Kwa maana itatubidi tuanze kufafanua maana ya mwanaadamu,
Je, sharti awe na roho au hata asipokuwa na roho.
Kama Kiumbe huyo si mwanaadamu mpaka awe na roho basi kwa mujibu wa hadithi hapa chini itatulazimu kufuatilia muda wa ukuaji wa huyu kiumbe, ila kama kiumbe hiki hata kisipokuwa na roho kinaitwa mwanaadamu basi tutasema ni mwanaadamu.
Imepokewa kutoka kwa Sayyiduna Abd Allah bin Mas’ud kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amesema:
“Kila mmoja wenu ameumbwa tumboni mwa mama yake siku arubaini, kisha akafanywa pande la damu kwa muda kama huo, kisha kipande kimoja cha nyama kwa muda kama huo.
Kisha Mwenyezi Mungu huntuma Malaika anayeamrishwa kuandika mambo manne.
Ameamrishwa aandike amali zake, riziki yake, na siku ya kufa kwake, na iwapo atabarikiwa au atakosa baraka (katika dini).
Kisha roho hupuliziwa ndani yake…”
(al-Bukhari no: 3036)
Kimsingi swali ulilouliza ni pana sana,