Wananchi Mara waandamana kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Magufuli



Dhambi ya "Ukagame" ni ipi? Tueleze ubora wa "U-Mwinyi", "U-Mkapa" au "U-Kikwete"? Mbona Mungu ni mmoja tu na mbona hujawahi kulalamika? Mbona hatubadilishi wanawake au wanaume zetu wa ndoa wenye tabia nzuri kila baada ya miaka 5 au 10? Kwani tumeumbwa ili tuutumikie muda au muda upo ili kutusaidia sisi kupanga na kuratibu tu mambo yetu?

Sisi ni binadamu tulioumbwa na kupewa uwezo wa akili unaotumia mantiki.Hatuwezi kushindwa kutumia kitu chema kwa sababu tu ya muda.Mwaka 2015, sisi wengine tulimtaka Ngoyai kwa sababu ya kutamani mabadiliko tu.Ikiwa mabadiliko yamefika inakuwaje tuachane nayo tuanze kuumizwa vichwa kutafuta "Kichwa" kingine tusichofahamu kiko wapi,kikoje na kitakuwa na sifa gani kiingia "ndani"?Sioni kosa la hao wananchi.Kwani wewe unafikiria kuwa walipandwa na "mapepo " tu kufikia kutamani hali hiyo?
 
Mwaka 2020 badala ya kuonyeshwa maendeleo tutaonyeshwa ndoo za usaha na makaburi yaliyowazi na mifupaaaa
 
Inawezekana kwa sababu kila iitwapo leo anapongezwa na vikund vya watu wachache. Huwez sikia akikubali akosolewe. Pia angalia list ya role model wake ndio utajua hyo kitu inawezekana kwa huyu mzee wetu
 
Yeye atawakatalia na ningekuwa mimi ningekataa kama mbunge fulani.
Na atafanya hivyo
 
Huo ni udikteta.. Ajabu ni kwamba wakiandamana waupande wake fresh tu, wakiandama wale wengine mpaka magari ya "faya" yanawashwa.
 
unasahau kuwa ni wabunge wa CCM ndio waliopitisha kuwa ni miaka kumi na ni makamanda wa chadema walio muondolea ukomo wa madaraka mwenyekiti wao
Anamuiga mjeda Kagame na kale kawilaya kake ni sawa na Chato yote.
Kwa Tanganyika yetu haitakaa itokee
 
Ngoja arudi mitano tena uone km hao wananchi watantaka tena, haya maigizo ya awali tu. 2021 wataandamana kumkataa
Nadhan wananchi unao waongelea sio watanzania , hakuna taifa lenye wananchi wajinga na wapumbavu na wenye kiherehere na kujipendekeza pamoja na unafiki kama tanzania , hii ni nchi yenye giza nene kuanzia wananchi hadi serikali yao.
 
Umemaanisha nini kusema awe Rais wa maisha?

Kwa upande wangu natamani sana abadilishe katiba imruhusu kutawala hata miaka 30 siyo mbaya.
 
Nisaidie namba zao niwapigie maake naona wanaelekea kuzimu akili imeshawaruka duuuh
 
Acha ramli chonganishi!!!Mbowe kabadili katiba kinyemela kuwa Mwenyekiti wa maisha hujafungua thread
Katika ya chama na katiba ya nchi ni vitu viwili tofauti kabisa tatizo shule huna ujinga umekujaa kichwan hivyo hata hujui kuwa hivyo ni vitu viwili tofauti.
 
Reactions: SDG
Tatizo la Kipara mshauri wake ni bashite ninavyoijua CCM hawawezi kukubali hasa hao Marais wastaafu
 
Hahahaaa kama wewe si mtanzania hilo ndio waweza ona gumu lakin kama ni mtanzania basi amini kuwa hakuna kitu ambacho rais atataka kifanyike nchi hii kikashindikana.
 
Tatizo la Kipara mshauri wake ni bashite ninavyoijua CCM hawawezi kukubali hasa hao Marais wastaafu
Kwa tanzania hilo linawezekana hata leoleo mkuu ,hii nchi ina laana ya kudumu ndio maana hakuna tunalo weza zaid ya ujinga
 
Utakuwa ni ujinga kukataa kuongeza muda kwa mtu anayefanya vitu kwa faida ya nchi eti kwa sababu tu kuna katiba na kuna watu wanapinga,ni ujinga,wakitetea kuwaweka watu walioshindwa kuisaidia nchi hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…