KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 19,185
- 37,239
Habari za jumapili waungwana wa jukwaa hili,
Katika hali ya kawaida kama ilivyozoeleka na wengi katika ulimwengu wa maraha na mahaba ukimuuliza mwanandoa sababu ipi iliyomfanya aolewe/ amuoe mwenza wake na kudumu nae miaka yote.....jibu linatakiwa kuwa jepesi kuwa
KWA KUWA NI CHAGUO LANGU NA NI YEYE PEKEE NIMEPENDAYE.
Linapokuja jawabu nje ya upendo na chaguo basi ni wazi NDOA hapo hakuna kwa kuwa ile sababu hasa iliyo wafanya kuwa pamoja imeshaondoka nafsini mwenu.
Ili maisha yaendelee mtu anaangalia cha ziada nje ya upendo uliokufa kama vile manufaa anayopata kwenye muunganiko huo kwa muda huo au kutoweza kumudu gharama za maisha baada ya kuwa na mzigo mzito wa majukumu.
Hadi kufikia hapo tena hakuna anayefurahia ndoa isipokuwa inakuwa gereza ambalo akimaliza Tu kutumikia kifungo na adhabu anaangalia ustaarabu mwingine.
Kama ni watoto wakikua na kujitegemea unashangaa mwenza anatumia muda mwingi kwa watoto kama ni biashara ikashaleta mafanikio na kujihakikishia kuwa anaweza kuishi peke yake ndio harakati za kudai uhuru zinaanza.
Haya mambo ninayoaandika ndio yanayoendelea kwenye ndoa nyingi mengine yapo wazi kama ukiwa karibu na wanandoa. Mengine yanafumuka baadae baada ya upande mmoja kupata uhuru wake.
Lakini kimsingi hasa ndoa inafungwa moyoni kutokana na ridhaa yako.
Uchunguzi usio kuwa rasmi na data mbali mbali kwenye jamii ambapo humo humo tunaishi na wanandoa kama majirani, wafanyakazi wenzetu, wenye nyumba na wengine wapangaji wetu zinatanabaisha uhalisia wa haya mambo.
Ndio maana wanandoa wengi ambao NDOA zao zimekufa mioyoni mwao wanaishi kwa plan B ya miaka mingi ijayo.
BE WISE.
CHOOSE WIFE, STAY SAFE.......