WanaJF tupeane mawazo kwa mtu anayetaka kufanya biashara Kariakoo kwa mtaji wa milioni 50

WanaJF tupeane mawazo kwa mtu anayetaka kufanya biashara Kariakoo kwa mtaji wa milioni 50

Auze bidhaa za kike mfano mawigi
China mawigi ya 25-40 huku yanauzwa kuanzia 70- 120.
Handbag china 5000-10000 huku ndio zinauzwa 18000- 25000 yeye alenge wateja wa jumla tu.
Kuna vitenge na Haya malace material Kazi kwake
 
yes akiweza awe winga kwanza na asiwaambie hao mawinga watakaomkaribisha sokoni kwamba anataka kuingia nkufanya biashara au kama anaweza azunguke mwenyewe kila siku ndani ya mwezi atakua amejifunza vingi

maana mawinga pia wana tabia ya kukuwingia wakikiona mshamba hata uwaambie na wewe ni winga
Sawa mkuu shukrani ngoja ntampa hii idea
 
Auze bidhaa za kike mfano mawigi
China mawigi ya 25-40 huku yanauzwa kuanzia 70- 120.
Handbag china 5000-10000 huku ndio zinauzwa 18000- 25000 yeye alenge wateja wa jumla tu.
Kuna vitenge na Haya malace material Kazi kwake
Kuna mtu aliniambia ukiwekeza kwenye urembo wa kina dada mzunguko ni mkubwa maana wanawaza kupendeza muda wote
 
mtoa mada anahitaji wazo la biashara gani afanye ... watu wanatoa ushauri ulio nje ya wazo its as if asha pata wazo la biashara

tujitahidi kua specific

with fact mhusika tayari ana exeperience unaanza mshauri biashara akili ... so do u think yeye hana akili na ka shasema katoka microfinance. what he/she need it IDEA

imagine una mshauri mtu akachukue frem wazo litakuja uko uko serious ... what kind of nonsense this is...

biashara ni prospect sio kitu ya kuingia tu inaitaji assessment kubwa mno na in depth unless otherwise atafungua na kesho akafunga

Binafsi sina idea so ntakua kama washaur walio pita ... "nothing beats old dog in his own yard"
Ndo maana nikasema aende afanye survey mwenyewe

Hili la kulipia frem hujajua hata unataka kufanya biashara Gani is a big risk
 
Siku hz nimekua mvivu kuandika ila tajitahidi.

Mtu ukiwa unaenda kariakoo mara Moja kufata mahitaji flan na kuondoka anahis kama kariakoo ili ufanye biashara inakutaka uwe na pesa nyingi kitu ambacho so kweli

Kuna watu kariakoo kama mawinga wana update zote za mchina au mchaga atashusha container lini atakachofanya yeye anawahi sample ambazo anaona zinatembea sana anaongea na wahusika anazuia kama katoni 70 au 100 then annapandisha Bei hata jero tu Kwa Kila sample ....hiii inataka uwe na connection nzuri ujue sample kabla haijafika store

Kuna anaingia kkoo anatafuta fremu yake anakua anauza Mali za watu, anachofanya yeye anakua anadesign order book ambayo inaweza kutoa mzigo store anakua analipwa Kwa commission eq kila pisi Moja 200

Kuna mwngn anatafuta tajiri huko china...then anakua anatumiwa mzigo yy anauza analipa taratibu hii wanaaply sana wahaya utakuta frame yake ina TV kapadesign anaweka picha nyingi alizopiga na viongozi wa kitaifa na wanajeshi wakubwa Glenn

Wachache wanaingia kwa akili zao wanapambana mpaka wanatoboa

Kikubwa we fanya research jitose kua makini tafuta watu wakupe mbinu la sivyo utakuta frame yako itajaa leseni na vyeti kibao
 
biashara inataka uthubutu 😂na uvumilivu wa mikikimiki
 
Mpaji Mungu Gily Gru reyzzap nimewatag kuna mada za kariakoo niliona mna uzoefu huko wa muda kidogo, wekeni neno msaidie kijiji
Uzoefu wangu ni biashara ya nguo tu za kiume. Za kike niliacha 12 years ago biashara yake ni ya kubeti

Kipindi hiki kwa miezi 6 biashara zimelala kkoo. Unakuta unauza nguo mbili per day mzee. Simshauri kabisa ni tofauti na mwanzo walikuwa wanakuja wakongo na wengine wengi kutoka nje ya nchi

Juzi nimetoka kulipa 14 million kodi ya fremu. Pasua kichwa nawaza kutoka kkoo kwa sasa

Wanaopata hela kkoo
1. Kuna watu wanaleta mizigo nje wanauzia kwemye ma warehouse ai niseme store. Hana machine ya EFD wala halipi kodi kubwa. Most of the rent storage are cheaper, unakuta ghorofani huko fremu hazifai

2. Machinga, wenye meza nje. Kuna watu wana mitaji mikubwa sana ana meza tano nje. Yani ana vijana na meza nje anapiga pesa kwa sababu analipia ushuru tu halipii fremu. Anauza nguo zile zile ambazo tunauza dukani.

Ushauri wangu. Aanze na biashara ndogo, kisha ikiwa ameimudu aongezee mtaji aifanye kubwa. Sina ushauri zaidi ya huo. Hajawahi kufanya biashara achunge sana asivamie biashara akapoteza hela yake

Pili aachane na biashara ya kilimo. Kilimo ni kwa ajili ya matajiri sio masikin, hakijawahi kumuinua masikini bongo. Nilikuwa natoa hela dukani naingiza shambani Acha tu.

Kila jambo ni shule

Usiku mwema
 
Kwema wakuu,

Kuna mtu kanifata anahitaji ushauri, anataka kujilipua kwenda kariakoo kufanya biashara.... Kwanini Kariakoo? Anaamini Kariakoo ndo hub ya biashara hapa Tanzania.... Mzunguko wa kariakoo si rahisi kuupata mahali pengine popote hata kama unapata faida ndogo

Amekua akifanya biashara ya microfinance muda wote anasema changamoto zimekua nyingi anataka kufanya biashara nyingine, hivyo kiufupi Hana uzoefu na biashara, nimekaa nae anasema ana milioni 50(pesa ya pango na mtaji hapohapo)... Kuhusu mahali pa kukaa yeye na mahitaji yake anasema ana bajeti nyingine tofauti kabisa

Sasa wakuu, JF ni ziwa la maarifa, nimekuja kupokea mawazo yenu, je anaweza kufanya biashara ya aina Gani, he is open minded anapokea ushauri ili ajipime, japo nimemwambia atenge kwanza kama Milioni 30 za biashara 20 aweke kama emergency mambo yakiwa mazuri atazi integrate taratibu bila haraka

Mi biashara nayofanya ni tofauti kabisa na yeye anachotaka so nimeshindwa kumshauri hasa afanye Nini, kwa faida ya Wana jf wote naomba mje na majibu serious maana huu Uzi unaweza kua msaada kwa wengine( samahani wenye mzaha au wanaovamia Uzi za watu kuanza kutongozana Leo mtustahi kwanza)

Karibuni wakuu naamini huu Uzi utakua wa manufaa hata kwa watu wengine hata kama ni miaka ya mbeleni maana jf ni hazina hakipotei kitu
Kwa uzoefu wangu mdogo pale kariakoo watu hawafanyi biashara pale watu wanatega pesa..
Akisema akafanye biashara ataangukia pua.
 
Back
Top Bottom