Peculiar
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 821
- 689
Naungana nawewe kua aachane na mambo ya dini kama tu anaona hayamfai na hayampendeziNO! achana na mambo ya dini, ni upuuzi mtupu na inventions za watu.
lakini siafikiani na wewe kuwa dini ni upuuzi.na sijui kama kuna mtu anaishi bila kuamini chochote,kwa sababu hata kuamini sayansi bado nayo ni amani ambayo wengine inawasaidia na kuwafaa lakini wengine wengine wasione hayo kama ilivyo katika dini.
Hapa kikubwa ni kuziishi hizo dini,kuacha kuzishiana uongo bali kuishi kwa upendo na haki.
Tukirudi kwa mtoa mada,japo tunamshauri aachane na udini lakini hawezi fanya ivo kirahisi maana ana chembe chembe za (UNAFIKI) ndani yake yaani,anajua anachokifanya,anaonesha ni mtu anayependa taharuki na mafarakano zaidi.
HALI HIYO INAWEZA KUSABABISHWA ZAIDI NA UJINGA(hata kama kasoma,maana sio wote waliosoma wameelimika) NA UTOTO(kutokuyajua maisha hasa katika maarifa na uhalisia wake).
Utamjuaje? kwenye heading kasema anaomba wanasayansi wamsaidie,lakini angalia wanasayansi aliowavuta(tag) Ili wasikose kumpa huo msaada anaohitaji.
Kuhoji,kudadisi ni sawa ikiwa lengo ni kujifunza ila si sawa kama lengo ni kukera au kudharaulisha.
Huyu akivaa rozari yule akivaa hijabu inaathiri vipi maisha ya mtu asiyeamini hadi ahamasishe wengine wavichukie ivo vitu kama achukiavyo yeye?
naungana nawewe kua aachane na hayo mambo kama hayana mana kwake,na naamini AKIKUA KISHA KUYAJUA MAISHA NA KUELIMIKA KISHA AKASTAARABIKA ATAACHA MWENYEWE.
Maana hakuna mtu ajuae yote na mkamilifu kwa kila kitu.