Wanaoondoka CHADEMA ni waliokuwa Viongozi peke yao, Vipi Wanachama?

Wanaoondoka CHADEMA ni waliokuwa Viongozi peke yao, Vipi Wanachama?

huyo hana tofauti na msigwa nayesema, et jamani si mnaona uwanja ulivyo? huku sura na roho vikiwa havina ushirikiano.
Na sasa hivi hakuna hata anayemzungumzia, kwisha habari yake, tusubiri na haya madunduka hayana muda wala impact
 
Narudia tena, matamanio yako wazi. Jitahidi usibadili hadithi.
Ndio zenu hizo. Mnapenda kuwa zushia watu. Mtu kuikosoa Chadema haimaanishi kuwa anataka ife. Mtazamo huo ndio umewafikisha hapa mlipofika. Nimemsikiliza Asia na Yosepher wakitangaza kwa uchungu mkubwa kujitoa Chadema. Mpaka sasa hivi sijasikia hata mtu mmoja akitangaza kujitoa kwa furaha. Lakini hiyo haitawazuia kuwatukana.

Amandla...
 
Ugumu unakuja kutokana na Bajeti ya manunuzi kushindwa kutosheleza, Inatosha kununua watu 10 lakini haitoshi kununua watu mil 1

Kumbuka kwamba wanaonunuliwa wameahidiwa pia kuhudumiwa kwa ajili ya kujikimu na ikiwezekana vyeo pia
Wakipewa vyeo wataongoza wannanchi wajinga kama wao, kama watakwepo....!

Inashangaza sana vyombo vya habari vinajitahidi kutoa coverage ya huu upuuzi wa kuhamahama Kila siku!
 
Wachina wana msemo, ''May you live in interesting times,'' yaani inapendenza kuishi wakati mambo yanatokea.

Nimejitahidi kueleza maana ya msemo huu kwa Kiswahili ingawa yawezekana pakawa na tafsiri bora zaidi.

Kila nikiangalia video ya viongozi wa CHADEMA ni viongozi peke yao ndiyo wanatoka chama na viongozi siku zote huwa watu wachache.

Hawa viongozi wanatoka chama lakini cha kustaajabisha sioni hata mwanachama mmoja kuwasindikiza.

Inanishangaza.

Kila nikiangalia mikutano ya CHADEMA mathalan mkutano wa Nyamagana Mwanza, kisha Mugumu, Musoma na kwengineko na kuangalia watu
wanaohudhuria mikutano hii kisha wanachama wa CHADEMA wanajikusanya
baada ya mkutano kuwasindikiza viongozi wao...

Ndugu yangu msomaji hebu malizia sentensi hiyo hapo juu.

Viongozi wanatoka chama na wanachama wa CHADEMA mtaani hawana
habari na viongozi hawa inanishangaza sana.

Kuna kitu hakijakaa sawa.

Naona kuna kitu hakijakaa sawa kati ya viongozi wanaotoka chama na wanachama
wabeba kadi za CHADEMA wanaojazana katika mikutano ya hadhara ya CHADEMA
kisha wakawasindikiza viongozi wao kwa shamra shamra baada ya mikutano.

Sijui kama na nyie wenzangu hili mnaliona.
Upo sahihi kabisa Mzee Mohamed Said ,ngoja tuone labda wafuasi wao watawafuata huko?

Tindo Pascal Mayalla Mag3 JokaKuu
 
Una hakika kuwa mimi ni Mrema? Ukiniita Mimi sitapata faida yeyote CDM ikidhoofika. Nitasikitika kwa sababu kuna wakati niliiamini sana.

Ukiniita tena mjinga au tusi lingine nitakuweka kwenye ignore list yangu.

Amandla...
Huna tofauti na yeye. Maandishi yako hayaonyeshi kama utasikitika cdm ikifa, ila maombi yako usiku na mchana na hilo litokee, na hata lisipotokea utatengeneza nadharia kutaka kujifariji. Halafu kuniweka mimi kwenye ignore list si tatizo maana sina la kupoteza. Jenga tabia ya kuvumilia ukweli usioupenda.
 
Ndio zenu hizo. Mnapenda kuwa zushia watu. Mtu kuikosoa Chadema haimaanishi kuwa anataka ife. Mtazamo huo ndio umewafikisha hapa mlipofika. Nimemsikiliza Asia na Yosepher wakitangaza kwa uchungu mkubwa kujitoa Chadema. Mpaka sasa hivi sijasikia hata mtu mmoja akitangaza kujitoa kwa furaha. Lakini hiyo haitawazuia kuwatukana.

Amandla...
Hakuna anayekuzushia, unalazimisha nadharia zako ili zibebe hisia zako. Hapa tulipo tumefika wapi, ama unataka tuone kwamba hili la kuhama ni jambo geni? Nionyeshe kikao chochote ambacho Mbowe aliitisha wakati viongozi na wanachama wanahama kwenda kuunga juhudi. Kila siku kulikuwa na tuhuma za uchaga, na kukaa madarakani muda mrefu, mbona hukutumia nguvu kubwa kuonyesha sasa ndio kuna tatizo kuliko huko nyuma! Hiki unaochoongea hakina tofauti na anachoongea mrema, na anachojiapiza ni hiki hiki unachokiandika ww. Unataka nielewe vipi?
 
Huna tofauti na yeye. Maandishi yako hayaonyeshi kama utasikitika cdm ikifa, ila maombi yako usiku na mchana na hilo litokee, na hata lisipotokea utatengeneza nadharia kutaka kujifariji. Halafu kuniweka mimi kwenye ignore list si tatizo maana sina la kupoteza. Jenga tabia ya kuvumilia ukweli usioupenda.
Nisichovumilia ni matusi. Ukweli wako sio ukweli wangu. Sio lazima tukubaliane. Hicho ndicho usicho elewa.

Ila kama unaamini kuwa njia pekee ya kunishinda ni kwa kunitukana nitajitoa katika majadiliano na wewe. Nitakuweka katika ignore list yangu ili nijipunguzie matusi na kejeli.

Amandla...
 
Fundi,
Kuna kisa cha mtu alitezwa nguvu na aliyemshinda akachomoa upanga wake kumchinja.

Bahati ule upanga ikawa hauwezi kukata kwa kuwa ulikuwa hauna makali.

Yule bwana akamwacha pale chini yule mtu yeye akaenda mjini kuunoa upanga wake.

Aliporudi akamkuta yule jamaa yuko pale pale alipomuacha shingo yake juu ya kigogo anasubiri kuchinjwa.

Hakunyanyuka toka chini kujiokoa.
Hana uwezo wa kuelewa hapo, akili yake is so shallow akijilisha upepo CHADEMA kinakufa
 
Wachina wana msemo, ''May you live in interesting times,'' yaani inapendenza kuishi wakati mambo yanatokea.

Nimejitahidi kueleza maana ya msemo huu kwa Kiswahili ingawa yawezekana pakawa na tafsiri bora zaidi.

Kila nikiangalia video ya viongozi wa CHADEMA ni viongozi peke yao ndiyo wanatoka chama na viongozi siku zote huwa watu wachache.

Hawa viongozi wanatoka chama lakini cha kustaajabisha sioni hata mwanachama mmoja kuwasindikiza.

Inanishangaza.

Kila nikiangalia mikutano ya CHADEMA mathalan mkutano wa Nyamagana Mwanza, kisha Mugumu, Musoma na kwengineko na kuangalia watu
wanaohudhuria mikutano hii kisha wanachama wa CHADEMA wanajikusanya
baada ya mkutano kuwasindikiza viongozi wao...

Ndugu yangu msomaji hebu malizia sentensi hiyo hapo juu.

Viongozi wanatoka chama na wanachama wa CHADEMA mtaani hawana
habari na viongozi hawa inanishangaza sana.

Kuna kitu hakijakaa sawa.

Naona kuna kitu hakijakaa sawa kati ya viongozi wanaotoka chama na wanachama
wabeba kadi za CHADEMA wanaojazana katika mikutano ya hadhara ya CHADEMA
kisha wakawasindikiza viongozi wao kwa shamra shamra baada ya mikutano.

Sijui kama na nyie wenzangu hili mnaliona.
Kutokana na hili nimeboresha maana ya unyumbu wa kisiasa itakuwa ni

Unyumbu wa kisiasa ni mfumo wa kisiasa unao wezesha kurubuniwa mtu ama kundi Kwa hali na mali ili watu hao wakengeuke kwa kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwa kulitii kundi fulani, (linalo wezesha wakengeuke), kwa masilahi binafsi kwa kuzingatia usaliti na uoga wa kuigiza, (unafiki), a.k.a kujizima data

Hili kundi linalo fadhili watu wajizime data hufurahia wengine wakidhurika kwa namna yoyote ile, hata wakiishi kwa shida
 
Hakuna anayekuzushia, unalazimisha nadharia zako ili zibebe hisia zako. Hapa tulipo tumefika wapi, ama unataka tuone kwamba hili la kuhama ni jambo geni? Nionyeshe kikao chochote ambacho Mbowe aliitisha wakati viongozi na wanachama wanahama kwenda kuunga juhudi. Kila siku kulikuwa na tuhuma za uchaga, na kukaa madarakani muda mrefu, mbona hukutumia nguvu kubwa kuonyesha sasa ndio kuna tatizo kuliko huko nyuma! Hiki unaochoongea hakina tofauti na anachoongea mrema, na anachojiapiza ni hiki hiki unachokiandika ww. Unataka nielewe vipi?
Mbowe hakuitisha kikao kwa sababu aliheshimu haki yao ya kuhama. Ulitaka aite kikao cha kuwatukana kama mnavyofanya nyie?

Hilo la kukaa muda mrefu alilisikia ndio maana akafanikisha uchaguzi ambao ulimtoa madarakani. Na aliposhindwa akampisha aliyeshinda kwa moyo mkunjufu.

Kama watu mliamini kuwa Chadema ni chama cha wachaga, hata angefanya nini msingemkubalia. Kama ambavyo kuna watu wanaamini kuwa ni chama cha wakristu. Sasa ulitaka kuwe na quota Chadema?

Mimi sijamsikia Mrema akiapa kuwa Chadema itakufa. Ninachojua ni kuwa mtu aliyesema kuwa Chadema ina kikundi cha kuteka watu ndie mnasimama nae jukwaani. Na aliyejiunga na CCM na kutangaza kifo chake Iringa ni rafiki mkubwa wa viongozi wa sasa wa Chadema. Lakini hao huwaoni, unamuona Mrema kwa sababu tu ni mchaga!

Amandla...
 
Nisichovumilia ni matusi. Ukweli wako sio ukweli wangu. Sio lazima tukubaliane. Hicho ndicho usicho elewa.

Ila kama unaamini kuwa njia pekee ya kunishinda ni kwa kunitukana nitajitoa katika majadiliano na wewe. Nitakuweka katika ignore list yangu ili nijipunguzie matusi na kejeli.

Amandla...
G-55 wote huu ndio utetezi wao, na ww unatiririka katika mashairi yaleyale, what coincidence. Yaani ni kama mnajiona mna mawazo fulani ya maana ila mnatukanwa! Ww hata kukutukana ni kukupa sifa usiyostahili. Tafuteni utetezi mwingine sio wa kutukanwa boss. Nasisitiza, weka kikao Mbowe alichokaa na waliokuwa wanataka kwenda kuunga juhudi, ili tuone uongozi wa sasa unakosea kwa kutokaa na hawa waitisha press. Maana hata chaguzi za kihuni, bado cdm chini ya Mbowe walisusia kushiriki. Nasubiri hiyo agosti matamanio yako yafikie.
 
May you live in interesting times ilikuwa inatumika kama laana kwa sababu "interesting times" ndio zinakuwa na machafuko.

Amandla...
 
G-55 wote huu ndio utetezi wao, na ww unatiririka katika mashairi yaleyale, what coincidence. Yaani ni kama mnajiona mna mawazo fulani ya maana ila mnatukanwa!
G-55 hawajitetei bali wanaeleza umma sababu zilizowatoa Chadema. Kufanana kwa sababu hizo ni uthibitisho kuwa tatizo ni structural, sio la mtu mmoja mmoja.
Ww hata kukutukana ni kukupa sifa usiyostahili.
Nimekusikia.
Tafuteni utetezi mwingine sio wa kutukanwa boss.
kutukanwa ni mojawapo za sababu. Sababu kubwa ni kutofautiana na strategy ya Chadema ya NRNE. Na nyingine ni ya kutosikilizwa. Sasa kama Chadema kinaona ushauri wao hauna maana kwa nini kinawaandama wanapo amua kujitoa?
Nasisitiza, weka kikao Mbowe alichokaa na waliokuwa wanataka kwenda kuunga juhudi, ili tuone uongozi wa sasa unakosea kwa kutokaa na hawa waitisha press.
Waliounga juhudi hawakuweka wazi tofauti zao na Chadema wakati wako ndani ya chama. Walitangaza tu wameondoka. Msigwa ambae alitangaza wazi wazi tofauti zake na Mbowe pamoja na kutoridhishwa na matokeo ya uchaguzi wa Kanda ya Nyasa alikaribishwa kwenye kikao ambako angepewa nafasi ya kujenga hoja zake. Sasa ulitaka Mbowe aite kikao na wakina Lijualikali baada ya wao kuwa wanachama wa CCM?

Nionyeshe lini waunga juhudi waliandika waraka wa masikitiko yao au waliita presa KABLA ya kutangaza kuhama.

Wanachosema G-55 ni kuwa hawakupewa nafasi hiyo wakiwa bado ni wanachama pamoja na kuongea na kuundakia uongozi kuhusu changamoto walizo ona.

Agosti sio mbali.

Amandla...
 
Kutakuwa na wimbi la wanachama na viongozi wa CHADEMA litakalo ungana na G-55. CDM itabaki hai lakini itakuwa inaelekea ICU.

Amandla...
Unapiga ramli au na wewe mmoja wao?
Nakushauri kakojoe ulale, hakuna prominent figures kama dk Aman Walid Kaborou, Zitto Kabwe, dk Salaam na wale kenge walioenda kuunga juhudi na bado CHADEMA Iko imara.

Imani kubwa kwa wanachadema ni kwa Tundu Lissu na Heche, kama ukiwaondoa hao basi itatetereka lakini siyo hao kenge unaowapigia chapuo.

Hata wewe G55 huna impact humu wanaokuunga mkono hawafiki kumi.
 
Mbowe hakuitisha kikao kwa sababu aliheshimu haki yao ya kuhama. Ulitaka aite kikao cha kuwatukana kama mnavyofanya nyie?

Hilo la kukaa muda mrefu alilisikia ndio maana akafanikisha uchaguzi ambao ulimtoa madarakani. Na aliposhindwa akampisha aliyeshinda kwa moyo mkunjufu.

Kama watu mliamini kuwa Chadema ni chama cha wachaga, hata angefanya nini msingemkubalia. Kama ambavyo kuna watu wanaamini kuwa ni chama cha wakristu. Sasa ulitaka kuwe na quota Chadema?

Mimi sijamsikia Mrema akiapa kuwa Chadema itakufa. Ninachojua ni kuwa mtu aliyesema kuwa Chadema ina kikundi cha kuteka watu ndie mnasimama nae jukwaani. Na aliyejiunga na CCM na kutangaza kifo chake Iringa ni rafiki mkubwa wa viongozi wa sasa wa Chadema. Lakini hao huwaoni, unamuona Mrema kwa sababu tu ni mchaga!

Amandla...
Kwanini mnataka Lisu aitishe kikao sasa kwa hawa wanaoniita G55, wanapoondoka, na kumuona hana busara? Mbowe aliitisha kikao na Covid19 na hawakwenda na covid19 wanasema walihofia usalama wao, mbona na nyie G55 mnapita kwenye sababu hizo hizo?

Hakufanikisha uchaguzi ili uomtoe maana hakujiandaa kishindwa, ila alifedheheka kushindana na Lisu, kwani huko nyuma hakuwahi kushindana na mshindani mwenye nguvu. Na alishindwa kihalali maana uchaguzi haukuwa na mianya ya wizi, na ingekuwepo asingeshindwa. Na kwa kukusaidia Mbowe hajakubali kushindwa, na kama angekubali usingeona hili kundi lake kuzira, na yeye ndio yuko nyuma ya kinachoendelea.

Mimi kama mimi sikuamini kuwa cdm ni chama cha wachaga, ila Mbowe kutaka kufia madarakani akiwa kwenye hicho kiti, kulichangia sana propaganda hiyo kupata nguvu.

Ningeshangaa kama ungesema umemsikia Mrema akisema hivyo. Na hili ndio linalokufanya useme utaniweka kwenye ignore list. Yaani unajihukumuje kwa mfano? Huyo aliyesema cdm ina watu wa kuteka watu, yuko jukwaani na kaomba msamaha hadharani, ni juu ya polisi kumfuata awape ushahidi. Siasa si uadui na wala Msigwa hakuwa na tatizo na kila mwanacdm, bali alikuwa na tatizo na Mbowe. Ni juu ya Mbowe na Msigwa kutafutana waongee wayamalize, uzuri mnasema Mbowe ana busara, na Msigwa ni mchungaji wataelewana tu. Hilo la Mrema kuwa mchaga ni ww unajistukia ili upate mpenyo kwa urahisi kubadili mantiki ya hoja.
 
Back
Top Bottom