Wanandoa wapya wafariki kwa ajali Iringa

Wanandoa wapya wafariki kwa ajali Iringa

“ndipo akakutana na basi la Luwinzo uso kwa uso.”

Duh na hii mashine inavyokuwaga moto mkali, lazoma ajali ilikuwa na impact kubwa sana...
 
Hizi ajali zinazidi kumaliza watu. Ajali hiyo imetokea Iringa ambapo watu 3 wakiwemo wanandoa ambao wamefunga ndoa siku 4 zilizopita.

======

Noah na Agnes wamefikwa na mauti katika ajali hiyo ikiwa ni siku nne zimepita tangu walipofunga ndoa, Desemba 17, 2022 jijini Arusha.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi akizungumza na Mwananchi Digital amesema, waliofariki katika ajali hiyo ni watatu wakiwemo askari wawili wa Polisi, Mkoa wa Arusha, Noah Semfukwe (30) aliyekuwa dereva na mkewe, Agnes Kiyeyeu (27).

ajaali-pic2.jpg


Gari lililopata ajali na kusababisha vifo vya watu watatu wakiwemo wanandoa Noah Semfukwe (30) na Agnes Kiyeyeu (27). Mwingine aliyekuwa kwenye gari dogo ni, Enocka Mbata (35), mkazi wa Iringa aliyekuwa kwenye gari hilo ambaye mwili wake umezikwa leo mkoani humo.

Kamanda huyo amesema, ajali hiyo ilitokea saa 3:05 asubuhi wakati gari hilo dogo aina ya Vits kulipiga katika tuta kubwa, ikaenda kwa kasi mbele na kukawa na lori mbeye yake, ikamlazimu kulipita, “ndipo akakutana na basi la Luwinzo uso kwa uso.”

Amesema miili ya askari hao imehifadhiwa Hospitali ya Mkoa wa Iringa na kesho Alhamisi, itasafirishwa kwenda Makongorosi, Mkoa wa Mbeya kwa maziko.
...Ajali Haileweki Vizuri. Eleza Vizuri. Isiwe kama Unawahi 'Like' ![emoji846]....
 
Wazungu wanavofundisha adabu madereva barabarani, HAWANA HAJA YA TUTA

Sehemu ya 80km/h ukaenda +100km/h
1. Wanakunyang'anya leseni wiki 2
2. Wanakupiga faini $450
3. Insurance company zinakucharge pesa ndefu ya bima inaweza toka 300$ to 700$ per year

Wanaheshimu barabara kuliko chochote
...Kweli. Na ndio maana husikii Ajali za Kijinga jinga za mara Kwa Mara kama Zetu !!..[emoji45][emoji45][emoji45]
 
Chanzo cha ajali:
Watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama, wakiendesha vyombo vya moto barabarani huwa hawaheshimu sheria za usalama barabarani.

Hii iwe fundisho kwa watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

R.I.P
Sema baadhi yao sio wote
 
Mkuu dunia ina mengi.. baki kwenye sintofahamu hivyo hivyo.. maombi ndio jambo pekee litakalokuepusha na mabaya..
Hatupo duniani tuishi milele, tulishaambiwa tutakufa hakika, maombi hayatakuepusha na kifo.
 
Back
Top Bottom