Wananchi mkoani Arusha waandamana kupinga Ushoga

Wananchi mkoani Arusha waandamana kupinga Ushoga

Hapo Arusha si wengi tu kupata hata milo miwili ya sembe na mchicha kwa siku ni tabu kubwa kwao, wengine si hawana maji au umeme, kwa nini wasiandamane kuhusu hayo badala yake waandamania jinsi watu wazima walivyamua kwa hiyari yao binafsi walivyoamua namna yao ya kufanya ngono??
Hawa utawalaumu bure tu, ufahamu wao ulishaharibiwa.

THE LAND OF THE BLIND, majizi yanatumbua fedha na mali za nchi halafu huku chini wanawarushia matakataka ya kujadili kama ushoga na singeli za zuchu.

Sasa hawa ni vikaragosi tu, hawaelewi chochote. Ukijumlisha na MIHEMKOO ni shida.
 
Rehema iliyopo kwa punga ni kujisalimisha kwa toba ya kuachana na huo usodoma na sii hata siku moja kutafuta namna ya kuufanya huo ufirauni kurasimishwa.
Kuna mijitu katika hili yanaangalia maendeleo ya kifedha na vitu badala ya maendeleo ya watu kiutu, kiafya na kijamii.
Mimi huku nilipo japo sipo Arusha naungana nao kuandamana kupinga kurasimisha kisheria ushoga.
 
Maandamano hayo yaliongozwa na viongozi wa dini, na wananchi walijitokeza kwa wingi kupinga matendo ya mapenzi ya jinsia moja.

Hali hii imetokana na baada ya vikundi vya kutetea mapenzi ya jinsia moja duniani kuzidisha kasi na msukumo wa kuhalalisha matendo hayo.

Tuliona presha nchi ya Qatar iliyopigwa wakati wa kombe la dunia.

Tukashuhudia vitabu vinavyofundisha mambo hayo vikisambazwa ktk shule za watoto.

Tumeshihudia shule fulani ambayo watoto wanafundishwa kufanyana kinyume cha maumbile.

Huko Kenya mahakama ya juu ikaruhusu uanzishwaji wa NGOs za kutetea ushoga ktk nchi hiyo.

Na kuna baadhi ya madhehebu ya dini duniani yameanza kurasimisha ndoa za jinsia moja na kuna Mengine yamebaki na msimamo uleule wa toka zamani wa kukataa mambo hayo machafu.

Kwa mfano hapa Tanzania Kanisa la Anglican la Tanzania limekataa katakata kukubaliana na kanisa la Anglican la Uingereza kuruhusu ndoa za mashoga. Katika barua ambayo uongozi wa kanisa la Anglican la Tanzania limeliandikia kanisa mama la Anglican la uingereza, Limegoma kabisa kukubaliana na msimamo wa kanisa hilo la Uingereza kuhusu kuruhusu ubarikio wa ndoa hizo.

Kwa bahati mbaya pia, kanisa la Kikatoliki huko Ujerumani limepiga kura kuruhusu ubarikio wa ndoa za Jinsia moja kuanzia mwaka 2026. Hii inafuatia kauli ya Papa ya kuwatakia "Rehema( Grace)" watu wote hata wale wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Hapa chini ni video ya wananchi huko Arusha kuandamana kupinga mambo ya ushoga.

View attachment 2547164

View attachment 2547165
 

Attachments

  • IMG_8673.MP4
    10.9 MB
  • IMG_8646.MP4
    12.3 MB
Inasikitisha sana.
Hawa utawalaumu bure tu, ufahamu wao ulishaharibiwa.

THE LAND OF THE BLIND, majizi yanatumbua fedha na mali za nchi halafu huku chini wanawarushia matakataka ya kujadili kama ushoga na singeli za zuchu.

Sasa hawa ni vikaragosi tu, hawaelewi chochote. Ukijumlisha na MIHEMKOO ni shida.
 
Wanajua km mie ni papai liliovaa, tena hadi mlaji wa papai hilo wanamfahamu vyedi. Na hakuna reaction yoyote walio ioneshaaa.
Poleeeeeeeeh.
Kwa hyo mkuu we ni papai[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]dah dunia hii sa si bora ungekuwa hata fenesi,unakuaje papai aasee???
 
Nna neno bas, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mashoga na wasagaji bado wapoo sanaa, na hakuna kitu mtawafanyaa.
Mweh[emoji1787][emoji1787][emoji1787]kazi ipo
 
Mkuu inawezekana una ufahamu mdogo sana juu ya haya masuala. Nikuhakikishie kabisa Mkuu kuna watu wanazaliwa ni mashoga na hii inatokana na mvugano wa homoni. Unatakiwa kufahamu ushoga ni suala la hisia sio vitendo.

Kuna watu wao wanahisia za kuwa ni jinsia tofauti na jinsia walizo nazo ndio maana kuna ma tom boy pia. Sasa kama mwanamke anaweza kuwa na hisia za kiume na kuwa tom boy tangu kazaliwa vipi kuhusu mwanaume kuwa na hisia za kike tangu kazaliwa?

Jambo lingine ambalo huwenda haulifahamu vizuri ni kuwa sio kila anayefira mwanaume mwenzake basi ni shoga hapana, kuna watu sio mashoga ila wanafira wanaume wenzao, kwanini sio mashoga.ni kwasababu hawana hisia za kimapenzi kwa hao wanaowafira.

Sasa utauliza kama hawana.hisia kwanini wanafanya hivyo?, zipo sababu nyingi sana mfano ukatili, hisia za kutaka kumtawala mtu, ulevi, imani potofu, tamaa n.k

Hivi unafahamu kuwa kuna watu ni mashoga ila hawaingiliwi kimwili na wanaume?.

Tukiweza kutofautisha hizo hali tutaweza kutatua tatizo, tofauti na hapo ni kudanganyana tu.
Umeandika vizuri mnooo, ila kuna kitu hakiko sawaa.
Nikiwa vizuri ntakuja kuelezea
 
Kwa hyo mkuu we ni papai[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]dah dunia hii sa si bora ungekuwa hata fenesi,unakuaje papai aasee???
Mie ni papai liloiva pyuuuuuuuh, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ni kweli Mkuu ila kwa masikitiko kabisa hakuwezi kukatungwa sheria ya kupinga ushoga nitakuambia kwanini haiwezekani na haitatungwa kabusa hiyo sheria.

Sababu ni moja rahisi kabisa, ushoga ni swala la kihisia haliwezi kutungiwa sheria sababu halithibitishiki.

Swala linaloweza kutungiwa sheria ni mapenzi ya jinsia moja, na inabidi ifahamike kuwa mapenzi ya jinsia moja ni ama mapenzi baina ya mashoga au wasagaji.

Sasa kama ushoga hauwezi kutungiwa sheria ni wazi kuwa mtu akijitangaza kuwa ni shoga hatakutwa na hatia, ila mtu huyo huyo akikutwa anafanya mapenzi na mtu wa jinsia yake awe ni shoga au msagaji ataweza kukutwa na hatia.

Sasa changamoto ni kuwa hayo matendo ya ngono hufanywa kwenye faragha, na hivi majuzi tu Tanzania imepitisga sheria ya faragha na watanzania wengi wakaifurahia bila kuipima vizuri.

Sasa umeipata picha vizuri?, hautawasikia viongozi wa kiserikali katika nafasi zao za kiuongozi wakiwa serious na hili swala kila atakayeongea ataongelea hili kulingana na hadhira atakayokuwa nayo na sio kama kauli ya kimamlaka, fuatilia.

Sasa Mkuu chakufanya ni nini?, chakufanya ni kurudi kwenye msingi wa jamii ambao ni familia na hizi taasisi za kiimani ziongelee haya mambo kwa watu wao na sio kuanza maandamani ambayo hayatakuwa na tija kama walichokifanya huko Arusha.

Lazima tufahamu tunapambana na kitu gani.

Nikupe ufahamu wa muelekeo wa sheria yetu juu ya mambo ya mapenzi ya jinsia moja.

Hadi sasa ushoga na usagaji sio kosa Tanzania(inashangaza) na hili sio bahati mbaya ni kwa makusudi kabisa.

Kilicho kosa ni kufanya mapenzi kinyume na maumbile/tofauti na ilivyo asili. Tena ukiisoma kwa undani hii sheria utagundua usagaji kuna namna sio kosa.

Sasa tujiulize ngono ni nini?, je ngono ni kuingiliana kimwili kwa kutumia via vya uzazi pekee?, je kunyonyana sio ngono?, kutomasana hadi kufikia mshindo sio aina ya ngono?

Hyo yote hapo juu sio makosa kwa sheria yetu, ina maana kama watatoka wanaume wawili wakabusiana na kutomasana hadharani hawatakuwa wamefanya kosa la jinai katika misingi ya ushoga. Waendesha mashtaka wakijitahidi sana watawashitaki chini ya makosa ya kuharibu maadili na hapo bado watashinda kesi.

Kitu gani nataka kusema hapa, ni kuwa tunahitaji elimu kubwa sana juu ya haya mambo, tuyasome turudi kuiangalia jamii yetu, tuangalie muelekeo wa dunia juu ya masuala ya kingono kisha tujue sasa tunatakiwa kufanya nini.

Natumaini utakuwa umepata ABC zingine juu ya hii vita Mkuu.
Sheria ipo tayari kasome kifungu cha 154 cha Penal Code kama nakumbuka vizuri.
 
Back
Top Bottom