Wachina wana msemo, ''May you live in interesting times,'' yaani inapendenza kuishi wakati mambo yanatokea.
Nimejitahidi kueleza maana ya msemo huu kwa Kiswahili ingawa yawezekana pakawa na tafsiri bora zaidi.
Kila nikiangalia video ya viongozi wa CHADEMA ni viongozi peke yao ndiyo wanatoka chama na viongozi siku zote huwa watu wachache.
Hawa viongozi wanatoka chama lakini cha kustaajabisha sioni hata mwanachama mmoja kuwasindikiza.
Inanishangaza.
Kila nikiangalia mikutano ya CHADEMA mathalan mkutano wa Nyamagana Mwanza, kisha Mugumu, Musoma na kwengineko na kuangalia watu
wanaohudhuria mikutano hii kisha wanachama wa CHADEMA wanajikusanya
baada ya mkutano kuwasindikiza viongozi wao...
Ndugu yangu msomaji hebu malizia sentensi hiyo hapo juu.
Viongozi wanatoka chama na wanachama wa CHADEMA mtaani hawana
habari na viongozi hawa inanishangaza sana.
Kuna kitu hakijakaa sawa.
Naona kuna kitu hakijakaa sawa kati ya viongozi wanaotoka chama na wanachama
wabeba kadi za CHADEMA wanaojazana katika mikutano ya hadhara ya CHADEMA
kisha wakawasindikiza viongozi wao kwa shamra shamra baada ya mikutano.
Sijui kama na nyie wenzangu hili mnaliona.
Ndugu yangu
Mohamed Said, habari za siku nyingi. Nadhani tunajuana vizuri tu...tumetoka mbali na
tumewahi kuwa na minakasha si haba.
Nyakati nyingi hatukukubaliana lakini kwenye jambo la wazi kama hoja uliyoiweka hapa
tuko pamoja lakini kwa tofauti dogo tu katika mtazamo,
Mtazamo huo unaoutofautisha ni mdogo sana lakini una ujumbe mzito;
wakati wewe unashangazwaa kwa yanayojiri, mimi sishangai hata kidogo.
Sishangai kwa sababu niliyategemea haya na sasa yanatokea kama nilivyoyatabiri. Mimi siyo nabii ila huwa
najifanyia tafiti zangu japo si mtafiti kwa maana ya kusomea.
Katika lugha ya Kiingereza kuna maneno mawili yanayoelezea ukweli,
fact na
truth. Neno ukweli (fact) linahitaji ushahidi (evidence), lakini neno ukweli (truth) huwa ni self-evident.
Katika utafiti wangu uchwara, nilimshauri Mh. Mbowe asigombee
kulinda heshima yake aliyoijenga kwa kipindi kirefu cha zaidi ya miaka ishirini!
Hata Mh. Mbowe mwenyewe awali, toka 2019, alionesha kusita kugombea
lakini vongozi ambao kwa sasa ndilo hili kundi linalojiita G-55 walimshauri tofauti.
Kwa mara ya kwanza Mh. Mbowe akaonesha udhaifu ambao ulituacha wengine tulio na nia nzuri midomo wazi.
Na sasa Mh. Mbowe anavuna alichopanda.
Chadema ilichagua uongozi mpya
katika uchaguzi ulioendeshwa kwa haki, uwazi na bila mizengwe aina ya tuliyoishi nayo kwa kipindi kirefu toka mwaka 1995.
Niliposikia dukuduku za
waliojiita G-55, niliwapa tahadhari wasi-
underestimate nguvu na ushawishi waliokuwa nao viongozi wapya kwa wananchama wa Chadema.
Hii ni Chadema mpya, chama cha wananchi ambacho kila mwanachama kwa uchungu wake
yuko tayari kupitia TONE TONE kukichangia hata kile kidogo alicho nacho.
Namshauri tena Mh. Mbowe asione haya, hajachelewa, aachane na
kakikundi haka ambacho kiko tayari Chadema ife lakini mikono yao iende kinywani, aluta contonua!
Chadema haisambaratiki labda nguvu ya ziada itumike kuwateka, kuwaua na kuwapoteza mamilioni ya wananchi ambao kwa sasa ndio wafadhili wakuu wa Chadema.