Hii umeandika tu hujakutana na wazee hizo mambo mwenyewe utarudisha mpira kwa kipa. Kuna mabaharia wakiamua hata mwaka wanautenga ili wakupige mambo. Nataka nikwambie jambo moja mtu yeyote akishaingia kwenye ndoa concentration ya mambo ya mapenzi inapungua, iwe mwanamke au mwanaume na wengi tunajikita kwenye issue ya maisha, kama kutafuta hela, kujenga na kusomesha watoto.
Hapa ndo mabaharia huingia na niwaombe samahani kwa kutoa siri za kambi. Hapa baharia atatenga muda ili tu akuvue nguo atahakikisha kwa siku anakujulia hali hata mara nne, yaani asubuhi, mchana, alasiri na jioni.
Huambatana na vijizawadi vidogo vidogo tu ambavyo havilingani thamani na vile alivokupatia mmeo. ( Wanawake wa kileo mtaanza kumwita baharia ROMANTIC) hahaha yaani ngoja nicheke. Ghafla utajikuta mwenyewe unampangia ratiba ya muda gani mzuri wa kuwasiliana na wewe.
Mzee baba akirudi nyumbani ana stress, watoto wanataka ada, chuo boom halijatoka, mara mzigo umekwama bandarini, gari imegonga nk. Akijitahidi anagonga kimoja na hana story analala usingizi. Baharia akija kwa sababu akili yake ameiandaa kwa ajili ya hayo mambo nawe umejiandaa kwa ajili hizo mambo, mechi inakuwa finali kila mmoja anaonyesha uwezo wa kumili dimba.