WanaJF tupeane mawazo kwa mtu anayetaka kufanya biashara Kariakoo kwa mtaji wa milioni 50

WanaJF tupeane mawazo kwa mtu anayetaka kufanya biashara Kariakoo kwa mtaji wa milioni 50

Mr mutuu

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2023
Posts
2,869
Reaction score
14,501
Kwema wakuu,

Kuna mtu kanifata anahitaji ushauri, anataka kujilipua kwenda kariakoo kufanya biashara.... Kwanini Kariakoo? Anaamini Kariakoo ndo hub ya biashara hapa Tanzania.... Mzunguko wa kariakoo si rahisi kuupata mahali pengine popote hata kama unapata faida ndogo

Amekua akifanya biashara ya microfinance muda wote anasema changamoto zimekua nyingi anataka kufanya biashara nyingine, hivyo kiufupi Hana uzoefu na biashara, nimekaa nae anasema ana milioni 50(pesa ya pango na mtaji hapohapo)... Kuhusu mahali pa kukaa yeye na mahitaji yake anasema ana bajeti nyingine tofauti kabisa

Sasa wakuu, JF ni ziwa la maarifa, nimekuja kupokea mawazo yenu, je anaweza kufanya biashara ya aina Gani, he is open minded anapokea ushauri ili ajipime, japo nimemwambia atenge kwanza kama Milioni 30 za biashara 20 aweke kama emergency mambo yakiwa mazuri atazi integrate taratibu bila haraka

Mi biashara nayofanya ni tofauti kabisa na yeye anachotaka so nimeshindwa kumshauri hasa afanye Nini, kwa faida ya Wana jf wote naomba mje na majibu serious maana huu Uzi unaweza kua msaada kwa wengine( samahani wenye mzaha au wanaovamia Uzi za watu kuanza kutongozana Leo mtustahi kwanza)

Karibuni wakuu naamini huu Uzi utakua wa manufaa hata kwa watu wengine hata kama ni miaka ya mbeleni maana jf ni hazina hakipotei kitu
 
kwanza kabisa akae akijua kariakoo unaweza kuwa na wazo la kuuza nguo ila ukapata fremu itakayo kufanya uuze vifaa vya simu, simu au hata nguo za ndani

pia asikurupuke kwanza atakula za pua anatakiwa ajue wafanya biashara kariakoo wanafanyaje biashara kariakoo biashara yoyote ile inalipa kikubwa akili tu

hapo kwenye fremu kuna kodi kuna kilemba unaweza shangaa anapata fremu kodi ya mwaka na kilemba ni 20M
 
Kwenye frame Kuna mtu namjua hapo kariakoo naweza kumsaidia asipigwe sana tatizo mpaka sasa afanye maamuzi na Nini hasa anataka kufanya maana kariakoo biashara zimekaa kimtaa, unaweza kupata frem sehemu ambayo ni kinyume kabisa na biashara yako
 
atafute fremu kwanza akishapata ndo atajua afanye nini

kariakoo kila kitu ni hela niyeye tu na target na akili zake

akienda bila gadi........
 
Kwenye biashara naamini knowledge inasimamia asilimia 70 ya mafanikio na mtaji unasimamia asilimia 30

Kuna mawinga pale kariakoo Wana ujanja wa Kila aina ya biashara ila hawana mtaji, naamini Kuna watu Wana maarifa wakipata hata 10M tu wanasogea mbali sana ila hawana mtaji

Unakuta kuna mwenye hata milioni 100 Hana maarifa, mwenye mtaji akisema atafute mwenye maarifa washirikiane kibongobongo uaminifu nalo tatizo, shida tupu
 
Namba watamgawa bila ya idadi😃

Naona angepata kwanza maamuzi anataka kufanya Nini ili atafute frem kwenye mtaa unaoendana na aina ya Hio biashara
Anaweza tafuta huo mtaa na kwa wakati huo akakosa then akakata tamaa,

Atafute frem taratibu akipata ataangalia wenzake wanauza nini hapo sana nae ataweka then atajifunza mengine taratibu au aanze kuweka booking frem zinazojengwa kwenye maghorofa yaliyobomolewa haswa huku mt. congo au soko lakaribia kuisha akipata huko fremu ataweka atakacho
 
anaweza tafuta huo mtaa na kwa wakati huo akakosa then akakata tamaa,

atafute frem taratibu akipata ataangalia wenzake wanauza nini hapo sana nae ataweka then atajifunza mengine taratibu
au aanze kuweka booking frem zinazojengwa kwenye maghorofa yaliyobomolewa haswa huku mt. congo au soko lakaribia kuisha akipata huko fremu ataweka atakacho
Wazo zuri
 
na kuna wafanya biashara kariakoo hawana instagram hawana facebook wako ndani ndani na wanauza balaa

akili mtu wangu
Sema Nini nina watu wawili watatu pale kariakoo, Kuna jamaa yangu ana apartment hapo hapo sema yeye hafanyi biashara ngoja nione kama naweza muunganisha nae ampe accomodation maana jamaa ana chumba Cha wageni then dogo achangie bills kidogo

Then nimuombe amuunganisha na mawinga pale hata wawili, dogo aende akatembee hata mwezi mwenyewe aingie Kila Chocho, sio akae kizembe tu asubiri kuletewa idea, naamini ndani ya mwezi atakua amepata idea nzuri, raha ya ngoma kuingia kuicheza
 
yes akiweza awe winga kwanza na asiwaambie hao mawinga watakaomkaribisha sokoni kwamba anataka kuingia nkufanya biashara au kama anaweza azunguke mwenyewe kila siku ndani ya mwezi atakua amejifunza vingi

maana mawinga pia wana tabia ya kukuwingia wakikiona mshamba hata uwaambie na wewe ni winga
 
na kuna wafanya biashara kariakoo hawana instagram hawana facebook wako ndani ndani na wanauza balaa

akili mtu wangu
Hawa wa ndani huwa wanauza bei ya Jumla na bei rahisi na wengi wanafunga mizigo China wenyewe, kwahyo Hawa wa nje hununua ndani Kwa Jumla kuuza ni lazima

Angewza kufunga mzigo China mwenyewe na akapata fremu angeuza Sana asitegemee mizigo ya wafanyabiashara wenzake lazima wamlangue.
 
mtoa mada anahitaji wazo la biashara gani afanye ... watu wanatoa ushauri ulio nje ya wazo its as if asha pata wazo la biashara

tujitahidi kua specific

with fact mhusika tayari ana exeperience unaanza mshauri biashara akili ... so do u think yeye hana akili na ka shasema katoka microfinance. what he/she need it IDEA

imagine una mshauri mtu akachukue frem wazo litakuja uko uko serious ... what kind of nonsense this is...

biashara ni prospect sio kitu ya kuingia tu inaitaji assessment kubwa mno na in depth unless otherwise atafungua na kesho akafunga

Binafsi sina idea so ntakua kama washaur walio pita ... "nothing beats old dog in his own yard"
 
sure sasa mtu hata hajui anataka kufanya biashara gani ndo tatizo sasa

labda ajue kwanza anataka kufanya nini then ndo anaweza enda huko china au kokote kufanya mzigo depends on anachotaka kuuza
 
mtoa mada anahitaji wazo la biashara gani afanye ... watu wanatoa ushauri ulio nje ya wazo its as if asha pata wazo la biashara

tujitahidi kua specific

with fact mhusika tayari ana exeperience unaanza mshauri biashara akili ... so do u think yeye hana akili na ka shasema katoka microfinance. what he/she need it IDEA

imagine una mshauri mtu akachukue frem wazo litakuja uko uko serious ... what kind of nonsense this is...

biashara ni prospect sio kitu ya kuingia tu inaitaji assessment kubwa mno na in depth unless otherwise atafungua na kesho akafunga

Binafsi sina idea so ntakua kama washaur walio pita ... "nothing beats old dog in his own yard"
unaujua mchakato wa biashara kariakoo? kauulize ni wafanya biashara wangapi walienda na wazo A la biashara wakaishia kwenye wazo B asilimia 70 ya wafanya biashara wanafanya biashara kutokana na mitaa walipo
 
Back
Top Bottom