Nimesoma hii mada yote na nakupongeza ndugu
Championship kwa kuileta na kuhoji na muhimu zaidi kujibu hoja mbalimbali.
Umenifanya niamue kuanza kuwa makini kusoma biblia yangu maana umeyajibu maswali ya
medisonmuta na
professional Driver kwa weledi mkubwa.
Kuna maswali yalipoulizwa nikawa naanza kuingiwa na wasiwasi juu ya imani yangu ya kikristo lakini ulipotolea ufafanuzi nimefurahi sana. Nimeona kumbe maswali ya waislamu ni mepesi sana mtu akiwa msomaji wa biblia.
Swali kama jina la mzazi wa yusuphu kuwa tofauti kwenye mathayo na luka liliniogopesha sana. Ulipojibu kwamba luka anaongelea ukoo wa mariamu na mathayo anaongelea ukoo wa yusuphu nikaamua kwenda kusoma na kuona ni kweli. Dah, nimefurahi sana.
Lile swali la mpangilio wa majaribu ya Yesu umelijibu kisomi sana. Luka hakutaja mpangilio lakini mathayo alitaja hivyo hakuna mkanganyiko. Pia nani alikuwa wa kwanza kumuona Yesu baada ya kufufuka umemaliza ubishi.
Uliua kabisa kuonesha Yesu akiitwa Mungu, kwamba yeye ndio kaumba ulimwengu wote, alikuwepo tangu milele, ni Mwana wa Mungu sio kwasababu alizaliwa bali ni Mwana wa Mungu tangu milele na kwamba atarudi kuhukumu ulimwengu.
Nimesikitika kwamba waislamu wameshindwa kujenga hoja vizuri katika kutetea imani yao. Mambo mengi ya msingi waliyohojiwa wameishia kuchomeka hoja nyingine au kuweka lugha ya kukera.
Chige ameshindwa kuonesha kwamba Issa aliwahi kuwa raia aliyeishi Israel. Hakuna ushahidi wowote uliotolewa. Hata wakristo ambao ni waarabu wanamuita Yesu Kristo Yasu.
Huyu
Wazolee ameshindwa kuonesha uthibitisho wa sperm kutokea eneo lililopo kati ya mbavu na uti wa mgongo. Amekuja na picha ambayo wameikuza na kuweka seminal vesticle ionekane ipo juu kuhalalisha madai ya Quran lakini picha zote zinazopatikana google hazipo hivyo.
Hoja nyingine ambazo waislamu hawajaweza kuzitolea ufafanuzi ni:
1. Baadhi ya manuscripts zilozopo birmingham england zinaonesha kuwa ziliandikwa 568-645 AD. Hii inaonesha Quran ilianza kuandikwa kabla ya kipindi cha Muhammad.
2. Kama malaika hawana freewill wasingeweza kufanya argument na Allah.
3. Muhammad alikuwa hajui kusoma lakini jibril alikuwa anamlazimisha asome. Ilitegemewa malaika awe anajua kwamba asingeweza kusoma au malaika angempa uwezo wa kusoma kimiujiza.
4. Mtiririko wa sperm kuwa damu iliyoganda halafu kuwa nyama kisha iwe mifupa na baadae ndio kiumbe mwingine atokee hauko sahihi.
5. Suala kwamba kiumbe kinachokuwa tumboni kinapewa pumzi baada ya miezi minne ni madai ya hatari sana.
Nawakopi wanazuoni wa kiislamu hapa pengine wataungana kuleta ufafanuzi usioacha mashaka.
FaizaFoxy Kisai JumaKilumbi inamankusweke Mohammed Said