingi sana magufuli hana huruma na maisha ya watu labda kama ni mtoto wa wakuu wa nchi
 
Mimi kila ninapopita napita na John Pombe Magufuli.

Nimeongea na watu6 leo 5 wanaume mmoja mwanamama mwenzangu.

Wale wanaume kulikua na kijana wa kama miaka25 akaniambia dada hakuna mtu mwenye akili timamu atamnyima kura Magufuli

Mwanaume mwingine wa kama miaka 45 akaniambia mdogo wangu wote hao wanaopiga kelele ni wanasiasa wachumia tumbo. Wafanye siasa tuu ila kura ni kwa Magufuli

Baada ya hapo tukaulizana kuhusu vikatio wakasema viko powaaa nikajiondokea

Wanaomuunga jpm mkono wengi wako mtaani na wameshafanya maamuzi
Huu ni uongo labda Kama umeongea na wanaCCM wasiojitambua hakuna MTANZANIA anayeweza kumpigia kura Magufuli
 
Ndugu wana JF, kwa miaka kibao tumepiga makelele humu juu ya udhalimu, ufisadi, uonevu, na incompentency ya serikali za CCM hususan hii ya awamu ya tano

Na kama mnavyojua, Sisi wanachama wa JF huenda ni watu ambao tumo katika kundi la watu wenye elimu na tuna upeo mkubwa wa mambo katika nchi.

Sasa ni jukumu letu kuchukua hatua katika kipindi hiki cha lala salama kusaidia kuuangusha mbuyu ambayo mizizi yake imekuwa ikifyonza hatima njema ya wana wa nchi hii na kuwaacha wakiwa hohe hahe

Sasa mwana JF, ni muda muafaka sasa wa kuingia front, kuchukua hatua na kumsaidia Lissu kushinda

1. Ongea na Familia yako, washawishi walio kwenye himaya yako wamchague Lissu

Kaa chini, waelezee hali yako ya kiuchumi, waelezee hali ya mwenendo wa haki katika nchi, kama una wanafunzi waelezee mustakbali wao kielimu hasa makato ya bodi ya mikopo, waeleze kuhusu athari za kutopandisha mishahara itakavyoathiri hata pensheni yako. Waombe watu wa familia yako wampigie kura Lissu aje aboreshe maisha yao

2. Wapigie simu ndugu, jamaa na marafiki huko kijijini kwenu, mijini na popote washawishi wampatie Lissu kura

Wanachama wa JF tupo wengi sana, Iwapo kila mmoja atamtafutia Lissu kura kumi tu basi CCM itakuwa na hali mbaya sana.

Hebu tuweke commitment, kila mtu aliyechoshwa na udhalimu wa serikali hii, awashawishi watu angalau kumi anaowamudu wampigie kura Lissu

Ndugu zangu, hii ishu siyo ya Lissu peke yake, hii ngoma ni yetu sote. CCM wametupuuza kiasi cha kutosha, wametunyanyasa kiasi cha kutosha, sasa tunataka mabadiriko, Sasa ni jukumu letu kusaidia hayo mabadiriko!
wazo la kijasili safi kijana
 
Huu ni uongo labda Kama umeongea na wanaCCM wasiojitambua hakuna MTANZANIA anayeweza kumpigia kura Magufuli
Unaishi kwenye ulimwengu wa kusadikika wewe. Ingia mtaani uelewe ulipo
 
Sisi Watanzania tuliowengi tutamchagua Rais Magufuli kipenzi cha Watanzani

Yule mropokaji na msaliti wa Nchi Lissu atapigiwa kura na robert tu
Polee sana certified kilaza uliyeshindwa kuonyesha usaliti wa Lissu.
 
Unaishi kwenye ulimwengu wa kusadikika wewe. Ingia mtaani uelewe ulipo
Mimi ni miongoni mwa researchers tuliotumwa kunguka nchi nzima na tukaleta utafti ukazimwa!Trust and take it from uchaguzi ukiwa huru na haki Magufuli hawezi kushinda!
 
Ulijisikiaje alipopigwa risasi msaliti? Au upo programmed kujibu aina ya majibu? Maana majibu yako ni yaleyale.
Wanalumumba wameKalilishwa jinsi ya kujibu, ukiwa-twist kidogo tu ktk hoja, basi tarajia kupewa majibu yale yale.
Sababu Mwalimu wao ni mmoja aliyewashikia akili.
 
Sisi tumeingia magotini tunaomba sasa! Kama kweli ni mpango wa Mungu tuendelee kutawaliwa na kubaguliwa sawa na iwe kama Muumba anavyotaka! Kama ameamua kutukomboa kutoka utumwani hakuna figisu itakayotuweza. SALA= Saidia Lissu Ashinde.
Hakika
 
Nimesha kwambia wewe ni Malaya wa kisiasa huwezi kuolewa .Mimi ni miongoni mwa researchers tuliotumwa kunguka nchi nzima na tukaleta utafti ukazimwa!Trust and take it from uchaguzi ukiwa huru na haki Magufuli hawezi kushinda!

Malaya wa kisiasa ni wewe unayerandaranda hadi ubelgiji. Subiri 28102020
 
Ingieni kazini ila msiingie barabarani, uzuri hua ni keyboard warrior
FA53D11A-E0A4-4994-B4B5-FE1FBEB4C6C3.jpeg

🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Uko sahihi. Mimi siwezi kuwa nakulisha nakulipia ada halafu ukashabikia ccm ambayo inanididimiza.
Mimi Kuna mmoja nime mwambia Ukiendeleza na ujinga wako wa kushabikia CCM ada utajilipia maana hujui ninavyo pata hii pesa kwa maumivu ya kodi kisa CCM !Kwanza ulinyimwa mkopo halafu unabinua midomo CCM !
 
Yan tangu Jana machozi yananitoka, naamini Tundu Lissu anashinda sasa je watamtangaza?
Yan sijui matokeo yakitoka nitakuwa katika hali gani jamani Naomba mniombee
Hayo Ni machozi ya furaha,na furaha Ni ushidi.

Lisu atashinda kwa uwezo wa Mungu Mkuu,Mungu wa miungu,Mungu wa mababu,Mungu Muweza,Muumba wa Mbingu na Dunia na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.

Na wakijaribu kuiba ushindi wake Mungu atawapiga kwa Moto ulao nao watatoweka katika uso wa Dunia kwa aibu.
 
Malaya wa kisiasa ni wewe unayerandaranda hadi ubelgiji. Subiri 28102020
Ona mnavyohangaika wawili tu Mama D na Bia yetu wengine wako wapi?
Tundu Lissu ndiye Rais ,Huyo JIWE anaye mwaga damu za watu hatumtaki period
 
Back
Top Bottom