Fundi...
Chama kinapata nguvu kutoka kwa wanachama.
Huna watu ni sawasawa na mtoto yatima.
Mohamed,
Nguvu ya chama ni wafuasi wake na sio wanachama. Act Wazalendo ina nguvu Zanzibar sio kwa sababu ina wanachama wengi bali ina wafuasi wengi ambao wengine ni wanachama wa vyama vingine.
Hatuna haja ya kujadili tatizo la uchaguzi nchini petu kwani sote tunajua yaliyotokea huko nyuma.
Uwanja wa uchaguzi una mabonde
Unahitaji kunyooshwa kwanza uwe sawa ndipo timu ziingie uwanjani kucheza.
Uchaguzi unaweza kufanyika.
Ila suala kubwa litakuwa kweli ni uchaguzi na demokrasia Tanzania inayotaka kujenga?
Ukweli utakuwa wazi kuwa tumeshindwa na dunia itaona kweli tumefeli pakubwa.
Tanzania itakuwa kichekesho cha ulimwengu.
Kwa bahati mbaya dunia haijali hicho unachosema. Nchi nyingi hazina uchaguzi wa haki na uwazi lakini zinakubalika na wenye nguvu duniani. Marekani wana kitu kinaitwa gerrymandering ambapo mipaka ya majimbo ya uchaguzi inawekwa ili chama kimoja kishinde uchaguzi hata kama kimepigiwa kura na wachache. Chama dola kinabadilisha mfumo wa uchaguzi ili kuzuia wapinzani wao kupiga kura. Vitu kama kutaka wapiga kura wawe na vitambulisho vyennye picha wakijua kuwa kuna wengi tu watashindwa kuvipata. Kuweka vituo vichache vya kupigia kura katika maeneo yenye wafuasi wengi wa chama cha upinzani. Lakini hakuna nchi inayofikiria kuiwekea vikwazo Marekani.
Hiyo EU inayotegemewa, ina nchi ya Hungary ndani yake na imeshindwa kuishughulikia.
Sasa hapa tutaweza kama nchi kukubali kuwa kichekesho cha Afrika au tujitoe kuwa wachekeshaji tufanye mabadiliko ili tuwe na heshima mbele ya jamii ya kimataifa.
Niambie lini tumekuwa na uchaguzi huru na wa haki na lini tumetengwa na dunia? Hizo nchi za kiafrika zitatucheka vipi wakati nyingi hazifanyi hata maigizo ya uchaguzi! Kiongozi wa Saudi alimchinja Khashoggi, amefunga watu wengi lakini ndio nchi ya kwanza iliyotembelewa rasmi na Rais wa Marekani!
Fidel Castro baada ya msukosuko mkubwa aliandika kitabu: "History Will Absolve Me."
Mandela kaandika: "Long Walk to Freedom."
Ndani ya vitabu hivi kuna mafunzo makubwa.
Castro alikuwa dikteta hivyo sio mfano sahihi wa mtu aliyependa demokrasi.
Mandela ni mfano wa kuigwa kwa matendo aliyofanya baada ya kushika hatama na sio kitabu chake.
Si lazima haki isimame leo kama vile haikusimama kwa Castro na Mandela kwa siku moja.
Kupata haki kunataka subira na kujtolea kukubwa sana.
Sijakuelewa hapa una maanisha nini.
Bahati mbaya sana wahamaji chama hawaelezi katika hotuba zao za kuhama viti vingapi CHADEMA ingeshinda kwa kushiriki uchaguzi.
Mimi sielewi hiyo inasaidia vipi maana ni projections tu. Kinachojulikana kwa uhakika ni kuwa Chadema haitashinda kiti hata kimoja kama haitashiriki kwenye uchaguzi.
G-55 ikipata hata mbunge mmoja watakuwa wamekishinda CDM. Na tumeona namna chama hata kikiwa na mbunge mmoja tu ambae ni committed (kama ilivyo kwa CDM) anavyoweza kusukuma ajenda yake.
Hili ni muhimu kupita kiasi.
Bahati mbaya sana hotuba zao zimefanana na zile za "kuunga juhudi," kama vile mwandishi ni yule yule.
Hotuba zao zitatofautiana vipi wakati sababu zao za kutoka Chadema zinafanana.? Badala ya kuzibeza, kiongozi makini angezifanyia kazi ili wengine wasitoke.
Huenda CHADEMA inaandika historia na Iko siku itasomwa na kufanyiwa rejea kama leo zinavyofanyiwa rejea historia za wengine kama sisi.
Pengine. Lakini kinachotokea kwa Chadema sasa hivi tulikiona kwa NCCR Mageuzi ya Mrema. Popularity ya sera za Mtikila hazijawahi ku translate kuwa kura za chama chake.
Hii sio mara ya kwanza kwa Chadema kususia uchaguzi. Ilijitoa katika uchaguzi wa serikali za mitaa na hamna kilicho badilika. Chama cha Maalim kilisusia uchaguzi wa marudio Zanzibar na hapakuwa na mabadiliko yeyote. Leo ACT Wazalendo haiko tayari kususia uchaguzi kwa sababu hiyo hiyo. Pamoja na uonevu wanaofanyiwa bado wanashiriki katika uchaguzi.
Dada mmoja wa G-55 alisema kuwa ukiisusia CCM sinia la chakula watakuka chakula chote bila chembe la aibu. Hii Chadema ya Lissu itakumbukwa kwa kuchezea shilingi chooni. Itakuwa mfano wa nini cha kutofanya katika nchi kama Tanzania.
CCM haijali inashinda vipi uchaguzi mradi inashinda. Na inajua this kuwa serikali ya JMT haitatengwa na dunia hata kama uchaguzi hautakuwa wa haki.
Wakina Lissu pamoja na kujaza watu kwenye mikutano wameshindwa ku articulate watahakikisha vipi uchaguzi haufanyiki. Na watafanya nini kama utafanyika. Angalau G-55 wana strategy iliyo wazi.
Kuwalinganisha na wakina Msigwa na Lijualikali hakuwatendei haki. Wanastahili heshima hata kama wamejitoa CDM.
CDM ingewatendea haki ingenuity katika historia kutoa fundisho kuwa demokrasia inawezekana ndani ya chama kama ambavyo walituonyesha katika uchaguzi wao Mkuu.
Ni upuuzi kuwaiti G-55 wasaliti kwa kufanya kile kile ambacho wakina Lissu walifanya dhidi ya msimamo wa chama chao kuhusu mpango wa maridhiano.
Oktoba 2025 na 2030 sio mbali. Tutaona nani yuko sahihi.
Amandla...