Mwaka mmoja nilienda hospitali kumjulia mke wa jamaa yangu akiwa kalazwa pale siku ya 2. Kulazwa kwake ilitokana na tukio la aibu lililofanywa na mkewe katika hali ya kushangaza sana.
Kabla ya kumuona mkewe jamaa alinipokea kituoni tukapata sehemu ya kujadili maendeleo ya mgonjwa tukiwa tunasubiri muda wa kuwaona wagonjwa.
Jamaa akanisimulia mkewe alipata shida akiwa kwenye harakati za kutoa mimba aliyopewa na mchepuko wake wa mjini. Hayo amekiri mwanamke baada ya madaktari kuweka wazi kuwa alikuwa anatoa mimba. Tukirudi nyuma kidogo huyu mwanamke aliingia kwenye mgogoro na mumewe kwa madai kuchoka kuzalishwa kila mara. Wakakubaliana watumie kondomu kama uzazi wa mpango.
Lakini mwanamke akawa na mchepuko mji wa pili ambapo ni dhahiri hawakuwa wanatumia kondom. Wakati huku nyumbani jamaa analazimika kula kwa kondom mchepuko ulikuwa unakula kavu mpaka ukatia mimba ya kwanza. Kuogopa mgogoro yule shemeji akatoa mimba, akafanikiwa.
Ajabu ni kwamba hakuacha kuchekupa kwa yule jamaa. Tena aliendelea kuliwa kavu baada ya muda tena mimba ikajaa. Akaona isiwe shida akapanga tena kutoa. Akiwa kwenye harakati za kutoa ndo mimba ikagoma na afya ikawa tete. Kukimbilia hospitali ndio yote hayo yakabainika.
Wakuu huyu ndio mwanamke. Wanaojiona wanamjua sana mwanamke wanajidanganya. Mwanamke amekuwa sehemu kubwa ya migigoro ngazi ya familia. Mwanamke ndio mchochezi wa kuni anaweza kuwasha moto anaweza kuuzima na kila kitu.
Ishi kwa akili sana na mwanamke,kuna watu wanawaamini wake zao kwa 100%. Sasa ukipigwa tukio usitusumbue oooh bora nife-kufaaaaaa
Huwezi ukaishi Kwa Akili na kitu au na MTU usiyemjua wala kumuelewa.
Unapomzungumzia Akili unazungumzia ufahamu, Uelewa, utambuzi, kumbukumbu, maarifa, ujuzi, kuchambua na kuchanganua.
Kitendo cha kushindwa kumjua au kumuelewa Mwanamke unayeishi naye kinamaanisha huna Akili ya kuishi naye, yaani huwezi kuishi naye.
Mapungufu ya Wanawake hasa ya kitabia kama kutokuwa waaminifu au kuwa Wanafiki, ni mapungufu ambayo hata wanaume wengi tunayo.
Ungemuuliza huyo Rafiki yako yeye hachepuki?
Au Kwa vile Sisi wanaume hatubebi mimba?
Mwanamke kuchepuka haimfanyi yeye awe kiumbe kisichoeleweka.
Kosa kubwa Watu wengi wanalolifanya ni kum-term Mwanamke as if sio binadamu kama tulivyo Sisi Wanaume.
MWANAMKE ni binadamu kama alivyomwanaume, anatamaa ya mwili, naye anatamani wanaume wengine zaidi ya Mume aliyemuoa kama ilivyo Sisi Wanaume tunavyotamani Wanawake.
Stara na aibu ya Mwanamke kujifanya ni wastaarabu Hali inayowafanya Wanawake kuwa pretenders ndio kunawachanganya Watu wengi na kudhani wao hawapo kama Sisi. 😂😂
Jinsi unavyojiona mwanaume ulivyo ndivyo hivyohivyo Mwanamke alivyo, tofauti iliyopo haizidi 10%