Wanaosema kujenga ni kuzika pesa

Kujenga ni sawa na kuweka pesa benki yenye faida kuliko benki zote. Ila kama kuna uwezekano wa kuwekeza pesa zako kibiashara fanya hivyo ili ujenge nyumba nzuri zaidi.
 
Mi nina uhakika hati ya kiwanja unaiweka collateral bank na unapewa terms nzuri tu.
Usikariri maisha, hata furniture unaweka collateral bank.

Bank issue Yao sio collateral Kwa sababu hata wao lengo lao sio kuuza nyumba/ Kiwanja unapokwama kulipia. Wanazingatia uwezo wako wa kurejesha mkopo. Hawezi kukupatia tu mkopo kisa una viwanja kumi na hauna mzunguko wa kufanya uweze kurejesha mkopo Kwa wakati.

Ndio maana hata mortgage atapewa mfanyakazi anaelipwa mshahara japo hati ya nyumba au Kiwanja itatumika kama collateral.

Kama ni mfanya biashara lazima athibitishe na benki wajiaminishe kwamba ana uwezo wa kurejesha mkopo Kwa wakati.
 
Hii ni kwa personal loans.
Lakini kama huna kazi, huna income na una kiwanja unaweza kupata mkopo kwa ajili ya biashara.
Unaandika bussiness Plan, unatoa collateral (mradi iakisi gharama, na uhitaji wa soko), unapata loan.
mifano ipo mingi tu ili mradi ujue kujieleza.
 

Nakwambia hivi, hata kama ni wa biashara kikubwa lazima uonyeshe uwezo wa kulipia nje ya hiyo collateral. Nipe mfano mmoja tu wa mtu aliyeenda na business plan bila kuwa na cash flow ya kuonyesha atalipa vipi mkopo benki wakampatia pesa kisa ana collateral.

Hiyo hata iwe overdraft lazima wahakikishe unauwezo wa kulipia nje ya collateral unayoiweka
 
Wapi huko mzee naweza pata loan kwa collateral ya nyumba wakati sina kazi? Ebu nidadavhlie maana naweza kuwa nimekalia utajiri huku nahangaika na upepo kwenye bodabkda yangu
 
Kuna jamaa yangu mmoja hunasema ajenge ili iweje wakati hata Yesu hadi leo hii yuko kwa baba yake!
 
Mkuu unaweza toa darasa katika hiki kipande kwa mapana zaidi kuna elimu hapa inaweza tusaidia...pls.
 
Mkuu unaweza toa darasa katika hiki kipande kwa mapana zaidi kuna elimu hapa inaweza tusaidia...pls.
Kweli atule elimu maana tunaweza jikomboa kimaisha kupitia hii elimu. Majumba ya urithi tunayo ila ukienda benki wanakwambia unafanya biashara gani...ukiwajibu wee bodaboda wanakusonya tuu
 
Mkuu unaweza toa darasa katika hiki kipande kwa mapana zaidi kuna elimu hapa inaweza tusaidia...pls.
Kwa mfano kama unataka mkopo wa Bajaji au Guta NMB unapata kama una akaunti na ni mwanachama wa chama cha waendesha boda.
Lakini ukiangalia kwanini wanataka uwe mwanachama, basically wanataka ku-deal na biashara siyo personal loans kwa sababu personal loans ndiyo hayo mambo ya kazi.
Register kampuni hata ndogo Brela, andika bussiness plan nzuri ndogo halafu peleka NMB.
Itabidi uwe na maelezo mazuri na collateral itakusaidia.
That's all. Ni wewe tu utavyojieleza.
 
Hio nyumba utakayojenga sasa ili ikupe kodi ya laki 5 kwa mwezi haiwezi kuwa vikindu au chamazi ambako viwanja vya kujenga vinauzwa million 2!

Thamani ya kodi hupanda kulingana na ujenzi ulipofanyika kwa hio rationality ya kumdiss jamaa haipo. We umejenga Sinza mwenzio uwezo wake kujenga ni mkuranga sasa ana achieve vipi kodi ya laki 5? Ingekuwa popote unapojenga kodi ya laki 5 inapatikana basi ungekuwa sahihi hata mimi ningejenga
 
Thanks
 
Mimi nilipanga 300k kwa mwezi, nyumba yenyewe ni vyumba 2, sebule na jiko. Halafu haina matengenezo. Full kero. Nikaona ni ujinga huu. Nikajenga na sasa niko kwangu, full kujiachia. Watu
 
Hata mi ningemuelewa, angesema kama una viwanja 10 uuze viwili ujenge kimoja, hapo sawa.
Ila utakopeje pesa kwa dhamana ya viwanja wakati siyo biashara?
 
My congratulations
 
Tunarudi kule kule kumbe kujenga nyumba ni dili maana unaenda kukopea,Kwa nini usiende kukopea alteza yako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…