Fundi...
Hakuna mtikisiko wowote mitaani.
Hawa wananchi walioko katika viwanja vya mikutano ya CHADEMA wako mbali sana na wahamaji chama.
Hili mosi.
Pili hawa wameshatoka CHADEMA.
Wanapo pengine pa kuwasiliana na wananchi?
Sijui kama wanatambua wanakuwa News kwa kutangaza kutoka CHADEMA.
Baada ya kutoka CHADEMA...
Wanapotea hakuna anaewakumbuka.
Mohamed,
Ulitegemea mtikisiko gani? Kuwa watu waandamane mtaani kuwaunga mkono? Usilinganishe kuondoka kwao na walivyoondoka wakina Maalim CUF. CUF palikuwa na msuguano wa muda mrefu ambao uli play out in public. Hawa relatively kimya kimya. Watu wachache wachache wanaita presa wanasema wamejitoa kwenye uanachama, wanatoa sababu zao wanasepa. Kikundi chao hakina kiongozi wa wazi kama ilivyokuwa kwa kundi la Maalim.
Mtikisiko ungetokea kama wangejiuzulu pamoja na Mbowe. Hawa strategy yao ni tofauti kabisa na ya CUF/ Maalim na hata CDM. Badala ya kulenga kuwa na impact nationally, wanalenga kuwa na impact kila mmoja katika constituency yake. Watu kama Catherine Ruge, Suzan Kiwanga, Devota Minja n.k. wote wana watu ambao wanawaamini. Wanachokifanya ni kuwa watatengeneza platform wale ambao bado wana tumaini la kugombea wataweza kukimbilia. G-55 itaendeleza mpambano katika ngazi ya majimbo ya uchaguzi. Wakati wa uchaguzi watapambana kuhakikisha kuwa wanatendewa haki maana wengi wao ni wapambanaji wazuri. Hata kama watadhulumiwa tena lakini wataonekana wakipambana.Ukifika wakati wa uteuzi wa wagombea ndio tutajua nani kweli ni muumini wa dhati wa NRNE na nani wanafuata mkumbo.
Unauliza kama watakuwa na platform nyingine ya kuwasiliana na wananchi nje ya Chadema? Ni hivi:
1. Chadema haitashiriki katika uchaguzi wa mwaka huu na mwaka 2029. Kwa sababu hiyo hawatakuwa na platform ya kuongea na wananchi wakati wa kampeni za uchaguzi. Kitu pekee watakachoweza kuongelea ni NRNE. Hawataweza kusimama majukwaani kunadi sera zao na kuwaeleza wananchi namna ambavyo wao watakuwa bora kuliko CCM kama wakichaguliwa. Kama ikifika mwezi wanane bila ya wao kutoa maelekezo ya nini wanachama wao wanatakiwa kufanya ili uchaguzi usifanyike watu wataanza kuwachoka.
2. Baadhi ya G55 watagombea uchaguzi kupitia chama kingine na wengine wataungana na wenzao kupambana na CCM. Watu watawasikia na wataendelea kuwaona wakiwapambania. Aidha, watakuwa na muda wa kutosha wa kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa 2029 na 200.
3. Baada ya uchaguzi, Lissu na Lema watatumia muda mwingi na familia zao nje ya nchi.
4. Hali ya kifedha itazidi kuwa ngumu kwa CDM na watu wataanza kulaumiana kwa kufikishana watakapokuwa wamefikia.
5. Wanachama zaidi wa CDM watawafuata G-55 huko waliko.
6. CDM itafifia lakini haitakufa.
Hii hali haikutakiwa ifikie hapa ilipofika. Uongozi wa sasa wangeweza kuithibiti kwa kuhakikisha kuwa wanachama wote wa CDM wanaheshimiwa. Ingawa Mbowe alishindwa uchaguzi lakini bado yuko moyoni mwa wanachama wengi wa CDM. Kuachia watu wamtukane na kumkebehi kunawaumiza watu wengi kuliko wanavyodhani.
Amandla...