Wanaojifanya wanaikubali ndoa wengi wao ni Makatili na watesaji Wakuu

Wanaojifanya wanaikubali ndoa wengi wao ni Makatili na watesaji Wakuu

MTU anasema yupo ndoani alafu jioni lipo na mchepuko au hawara, mpaka unajiuliza huyu anajua maana ya Ndoa Kweli?

Ndoa ni UPENDO. Na MTU mwenye upendo hawezi kuchepuka wala kumfanya mwenza wake ateseke.
Usitujumuishe Me sote tuliooa kwenye tabia za kipumbavu.

Tuliojaliwa Wake wema na Mungu tunaendelea kula mema ya nchi na hatutishwi wala kubabaishwa na Michepuko zaidi ya mwaka wa 5 hivi sasa [emoji38]

Kama ulikosea njia pole, Mungu awape neema nanyi mpate Wake wema [emoji847]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Palipo na giza kuna nuru.. hakuna ngetive bila positive... Walio naupendo na utii wapo na ambao wamepinda wapi.. Mungu anakupa cha kufanan nacho.. kama unashinda kutia malaya iwaje akuletee kilichobora ili ukiumize ? Utapewa wa type yako.. Shida sio ndoa mbaya au haifai.. Tatizo lipo katika mtindo mzima wa makuzi na malezi watu wamekuwa na tabia chafu kama ibilisi.. ndoa tamu banaaa
Shangaa hata wewe, Dume linajisifia tu kila siku jinsi linavyotafuna Ke kimasihara afu likipewa Malaya wa kufanana naye linaibuka na sera za kijinga humu kulaani ndoa mbaya likihamasisha Watu wengine wasioe kisa tu lenyewe halikubarikiwa [emoji23]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Usitumuishe Me sote tuliooa kwenye tabia za kipumbavu.

Tuliojaliwa Wake wema na Mungu tunaendelea kula mema ya nchi na hatutushwi wala kubabaishwa na Michepuko zaidi ya mwaka wa 5 hivi sasa [emoji38]

Kama ulikosea njia pole, Mungu awape neema nanyi mpate Wake wema [emoji847]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app

😀😀😀
Acha Vitisho Mkuu.
 
[emoji3][emoji3][emoji3]
Acha Vitisho Mkuu.
Ikiwa Mungu ni Babu yangu basi sawa, ila ikiwa ninachoeleza hapa namaanisha basi amini tu hivyo.

Maombi yanatakiwa sana katika ndoa maana usidhani hata hapa ninapojinasibu kudumu muda wote huo bila ya kuchepuka ni rahisi kuendeleza hivyo maana shetani huchukia sana ndoa na huwinda Wanandoa kila siku kwa mitihani tofauti ilimradi tu ndoa zivunjike.

Mungu atusaidie tuwe na hekima tele katika ndoa zetu, Amina.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
WANAOJIFANYA WANAIKUBALI NDOA WENGI WAO NI MAKATILI NA WATESAJI WAKUU.

Anaandika, Robert Heriel.
Kuhani.

Ndoa ni nzuri. Ndoa ni tamu Sana. Ndoa inahitaji upendo wa kweli, sio huu upendo wa kinafiki nafiki. Pamoja na uzuri WA ndoa lakini ndoa sio lazima ikiwa hakuna Upendo WA kweli. Mambo ya kulazimisha Watu waoe au waolewe bila kujali nguzo kuu ya Ndoa ambayo ni upendo ni ukatili na utesaji Mkuu.

Ndoa ni heshima sio kufehedheshana,
Ndoa ni kupeana Raha sio kurushana Roho.
Ndoa ni kusaidizana na sio kutumikishana na kugeuzana watumwa na misukule.

Wanaoikubali ndoa ukiwafuatilia Kwa ndani kabisa ni Wanafiki, MAKATILI na WATESAJI wakubwa wa wenza wao.
Wafuata Mkumbo, Kwa vile jamii inasema hivi nao wanasema hivyohivyo.

Unafiki nafiki wa kipumbavu ndio Sisi Akina Taikon tulishaukataaga.

Yaani Taikon nijibadilishe tabia zangu ninazozipenda na zinazonifurahisha ati ili nipate MKE, seriously! Tabia zangu ziwe nzuri au Mbaya nitazihirisha waziwazi ili Watu wanaofanana na Mimi wanipate kirahisi ili tuishi Maisha Real pasipo kutesana na kumuumiza yeyote. Anayetaka kuingia kwenye circle yangu atakubaliana na vile nilivyo. Hivyo ndio namna nzuri ya kuishi Maisha ya furaha na Amani na wanaokuzunguka.

Unaoa Wakati huwezi ishi na Mwanamke mmoja, unajua kabisa utakuwa na michepuko na utamuumiza Mkeo lakini unakazana kuoa. Wewe ni Katili na mtesaji Mkuu. Ndoa inahitaji uaminifu Kwa wanandoa wote Wawili. Uaminifu hauna Excuse kuwa sijui Mimi ni Mwanaume hivyo ninatamaa, ni ubinafsi, na kushindwa kuzuia tamaa ya Mwili.

Unakubali Kuolewa Wakati unajua kabisa wewe ni Mwanamke unayependa upewe tuu, kila kitu uhudumiwe kama maiti. Yaani umemgeuza kijana wa Watu Msukule wako wa kukufanyia kila kitu. Hayo ni mateso, huo ni ukatili.

Kijana usioe Mwanamke ambaye CHAKE NI CHAKE na chako ni cha wote. Huyo atakufanya uwe mtumwa, Msukule, kibobojo.

Ndoa ni Taasisi ya UMOJA na USHIRIKIANO. Mambo ya ubinafsi huondoa maana yandoa.

Unashangaa ati Pesa ya MKE haijulikani inamatumizi gani, mwanaume naye hataki kuulizwa mapato na matumizi, mpaka unajiuliza hawa ni vichaa au wendawazimu. Wewe kama hutaki Pesa na Mali yako iwe ya familia, usioe wala kuingia kwenye Ndoa. Ubinafsi na matabia ya hovyo unayo alafu unataka kuoa au kuolewa. Kenge wewe!

Unakuta jitu linajijua kabisa ni lilevi na linashindwa kujizuia na ulevi wake, linathamini kampani za nje na marafiki kuliko MKE, alafu linataka Kuoa. Mpaka unajiuliza hata huyo Mwanamke anayeolewa na MTU mjinga kama huyu anaakili au anamatope kichwani.

Kuwa mwanaume haikupi mamlaka ya kutesa hisia za Mkeo na watoto. Jambo lolote ambalo halikufurahishi wewe ukifanyiwa basi usimfanyie mwenza wako.

Kampani yako ya Kwanza ni familia. Kama wewe ni MTU wa Bar au Michezo basi toka na Mkeo au familia yako.
Vinginevyo hakuna maana ya Ndoa.

Mara mojamoja ndio utoke na Marafiki lakini sio mara mojamoja ATI ndio unatoka na Familia Baada ya kuwatesa Kwa Mwaka mzima.

Kama unapenda Kutoka hata Mkeo anataka Kutoka, kama unapenda Mpira elewa hata Mkeo anaweza kutaka hayo.

Vinginevyo Mkeo awe radhi, yaani asiwe na shida. Lakini kama inamuuma basi usimtese wala kumfanyia ukatili.

Alafu Wanawake wenyewe wameshazoea mateso mpaka wameyafanya ni Haki zao. Kama majinga.
Ni kama vile wanaume tulivyozoeshwa mateso ya kutoa Huduma ya kila kitu mpaka tumeona ni haki. Kumbe ni mateso.

Unaoa Mwanamke tambua kuna mambo anayapenda kama kucheza muziki, mambo ya kumfanya mfungwa ni mateso makubwa, MTU kama Mkeo anapenda muziki, muwekee muziki acheze asikilize afurahi, nendeni Night Club kachezeni Muziki. Hiyo ndio ndoa yenyewe. Ndoa ni furaha. Sio kuwekeana misheria miiiingi isiyo na kichwa wala miguu.

Wewe Kam hutaki Mwanamke asiyependa muziki ungeoa huyo asiyependa muziki. Sio uoe apendaye muziki alafu utake kumbadilisha asipende Muziki. Upuuzi mtupu.

Kijana anayetaka kukuoa unafahamu kabisa ni Mnywaji wa pombe, ndio starehe yake alafu unamlazimisha aache pombe Ati anakukera. Yaani umtese kijana watu kisa nini, tafuta ambaye hanywi. Mnaefanana.

Hutaki Kulea mtoto wa mwanaume mwenzako alafu muda huohuo unataka kuoa single mother, wewe ni chizi, wewe ni mtesaji, mkatili. Elewa kuwa kuoa single mother ni kuamua kuingia kwenye familia ya MKE mmoja waume Wawili au zaidi. Mawivu yako ya kijinga yasigeuke mateso Kwa mwenza wako.

Sasa Mkeo asiongee na Mzazi mwenzake kisa nini, kisa umemuoa wewe sio, wewe chizi Kweli.

Ndoa sio kuvumiliana, unavumiliana nini?
Mkiwa mnafanana hakuna kuvumiliana Bali mnaishi Maisha yenu kwani ninyi ndio mpo hivyo.
Kama ni walevi wote ni walevi. Hapo hakuna kuvumiliana Bali ni bata tuu mwanzo mwisho.

Unaoolewa na jitu gomvi, korofi, linapenda kupiga hovyohovyo kama kichaa. Alafu wewe sio WA type hiyo unategemea nini kama sio Ndoa ndoano, na Yale mawaidha ya kuvumiliana.

Acha wakorofi waoane wao Kwa wao.

Mambo ya kusema atabadilika Achana nayo hayo. Ni Akili za kitoto na watu wenye Upeo mdogo. Kwa nini uchukue kitu ambacho unabet kitabadilika Wakati vipo vitu ambavyo tayari vipo unavyotaka viwe.

Ndoa sio sehemu ya kutesana, ndoa sio sehemu ya kutumikishana, ndoa sio sehemu ya kubadilishana Hobby, ndoto, furaha n.k.

Ni sehemu ambayo Watu wanaofanana wenye jinsia tofauti wanakutana kufanya Maisha pamoja. Kufurahia mambo yao, maumbile Yao, Tabia zao, shida zao, na hatma Yao.

Vijana nisikieni Mimi Taikon, ndiye Kuhani. Msitafuta au msitafutiwe mateso na ukatili WA hiyari Kwa kile kiitwacho Ndoa.

Chagueni wenza mnaofanana kitabia, ndio maana mahusiano yanapaswa yaanzie kwenye urafiki, kisha uchumba ndipo NDOA. Ili mjiridhishe kuwa mnafanana kweli au ni kuingia katika GEREZA la hiyari la mateso.

Taikon nimemaliza. Hujanielewa ruhusa kuulizwa swali

Nawatakia Sabato NJEMA

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Unakataa ndoa ila unazini, uasherati kutwa kucha. Hii ni agenda ya devil worshipers. Haita fanikiwa.
 
Mtu kama hutaki kuoa bora uolewee. Acheni kelele zenuu
 
Mmwagie

Sepa..we lea tu mtoto

Full stop

Mambo ya ndoa sahv kusumbuana tu

Ova
shida ya wanaume wengi hawawezi toa hela ya kulea mtoto bila kuleta mambo ya feelings ni ngumuu... yani utajikutaa unataka tu uchiii hapo ndo tatizo linapoanza!! na akibana hutaki kutuma tena helaaaa.
 
shida ya wanaume wengi hawawezi toa hela ya kulea mtoto bila kuleta mambo ya feelings ni ngumuu... yani utajikutaa unataka tu uchiii hapo ndo tatizo linapoanza!! na akibana hutaki kutuma tena helaaaa.

😂😂😂😂
Na hapo ndipo Vijana hawataki kuoa single mother Kwa sababu wanajua Tabia za kiume zilivyo
 
Ikiwa Mungu ni Babu yangu basi sawa, ila ikiwa ninachoeleza hapa namaanisha basi amini tu hivyo.

Maombi yanatakiwa sana katika ndoa maana usidhani hata hapa ninapojinasibu kudumu muda wote huo bila ya kuchepuka ni rahisi kuendeleza hivyo maana shetani huchukia sana ndoa na huwinda Wanandoa kila siku kwa mitihani tofauti ilimradi tu ndoa zivunjike.

Mungu atusaidie tuwe na hekima tele katika ndoa zetu, Amina.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app

Kuchepuka ni maamuzi tuu ya MTU.
Mazingira pia yanachangia Kwa sehemu kubwa
 
Unakataa ndoa ila unazini, uasherati kutwa kucha. Hii ni agenda ya devil worshipers. Haita fanikiwa.

Alafu unakubali ndoa, umeoa alafu muda huohuo unazini na kufanya uasherati kutwa kuchwa. Hiyo ni agenda ya devil worshippers
 
Aisee acheni unafiki ya nini unapinga ndoa halafu hapo hapo unataka kufanya ngono na mwanamke?
Hutaki ndoa basi acha kufanya ngono baki hivyo hivyo au piga punyeto.
 
Back
Top Bottom