Wanasayansi naomba mnisaidie maana Quran inaniambia mtoto anaumbwa baada ya sperm kuingia kwenye damu iliyoganda

Maswali yangu

1. Sperm inaingia kwenye damu iliyoganda?
2. Damu iliyoganda inaishi ndani ya tumbo la mwanamke?
3. Quran haifahamu kuhusu yai la mwanamke?
4. Sperm peke yake inaweza kuumbwa ikawa mtu?
5. Kauli kwamba tukamfanya kiumbe mwingine inamaanisha nini?

NITAJIBU KWA JINSI NILIVYOISOMA SAYANSI KWA ELIMU YANGU NDOGO HII

1. Ndio, Sperm inaingia kwenye damu iliyoganda
2. Ndio Damu iliyoganda inaishi ndani ya tumbo la Mwanamke. Damu hiyo iliyoganda ndio inaitwa(Female Gamete/Egg Cell/Ovum). Ukitaka kuamini hilo ni hivi.

Hiyo Damu iliyoganda au Yai la kike kuna kipinfi hutoka katika Ovary kwa ajili ya urutubishaji(Fertilization) na husogea na kukaa katika Falopian Tube kwa ajili ya kusubiri hiyo fertilzation ndani ya siku takribani 3. Sasa ikikosa Sperm ya kiume hujivunjavunja(Disintegrate) na kutoka kama Bleed.

Kumbuka hilo yai limezungukwa na damu(kwakuwa damu ni Cell na zimegawanyika yani White blood cell, red blood cell,. plasma membrane na platelete), Na ndio mana hutoka kama Damu(bleed) hapo tunasema Mwanamke anakuwa kwenye Hedhi.

3)Quran inafahami kuhusu yai la Mwanamke ndio hilo pande la damu iliyoganda au Egg Cell/Ovum.

4)Hapana

5) Inamaanisha inamaanisha baada ya pande la damu/Egg cell kufanikiwa kupata Sperm(Mbegu za Kiume) basi hapo mimba ndipo inapoanzia kutungwa na process zote tumboni kwa Mama ila vyote hivyo hufanyika kwa Idhini ya MWENYEZI MUNGU au kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu. Na kuna Miezi ikifika Mtoto akiwa tumbo basi mtoto atapewa pumzi kwa uwezo wa Mungu.
 
Wote mnaruka stage ya mifupa tupu kwa Nini?

Damu kuganda ni damu mfu clot
Ki clot tu kichembe kikiingia kwenye moyo au kwenye ubongo mziki wake sio wa kitoto

Sasa hii clot kwenye mji wa uzazi kwa siku 40 inakuwaje, mwanamke si angeoza kizazi
 
Una force sana kuifanya kuran iwe relevant kwenye mambo ya kisayansi ila ni uongo mtupu
Wanasayansi wako wanasema sperm zinarushwa kutoka katika Seminal vesicle na sio korodani
Korodani ikisha tengeneza sperm cell inazipeleka katika Seminal vesicle kwa ajili ya kuwekewa virutubisho vingine muhimu na kurushwa kuenda ukeni kutungisha mimba

FACTION OF SEMINAL VESICLE
The main function of the seminal vesicles is to produce a fluid that is high in fructose, a sugar that provides nutrients for sperm cells, as well as other proteins, enzymes, and mucus. This fluid is a major component of semen, and it accounts for about 50%–80% of semen volume.2

Muscles in your seminal vesicles contract to move seminal fluid and sperm into your urethra and the out through your penis.

JE NA QURAN INASEMAJE?

Quran 86:6
Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa,
7.
Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu.

JE SEMINAL VESICLE IPO WAPI
michoro ya wanasayansi wako inaonyesha hapo chini ilipo hiyo SEMINAL VESICLE ukienda ju unakutana mfupa wa mbavu na ukienda pembeni unakutana na uti wa mgongo

Na kama unabisha sema hapo katika Seminal vesicle ukienda ju unakutana na mfupa gani na ukienda pembeni unakutana na mfupa gani


Nitajie uongo uliyopo hapa iwe ni uongo kutoka kwangu au kwa hao wanasayansi wenu au katika Quran
 
Hiyo accuracy umeipima vipi ? wakati wametoa maboko mengi ya wazi hapo automatically ishakosa sifa ya kuaminika.
 
Nyie mlikuwa mnajazana madrasa kusoma quran na mwalimu akaamua kuwatoa huko na kuwapa elimu. Mkapa akawapa chuo ambacho ni mali ya uma kwasababu hamna uwezo wa kujenga chochote.
Si aliua East African Muslim Welfare Association na kutaifisha plot zake?
 
Hiyo accuracy umeipima vipi ? wakati wametoa maboko mengi ya wazi hapo automatically ishakosa sifa ya kuaminika.
Accuracy unaipima kwa usahihi wa ujumbe uliotolewa. Huwa sihoji sana maeneo ya quran ambayo Muhammad anaongea ila nitahoji pale inapoonekana Allah ndio anaongea directly.

Hata hii mada imekuja kwa msingi kwamba hicho kinachosemwa hapo ni directly kutoka kwa Allah na hakipo sahihi kisayansi.
 
Si aliua East African Muslim Welfare Association na kutaifisha plot zake?
Mwalimu alisaidia sana waislam kuwa na wasomi wengi kwenye elimu ya darasani. Sijui ni kwanini hamjapenda ku-appreciate hili.

Mwalimu alimwachia uraisi Mwinyi ambaye ni muislamu. Mkapa mwenyewe ameandika kwenye kitabu chake kwamba mwalimu alikuwa anamtaka Dr Salim ndio awe rais 1995 lakini Salim akawa analegalega. Mwalimu hakuwahi kuwachukia wala kuwaonea waislam.

Association ya waislam ilivunjwa na bakwata ikaundwa. Wakristo ndio walipoteza mali nyingi kutokana na maamuzi ya Nyerere kipindi kile.
 
Ndio Damu iliyoganda inaishi ndani ya tumbo la Mwanamke. Damu hiyo iliyoganda ndio inaitwa(Female Gamete/Egg Cell/Ovum)
Damu iliyoganda inawezaje kuishi? Damu iliyoganda ndio iitwe yai?😂
 
1. Mwalimu alisaidia waislamu na yeye pia alisaidiwa na waislamu wakati alipokuwa anagombea uhuru. Lakini kwa nini alishindwa kuwaamini na kuona kama ni wapingaji baada ya uhuru?

2. Hao waliompinga Salim ni akina nani kama siyo akina Mongela na wenzake? (hii niliisoma zamani kwenye gazeti kama sikosei ilikuwa RAia mwema)

3. Bakwata iliundwa kwa mantiki ya kutumikia serikali siyo waislamu. Hakukuwa na sababu ya kuvunja EAMW.

Hebu jaribu kutafuta kitabu 'Nyerere na kanisa katoliki Tanzania' na 'The Partnership' vitakuongezea maarifa kuhusu siasa za Tanzania.
 
1. Mwalimu alisaidia waislamu na yeye pia alisaidiwa na waislamu wakati alipokuwa anagombea uhuru. Lakini kwa nini alishindwa kuwaamini na kuona kama ni wapingaji baada ya uhuru
Unaweza kueleza ni kwa vipi hakuwaamini? Maana hata Zanzibar kawasaidia waislam kwa kupindua utawala wa sultani.

2. Hao waliompinga Salim ni akina nani kama siyo akina Mongela na wenzake? (hii niliisoma zamani kwenye gazeti kama sikosei ilikuwa RAia mwema
Salim mwenyewe tu alishindwa kucheza na siasa. Ilikuwa rahisi kwake kushinda akiwa na support ya mwalimu akazembea.
3. Bakwata iliundwa kwa mantiki ya kutumikia serikali siyo waislamu. Hakukuwa na sababu ya kuvunja EAMW
Hili sitaki kulizungumzia sana kwasababu sijawahi kulisoma na kulifuatilia kiundani. Ninachofurahia tu ni kwamba mwalimu aliweza kudhibiti nchi isiwe na vikundi vyenye siasa kali za kidini.
Hebu jaribu kutafuta kitabu 'Nyerere na kanisa katoliki Tanzania' na 'The Partnership' vitakuongezea maarifa kuhusu siasa za Tanzania.
Nimesoma vingi tu mpaka kwaheri ukoloni kwaheri uhuru na nikagundua vingi ni propaganda tupu zenye lengo la kuleta uchafuzi wa amani.
 
Kama hata majina ya mitume huwajui basi hauna haki ya kuhoji.

Wapi nimesema hawakuandika kwa inspiration ya Roho Mtakatifu?
Kama wame andika kwa kuongozwa na roho mtakatifu kwanini wakosee kila wakati hao kama sio wameshiba maboga ndio wanajiandikia tu
 
Hiyo ni lugha ya cheo mkuu kasome bibilia ya kiyunani uone Muhammad katajwa vipi mule someni wakristo msi kariri
1. Hakuna mahali popote katika Biblia ambapo Mohamad ametajwa.

2. Lugha ya Cheo ndio inakuwa wingi? Kwamba cheo cha Mungu ndio kinatumia Wingi? Hebu acheni ujuha nyie watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…