Wanasayansi naomba mnisaidie maana Quran inaniambia mtoto anaumbwa baada ya sperm kuingia kwenye damu iliyoganda

Wanasayansi naomba mnisaidie maana Quran inaniambia mtoto anaumbwa baada ya sperm kuingia kwenye damu iliyoganda

NO! achana na mambo ya dini, ni upuuzi mtupu na inventions za watu.
Naungana nawewe kua aachane na mambo ya dini kama tu anaona hayamfai na hayampendezi

lakini siafikiani na wewe kuwa dini ni upuuzi.na sijui kama kuna mtu anaishi bila kuamini chochote,kwa sababu hata kuamini sayansi bado nayo ni amani ambayo wengine inawasaidia na kuwafaa lakini wengine wengine wasione hayo kama ilivyo katika dini.

Hapa kikubwa ni kuziishi hizo dini,kuacha kuzishiana uongo bali kuishi kwa upendo na haki.

Tukirudi kwa mtoa mada,japo tunamshauri aachane na udini lakini hawezi fanya ivo kirahisi maana ana chembe chembe za (UNAFIKI) ndani yake yaani,anajua anachokifanya,anaonesha ni mtu anayependa taharuki na mafarakano zaidi.

HALI HIYO INAWEZA KUSABABISHWA ZAIDI NA UJINGA(hata kama kasoma,maana sio wote waliosoma wameelimika) NA UTOTO(kutokuyajua maisha hasa katika maarifa na uhalisia wake).

Utamjuaje? kwenye heading kasema anaomba wanasayansi wamsaidie,lakini angalia wanasayansi aliowavuta(tag) Ili wasikose kumpa huo msaada anaohitaji.

Kuhoji,kudadisi ni sawa ikiwa lengo ni kujifunza ila si sawa kama lengo ni kukera au kudharaulisha.
Huyu akivaa rozari yule akivaa hijabu inaathiri vipi maisha ya mtu asiyeamini hadi ahamasishe wengine wavichukie ivo vitu kama achukiavyo yeye?

naungana nawewe kua aachane na hayo mambo kama hayana mana kwake,na naamini AKIKUA KISHA KUYAJUA MAISHA NA KUELIMIKA KISHA AKASTAARABIKA ATAACHA MWENYEWE.

Maana hakuna mtu ajuae yote na mkamilifu kwa kila kitu.
 
Katika soma yangu nimekutana na hii aya. Naona inapishana na baiolojia niliyosoma miaka ile ya sekondari.

Quran 23:14

Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyoganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu mbora wa waumbaji

English translation:

Then We made the sperm drop into a clinging clot, and We made the clot into a lump [of flesh], and We made [from] the lump, bones, and We covered the bones with flesh; then We developed him into another creation. So blessed is Allah, the best of creators.

Ukisoma tafsiri ya kiingereza na kiswahili unaelewa kwamba sperm inaingia kwenye damu iliyoganda. Nikatafuta wataalamu wa tafsiri kuhusu hiyo clot.

Prof Haanein Muhammad Makhloof, on page 508 of his Dictionary of the meanings of words of the Quran says that the Arabic word alaq translated into English as "clot" means frozen blood.

Maswali yangu

1. Sperm inaingia kwenye damu iliyoganda?
2. Damu iliyoganda inaishi ndani ya tumbo la mwanamke?
3. Quran haifahamu kuhusu yai la mwanamke?
4. Sperm peke yake inaweza kuumbwa ikawa mtu?
5. Kauli kwamba tukamfanya kiumbe mwingine inamaanisha nini?

battawi FaizaFoxy Mokiti adriz Kisai
 
Hivi watu wa dini huwa mnabishana nini hawa waislam kitabu chao kimeeleza process za upatikanaji wa mtoto kwa imani yao nyie wengine hamkubali na nilivofuatilia izo hatua zinakaribia kufanana na zile wanazoamini wanasayansi tofauti ni ndogo sana kwanini mmoja amuone mjinga mwenzie uyu anasema sperm inaenda kukutana na yai la mwanamke ili apatikane mtoto mwingine anasema sperm inaenda kweny pande la damu iliyoganda ili apatikane mtoto na ukiangalia mwili wa binadam umezungukwa na damu sioni kitu kikubwa chakubishana mambo ya imani yamekaa kimtego yani unatakiwa uamini kitu hata kama haki make sense

Kwa imani yaki sayansi unatakiwa uamini kitu kinacho make sense kweny akili ya kawaida ndo maana wanasayansi wengi walikuwa wanafungwa walijaribu kugundua vitu mbali mbali na kuviweka public watu waliwaona ni waongo

Akili ya binadamu haiwezi kukubali kitu kirahisi ndo mitihani ya imani ilipojificha apo.. ukitaka amini, usipotaka tafuta jambo linaloridhisha ubongo wako

Acheni kelele kila mtu ashike lake
 
😂 😂 😂

Usikaze kichwa, majibu yako kichwani futa, muhemko wa kidini uweke kando ndio tujadili hili.

Kwa mujibu wa tafsiri yako, si niliyoleta mimi,hakuna sehemu shahawa imeingia kwenye pamde la damu kama ipo nioneshe nijipige ban JF, umeiandika wewe mwenyewe umesema hivi
"Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine.
Na kingereza chake uliweka kinachosema" Then We made the sperm drop into a clinging clot, and We made the clot into a lump"

Mbona hii lugha inazungumzia stage moja kwenda inayofata, kwamba aliumba/badili tone la shahawa kwenda kuwa pande la damu na sio kuingia kwenye pande la damu

Sasa hapo sijui tatizo ni lugha kwako, maana hakuna sehemu pameandikwa shahawa imeingia kwenye pande la damu bali shahawa imebadilika na kuwa pande la damu katika tumbo la uzazi la mwanamke.

Usikaze kichwa mzee, lugha nyepesi saana hiyo.
🥰💕💕💕💕
 
Hebu

Hiyo kwa mujibu wa sayansi gani?
Hebu niambie baada ya sperm kukutana na yai kipi kinatokea!? Kiumbe haswa kinaanza baada ya muda gani!? Je muda kabla hakijakuwa kiumbe kinakuwa ni kinini hapo?
Je vipi mimba ya miezi 6 ikitolewa inakuwa ni pande la damu au kiumbe?
Mheshimiwa makaveli10 usipoteze mda kumjibu Mpumbavu anaejifanya ni much know while ni empty head kichwa maji typically anaeongozwa na mihemko ya kitoto iliyojawa na chuki juu ya Uislam…….barikiwa kwa hints zako📌📌📌📌📌
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23]

Usikaze kichwa, majibu yako kichwani futa, muhemko wa kidini uweke kando ndio tujadili hili.

Kwa mujibu wa tafsiri yako, si niliyoleta mimi,hakuna sehemu shahawa imeingia kwenye pamde la damu kama ipo nioneshe nijipige ban JF, umeiandika wewe mwenyewe umesema hivi
"Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine.
Na kingereza chake uliweka kinachosema" Then We made the sperm drop into a clinging clot, and We made the clot into a lump"

Mbona hii lugha inazungumzia stage moja kwenda inayofata, kwamba aliumba/badili tone la shahawa kwenda kuwa pande la damu na sio kuingia kwenye pande la damu

Sasa hapo sijui tatizo ni lugha kwako, maana hakuna sehemu pameandikwa shahawa imeingia kwenye pande la damu bali shahawa imebadilika na kuwa pande la damu katika tumbo la uzazi la mwanamke.

Usikaze kichwa mzee, lugha nyepesi saana hiyo.
Amekuja kwa mlengo wa kidini sio kuelewa .
 
Nimesoma comments zote, nimejaribu kupitia maswali ya msingi ya mleta mada.

Nilichogundua ni kwamba mleta mada hakujiandaa kupata majibu sahihi. Alikuja na majibu yake tayari kichwani hivyo hata kama waislam walioisoma ....
📌📌📌📌📌
 
We ndugu yangu unajitoa akili tu, mbona hicho kitu kiko wazi.

Taja hatua zako za kibaiolojia uzijuazo, je baada ya manii kukutana na yai la mwanamke haliwi pande la damu?
Hapo ni mola kakuonesha uwezo wake katika hali ua shortcut maana ilibidi aamze kueleza ukila msosi, machungwa yanakhwaje kuwaje shahawa, bado alichambue yai la mwanamke, linavyotoka katika mirija ya falopia na kadhalika.

Hapo kakuonesha uwezo wako toka shahawa mpaka kuwa kiumbe kwa shortcuts.
Soma quraan yoote utapata maelezo zaidi humo humo.

Swali ushawahi toa mimba kabla miezi mi4 linalotoka pale sio bonge la damu?
📌📌📌
 
Embryology ya Allah na Muhammad huwa inachekesha Sana
Damu inaganda (dead blood) alafu ipo ndani ya mwanamke
Damu iliyoganda inabadilika kuwa pande la nyama ! , Pande la nyama linabadilika linakuwa mifupa tupu alafu mifupa inakuja tena kuvalishwa nyama dah!

Ila sio makosa yake Muhammad, hakuwa na technology iliyokuwepo kipindi icho aweze kujua ukweli wa embriology kwa kuangalia stages
Hii ndo kilaza kumuigilizia majibu kilaza....haya maelezo ya reproduction Muhammad aliyaiga sehemu...Mbaya zaidi aliyemkopi ni kilaza.
 
Quran 22:5

Enyi watu! Ikiwa nyinyi mna shaka ya kufufuliwa basi kwa hakika Sisi tulikuumbeni kutokana na udongo, kisha kutokana na manii, kisha kutokana na kipande cha damu ilio gandana, kisha kutokana na kipande cha nyama chenye umbo na kisicho kuwa na umbo, ili tukubainishieni. Nasi tunakiweka katika matumbo ya uzazi tunacho kitaka mpaka muda ulio wekwa. Kisha tunakutoeni kwa hali ya mtoto mchanga, kisha mfikie kutimia akili. Na wapo katika nyinyi wanao kufa, na wapo katika nyinyi wanao rudishwa kwenye umri wa unyonge kabisa, hata mtu awe hajui kitu baada ya kuwa anakijua. Na unaiona ardhi imetulia kimya, lakini tunapo yateremsha maji juu yake husisimka na kututumka, na kumea kila namna ya mimea mizuri
📌📌📌📌📌📌
 
Za kuambiwa changanya na za kwako...

Kweli mkuu. Waumini wanajiolea tu vitoto vidogoo.. kwa kisingizio cha quran na dini inaruhusu
 

Attachments

  • ASIA_-_covid_e_spose_bambine.jpg
    ASIA_-_covid_e_spose_bambine.jpg
    20.5 KB · Views: 9
  • Screenshot_20221001-100627_Firefox.jpg
    Screenshot_20221001-100627_Firefox.jpg
    89.2 KB · Views: 6
  • Screenshot_20221001-100343_Firefox.jpg
    Screenshot_20221001-100343_Firefox.jpg
    116.7 KB · Views: 7
Back
Top Bottom