Wanaoondoka CHADEMA ni waliokuwa Viongozi peke yao, Vipi Wanachama?

Unajua, wewe Mzee Mohamed Said mimi huwa sikukubali kwasababu siamini kama una akili timamu. Ebu nikuulize, Mzee Lowassa alipoondoka CCM alikuwa na wanachama wangapi aliondoka nao?
 
Nimefuatilia sana wengi wanao jitoa huko ni wa kaskazini hapo ndio nashangaa mwenyewe
 
Unajua, wewe Mzee Mohamed Said mimi huwa sikukubali kwasababu siamini kama una akili timamu. Ebu nikuulize, Mzee Lowassa alipoondoka CCM alikuwa na wanachama wangapi aliondoka nao?
Lowasa alisepa na Kijiji mkuu, na Cha kukumbusha tu ni kwamba lowasa alikuta chadema ikiwa na wanachama wa kutosha Sasa ACT na Hawa sijui Chuma oooh Chauma hata hawashtui.
 
Mohamed,
Ulitegemea mtikisiko gani? Kuwa watu waandamane mtaani kuwaunga mkono? Usilinganishe kuondoka kwao na walivyoondoka wakina Maalim CUF. CUF palikuwa na msuguano wa muda mrefu ambao uli play out in public. Hawa relatively kimya kimya. Watu wachache wachache wanaita presa wanasema wamejitoa kwenye uanachama, wanatoa sababu zao wanasepa. Kikundi chao hakina kiongozi wa wazi kama ilivyokuwa kwa kundi la Maalim.

Mtikisiko ungetokea kama wangejiuzulu pamoja na Mbowe. Hawa strategy yao ni tofauti kabisa na ya CUF/ Maalim na hata CDM. Badala ya kulenga kuwa na impact nationally, wanalenga kuwa na impact kila mmoja katika constituency yake. Watu kama Catherine Ruge, Suzan Kiwanga, Devota Minja n.k. wote wana watu ambao wanawaamini. Wanachokifanya ni kuwa watatengeneza platform wale ambao bado wana tumaini la kugombea wataweza kukimbilia. G-55 itaendeleza mpambano katika ngazi ya majimbo ya uchaguzi. Wakati wa uchaguzi watapambana kuhakikisha kuwa wanatendewa haki maana wengi wao ni wapambanaji wazuri. Hata kama watadhulumiwa tena lakini wataonekana wakipambana.Ukifika wakati wa uteuzi wa wagombea ndio tutajua nani kweli ni muumini wa dhati wa NRNE na nani wanafuata mkumbo.

Unauliza kama watakuwa na platform nyingine ya kuwasiliana na wananchi nje ya Chadema? Ni hivi:
1. Chadema haitashiriki katika uchaguzi wa mwaka huu na mwaka 2029. Kwa sababu hiyo hawatakuwa na platform ya kuongea na wananchi wakati wa kampeni za uchaguzi. Kitu pekee watakachoweza kuongelea ni NRNE. Hawataweza kusimama majukwaani kunadi sera zao na kuwaeleza wananchi namna ambavyo wao watakuwa bora kuliko CCM kama wakichaguliwa. Kama ikifika mwezi wanane bila ya wao kutoa maelekezo ya nini wanachama wao wanatakiwa kufanya ili uchaguzi usifanyike watu wataanza kuwachoka.
2. Baadhi ya G55 watagombea uchaguzi kupitia chama kingine na wengine wataungana na wenzao kupambana na CCM. Watu watawasikia na wataendelea kuwaona wakiwapambania. Aidha, watakuwa na muda wa kutosha wa kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa 2029 na 200.
3. Baada ya uchaguzi, Lissu na Lema watatumia muda mwingi na familia zao nje ya nchi.
4. Hali ya kifedha itazidi kuwa ngumu kwa CDM na watu wataanza kulaumiana kwa kufikishana watakapokuwa wamefikia.
5. Wanachama zaidi wa CDM watawafuata G-55 huko waliko.
6. CDM itafifia lakini haitakufa.

Hii hali haikutakiwa ifikie hapa ilipofika. Uongozi wa sasa wangeweza kuithibiti kwa kuhakikisha kuwa wanachama wote wa CDM wanaheshimiwa. Ingawa Mbowe alishindwa uchaguzi lakini bado yuko moyoni mwa wanachama wengi wa CDM. Kuachia watu wamtukane na kumkebehi kunawaumiza watu wengi kuliko wanavyodhani.

Amandla...
 
Mtoto...
Lowassa alikwenda CHADEMA kawakuta wanachama wanamsubiri.
Lowassa hakuwa na nguvu kiasi hivyo ndani ya Chadema maana weni walikuwa hawana imani nae. Kilichombeba Lowassa ni wafuasi wake waliokuwa bado CCM. Kura zao pamoja na za Chadema ndio zilimfikisha alipofika CDM. Baada ya uchaguzi akarudi nyuma. Pamoja na kuwa mgombea wa CDM, sikuwahi kumuona akiwa amevaa magwanda. CDM walimtumia kuongeza idadi ya wabunge pamoja na ruzuku.

Amandla...
 
Kuna mtu anaandika vitu visivyoeleweka halafu yeye ndiyo anataka kuonesha kuwa Mohamed Said haeleweki.

Hoja ya Mzee Said inajitosheleza tena Ina mashiko. Wanaotoka lengo lao lilikuwa kuleta taharuki lakini imeshindikana.

Mwanzoni waandishi wa habari walijazana lakini Sasa kutoka kwao CHADEMA siyo habari tena!
 
Bila shaka nilitegemea jibu la kipuuzi kutoka kwako. Anyway, kwanini alirudi CCM na akasema asiulizwe na mtu yoyote kwanini karudi?
Usianzishe mada ndani ya mada. Hoja ya Mzee Mohamed Said hukuizingatia wakati unaisoma.

Lowassa alikuta wanachadema wapo wanasubiri mgombea Urais. Lowassa alikuta CHADEMA Ina mtaji wa watu tayari.
 
Mzee mohamed hali ndo ilivyo sasa mtu kama salumu,mrema sijui kigaila nani anawajua?
Nimecheka jana kusikia Henry Kilewo kupiga beat kwamba Mwanga Cdm bila yeye haipo?! Hahaa
Huyuhuyu Kilewo aliekosa ubunge 2015 kwenye mafuriko ya lowasa ambapo cdm mkoa kilimanjaro wenye majimbo 9 walipata 7...
Naye kukosa jimbo...

Leo apiga mkwara??
 
Kila mwenye akili timamu anashangaa hii Hali bwana mkubwa ,Siasa zetu ngumu Mno....KWA HERI UKOLONI KWA HERI UHURU!
 
Hiyo ni rahisi kujibu. Viongozi wanaotaka wanajitangaza kwenye media ili wajulikane na Kwa kuwa wanauwezo wa kuwaita waandishi wa habari. Sasa usiwalinganishe hao viongozi na wanachama wa kawaida ambao pia ni wapiga kura. Hivyo basi jua ya kwamba Chadema ni mali ya wananchi si ya viongozi.
 
 
Nimecheka vibaya, eti watu wataichoka cdm maana haitashiri uchaguzi. Kwanza wengi tunaikubali cdm si kwa sababu inashiriki uchaguzi. Chaguzi karibu zote chini ya Magufuli cdm haikushiriki, na bado tulizidi kuikubali cdm. Ifahamike wakati wa Magufuli alipiga marufuku siasa za upinzani na lengo hasa ilikuwa ni ili kuiua cdm, mbona hatukuichoka? Kama ni kuhama walihama wengi enzi za kuunga juhudi. Cdm ni imani si kushiriki, na imani yetu kwao si kushiriki chaguzi za kishenzi.
 
Bila shaka nilitegemea jibu la kipuuzikutoka kwako. Anyway, kwanini alirudi CCM na akasema asiulizwe na mtu yoyote kwanini karudi?
Kwani Lowassa alikuwa cdm kwa itikadi, ama pesa zake ndio zilimpa nafasi ya kugombea urais kupitia cdm ili atimize ndoto yake ya kuwa rais baada ya kuikosa ndani ya ccm. Alirudi ccm maana alikuwa fisadi na aliona bora ajisalimishe kwa dhalimu magu baada ya kuanza kubwana kwenye miradi yake ya wizi, na Magu alijua Lowassa akirudi cdm atachangia kung'arisha utawala wake na itaoneka kaiua cdm.

Na kikubwa Lowassa alikuwa anaona anakaribia kung'ata udongo, hivyo akaona bora ajisalimishe ccm ili aendelee kupata stahiki zake, na akifa azikwe kwa heshima za serekali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…