Mohamed,
Ulitegemea mtikisiko gani? Kuwa watu waandamane mtaani kuwaunga mkono? Usilinganishe kuondoka kwao na walivyoondoka wakina Maalim CUF. CUF palikuwa na msuguano wa muda mrefu ambao uli play out in public. Hawa relatively kimya kimya. Watu wachache wachache wanaita presa wanasema wamejitoa kwenye uanachama, wanatoa sababu zao wanasepa. Kikundi chao hakina kiongozi wa wazi kama ilivyokuwa kwa kundi la Maalim.
Mtikisiko ungetokea kama wangejiuzulu pamoja na Mbowe. Hawa strategy yao ni tofauti kabisa na ya CUF/ Maalim na hata CDM. Badala ya kulenga kuwa na impact nationally, wanalenga kuwa na impact kila mmoja katika constituency yake. Watu kama Catherine Ruge, Suzan Kiwanga, Devota Minja n.k. wote wana watu ambao wanawaamini. Wanachokifanya ni kuwa watatengeneza platform wale ambao bado wana tumaini la kugombea wataweza kukimbilia. G-55 itaendeleza mpambano katika ngazi ya majimbo ya uchaguzi. Wakati wa uchaguzi watapambana kuhakikisha kuwa wanatendewa haki maana wengi wao ni wapambanaji wazuri. Hata kama watadhulumiwa tena lakini wataonekana wakipambana.Ukifika wakati wa uteuzi wa wagombea ndio tutajua nani kweli ni muumini wa dhati wa NRNE na nani wanafuata mkumbo.
Unauliza kama watakuwa na platform nyingine ya kuwasiliana na wananchi nje ya Chadema? Ni hivi:
1. Chadema haitashiriki katika uchaguzi wa mwaka huu na mwaka 2029. Kwa sababu hiyo hawatakuwa na platform ya kuongea na wananchi wakati wa kampeni za uchaguzi. Kitu pekee watakachoweza kuongelea ni NRNE. Hawataweza kusimama majukwaani kunadi sera zao na kuwaeleza wananchi namna ambavyo wao watakuwa bora kuliko CCM kama wakichaguliwa. Kama ikifika mwezi wanane bila ya wao kutoa maelekezo ya nini wanachama wao wanatakiwa kufanya ili uchaguzi usifanyike watu wataanza kuwachoka.
2. Baadhi ya G55 watagombea uchaguzi kupitia chama kingine na wengine wataungana na wenzao kupambana na CCM. Watu watawasikia na wataendelea kuwaona wakiwapambania. Aidha, watakuwa na muda wa kutosha wa kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa 2029 na 200.
3. Baada ya uchaguzi, Lissu na Lema watatumia muda mwingi na familia zao nje ya nchi.
4. Hali ya kifedha itazidi kuwa ngumu kwa CDM na watu wataanza kulaumiana kwa kufikishana watakapokuwa wamefikia.
5. Wanachama zaidi wa CDM watawafuata G-55 huko waliko.
6. CDM itafifia lakini haitakufa.
Hii hali haikutakiwa ifikie hapa ilipofika. Uongozi wa sasa wangeweza kuithibiti kwa kuhakikisha kuwa wanachama wote wa CDM wanaheshimiwa. Ingawa Mbowe alishindwa uchaguzi lakini bado yuko moyoni mwa wanachama wengi wa CDM. Kuachia watu wamtukane na kumkebehi kunawaumiza watu wengi kuliko wanavyodhani.
Amandla...
Fundi...
Chama kinapata nguvu kutoka kwa wanachama.
Huna watu ni sawasawa na mtoto yatima.
Hatuna haja ya kujadili tatizo la uchaguzi nchini petu kwani sote tunajua yaliyotokea huko nyuma.
Uwanja wa uchaguzi una mabonde
Unahitaji kunyooshwa kwanza uwe sawa ndipo timu ziingie uwanjani kucheza.
Uchaguzi unaweza kufanyika.
Ila suala kubwa litakuwa kweli ni uchaguzi na demokrasia Tanzania inayotaka kujenga?
Ukweli utakuwa wazi kuwa tumeshindwa na dunia itaona kweli tumefeli pakubwa.
Tanzania itakuwa kichekesho cha ulimwengu.
Sasa hapa tutaweza kama nchi kukubali kuwa kichekesho cha Afrika au tujitoe kuwa wachekeshaji tufanye mabadiliko ili tuwe na heshima mbele ya jamii ya kimataifa.
Fidel Castro baada ya msukosuko mkubwa aliandika kitabu: "History Will Absolve Me."
Mandela kaandika: "Long Walk to Freedom."
Ndani ya vitabu hivi kuna mafunzo makubwa.
Si lazima haki isimame leo kama vile haikusimama kwa Castro na Mandela kwa siku moja.
Kupata haki kunataka subira na kujtolea kukubwa sana.
Bahati mbaya sana wahamaji chama hawaelezi katika hotuba zao za kuhama viti vingapi CHADEMA ingeshinda kwa kushiriki uchaguzi.
Hili ni muhimu kupita kiasi.
Bahati mbaya sana hotuba zao zimefanana na zile za "kuunga juhudi," kama vile mwandishi ni yule yule.
Huenda CHADEMA inaandika historia na Iko siku itasomwa na kufanyiwa rejea kama leo zinavyofanyiwa rejea historia za wengine kama sisi.