Habarini wanaJF,
Nimeandaa Uzi huu ili na Mimi nilete Challenge na Maswali kuhusiana na Biblia kama mwenzetu Champion alivyofanya katika uzi wake uliokwenda kwa jina la
(“Wanasayansi naomba mnisaidie maana Quran inaniambia mtoto anaumbwa baada ya sperm kuingia kwenye damu iliyoganda")
Katika uzi wake huo ameuchallenge Uislamu huku akisaidiwa na mwenzie anayekwenda kwa jina la Mokiti na wengineo.
Lakini imekuwa heri kwani wamepewa majibu mengi ya kuridhisha japo wamekuwa wabishi tu na kutokutaka kukubali huku wakijitahidi kupambana kuwakaribisha watu(Waislamu) kwa Yesu na kuwashawishi Waokoke.
Mimi nasema hapana, bado hamjatushawishi kutufanya sisi waisilamu tuje kwa Yesu tuokoke na hamtaweza kamwe kwa njia yoyote ile.
Sasa kama kweli mnatuhitaji tuje kwenye Dini yenu, tunaomba mtujibu maswali kwanza tutakayoweka hapa kwa mujibu wa Aya(Maandiko) ndani ya Bibilia ambayo nitaweka hapa na kuulizia Maswali, kwa maana Aya hizo zinanichanganya na pia zinajichanganya.
TUANZE
KWANZA kabisa ukisoma MARKO 15:25 alafu ukaja ukasoma YOHANA 19:14 ni vitu viwili tofauti na vinachanganya. Acha nianze kunukuu hizo aya.
MARKO 15:25 inasema,
Marko 15:25-27 (Basi ilikuwa saa tatu, nao wakamsulibisha.
Palikuwa na anwani ya mashitaka yake iliyoandikwa juu, MFALME WA WAYAHUDI.
Na pamoja naye walisulibisha wanyang'anyi wawili, mmoja mkono wake wa kuume na mmoja mkono wake wa kushoto.)
YOHANA 19:14 inasema,
Yohana 19:14-15 (Nayo ilikuwa Maandalio ya pasaka, yapata saa sita. Akawaambia Wayahudi, Tazama, Mfalme wenu!
Basi wale wakapiga kelele, Mwondoshe! Mwondoshe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Je! Nimsulibishe mfalme wenu! Wakuu wa makuhani wakamjibu, Sisi hatuna mfalme ila Kaisari.)
Kwamujibu wa hizo Aya hapo juu inaonesha Mkanganyiko kwani MARKO 15:25 anasema saa 3 tayari Yesu kashatundikwa msalabani wakati ukisoma YOHANA 19:14 anasema saa 6 yesu ndio kwanza yupo kwa Pilato yani hata Msalabani bado hajafikishwa.
Sasa mbona Yesu wanaonekana wapo tofauti tofauti yani Yesu anayemzungumzia Marko na Yohana ni vitu viwili tofauti. Ndio Mana sisi waisilamu hatuamini kama Yesu alikufa Msalabani.
SWALI
1) NI YESU GANI SAHIHI ALIYEKUFA MSALABANI?
JE NI HUYU ANAYEMZUNGUMZIA MARKO AMBAYE SAA 3 TAYARI YUKO MSALABANI?
AU NI YULE ANAYEMZUNGUMZIA YOHANA AMBAYE SAA 6 BADO WANAMTEMBEZA BARABARANI NA MUDA HUO YUKO KWA PILATO SAFARI YA MSALABANI BADO?
PILI, Ukisoma 2MAMBO YA NYAKATI 22:2 na ukaja ukasoma 2WAFALME 8:26 ni vitu viwili tofauti,. sasa sijui kumeharibiwa au ni vipi na sijui Wakristo wanakwama wapi. Maana naona ubabaishaji kama ni mwingi na najiuliza huwaga hizi Aya hamsomi Makanisani na kuzilinganisha? Nanukuu hizo Aya
2MAMBO YA NYAKATI 22:2
2 Mambo ya Nyakati 22:2 (Ahazia alikuwa na umri wa miaka arobaini na miwili alipoanza kutawala; akatawala mwaka mmoja huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Athalia binti Omri.)
2WAFALME 8:26
2 Wafalme 8:26 (Ahazia alikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili alipoanza kutawala; akatawala mwaka mmoja huko Yerusalemu. Na jina la mamaye aliitwa Athalia binti Omri mfalme wa Israeli.)
Hizo Aya hapo juu, ukisoma utakutana na miaka toafuti ya Ahazia huku ikiongelea kitu kile kile, Aya moja inasema Ahazia ana miaka 42 na Nyingine jnasema Ahazia ana miaka 22.
SWALI:
2)(A) ILI BIBLIA IWE NI UKWELI, AYA IPI IKO SAHIHI KATI YA 2MAMBO YA NYAKATI 22:2 NA 2WAFALME 8:26?
(B) MIAKA SAHIHI YA AHAZIA NI MINGAPI?
Kwa ufupi ni kwamba kuna Maboko Mengi ndani ya Biblia ila nimeanza na hayo kwanza. Hivyo vingine nitauliza kwenye thread itayofuatia, kama mtahitaji niulize.
Haya sasa ninaomba Majibu ndugu zetu Wakristo.
Nawasilisha.