Ndugu yangu
Mohamed Said, habari za siku nyingi. Nadhani tunajuana vizuri tu...tumetoka mbali na
tumewahi kuwa na minakasha si haba.
Nyakati nyingi hatukukubaliana lakini kwenye jambo la wazi kama hoja uliyoiweka hapa
tuko pamoja lakini kwa tofauti dogo tu katika mtazamo,
Mtazamo huo unaoutofautisha ni mdogo sana lakini una ujumbe mzito;
wakati wewe unashangazwaa kwa yanayojiri, mimi sishangai hata kidogo.
Sishangai kwa sababu niliyategemea haya na sasa yanatokea kama nilivyoyatabiri. Mimi siyo nabii ila huwa
najifanyia tafiti zangu japo si mtafiti kwa maana ya kusomea.
Katika lugha ya Kiingereza kuna maneno mawili yanayoelezea ukweli,
fact na
truth. Neno ukweli (fact) linahitaji ushahidi (evidence), lakini neno ukweli (truth) huwa ni self-evident.
Katika utafiti wangu uchwara, nilimshauri Mh. Mbowe asigombee
kulinda heshima yake aliyoijenga kwa kipindi kirefu cha zaidi ya miaka ishirini!
Hata Mh. Mbowe mwenyewe awali, toka 2019, alionesha kusita kugombea
lakini vongozi ambao kwa sasa ndilo hili kundi linalojiita G-55 walimshauri tofauti.
Kwa mara ya kwanza Mh. Mbowe akaonesha udhaifu ambao ulituacha wengine tulio na nia nzuri midomo wazi.
Na sasa Mh. Mbowe anavuna alichopanda.
Chadema ilichagua uongozi mpya
katika uchaguzi ulioendeshwa kwa haki, uwazi na bila mizengwe aina ya tuliyoishi nayo kwa kipindi kirefu toka mwaka 1995.
Niliposikia dukuduku za
waliojiita G-55, niliwapa tahadhari wasi-
underestimate nguvu na ushawishi waliokuwa nao viongozi wapya kwa wananchama wa Chadema.
Hii ni Chadema mpya, chama cha wananchi ambacho kila mwanachama kwa uchungu wake
yuko tayari kupitia TONE TONE kukichangia hata kile kidogo alicho nacho.
Namshauri tena Mh. Mbowe asione haya, hajachelewa, aachane na
kakikundi haka ambacho kiko tayari Chadema ife lakini mikono yao iende kinywani, aluta contonua!
Chadema haisambaratiki labda nguvu ya ziada itumike kuwateka, kuwaua na kuwapoteza mamilioni ya wananchi ambao kwa sasa ndio wafadhili wakuu wa Chadema.