Wanasayansi naomba mnisaidie maana Quran inaniambia mtoto anaumbwa baada ya sperm kuingia kwenye damu iliyoganda

Daah sijaona kilaza mkubwa wa kiwango cha lami kama wewe.
Hata vitu vidogo tu kuhusu principles za lugha hujui.
Hujui hata maana ya “QUOTATIONS’
Tukienda kama akili yako inavyokutuma tutajaza tu servers za Jamii forums bure.
Mfano, mungu wako wa kwenye biblia (yesu) alichukuliwa na shetan na kupelekwa mlimani kujabiriwa. Eti mungu anajaribiwa na shetani daah hili likitabu lenu miyeyusho sana😀😀.
Walipofika mlimani,”shetani kamwambia Yesu ikiwa yeye ni mwana wa mungu ajitupe chini au abidili mawe kuwa mkate”
kwahiyo unatwambia biblia na yenyewe ni maneno ya shetani coz shetani hapo anazungumza kwenye biblia.
Una logic za kitoto sana…
Tukisema tufate logic zako humu , si tutajaza servers bure tu kwa upuuzi wako….
 
Daah sijaona kilaza mkubwa wa kiwango cha lami kama wewe.
Hata vitu vidogo tu kuhusu principles za lugha hujui.
Hujui hata maana ya “QUOTATIONS’
Maneno ni ya hao viumbe yeye kaya quote kayaweka kwenye koran kama yalivyo,
  • Kikubwa ungesema Allah alitakiwa aache Plagiarism maana katoa maneno ya viumbe na hapo hapo kadai viumbe viweke kama yake 🤣 yani maneno ya viumbe ameyachukua na kufanya yake
  • Alitakiwa kuweka Reference kuwa taja Kina shetani , siafu ndege huhud n.k
  • Hakutakiwa kujitapa na challenge wakati kanukuu maneno ya wengine
 
we jamaa kama akili yako ndo iko hivyo, You have a very long way to go….
Sasa ww tengeneza Quran yako iliyo bora kuliko ya Allah, alaf uweke reference zako kama unavyotaka ww kama utaweza, ita na mashetani na viumbe vyote wakusaidie.
Ukiweza kutengeneza hiyo Quran yako kisha ni tag, nipo hapa nakusubiri 🤔
And for now, siwez tena endelea kujadiliana na mpumbavu ni kupoteza muda bure, nitakuacha nao huo upumbavu wako…
 
Usikimbie nondo zangu , challenge aliyotoa allah ni ya nini?
 
alichotakiwa kusoma ni aya ya kwanza kabisa kuteremshwa ktk surat Al'alaq ambayo inapatikana ktk kitabu cha Qur-an.
Kwahiyo sasa hivi itabidi mbadilishe maana mlisema quran haikuwa imeandikwa isipokuwa muhammad alikariri tu.
 
Sasa kama majini, wadudu, watu, shetani nk walihusika kutengeneza aya (kwa kunukuliwa) ni kipi kinakuwa challenge kwa yeyote?
 
Isaac Newton ameandika vitabu bora na vyenye manufaa kwa ulimwengu kuliko hicho kitabu cha umwagaji damu na machafuko.
 
Habarini wanaJF,

Nimeandaa Uzi huu ili na Mimi nilete Challenge na Maswali kuhusiana na Biblia kama mwenzetu Champion alivyofanya katika uzi wake uliokwenda kwa jina la
(“Wanasayansi naomba mnisaidie maana Quran inaniambia mtoto anaumbwa baada ya sperm kuingia kwenye damu iliyoganda")

Katika uzi wake huo ameuchallenge Uislamu huku akisaidiwa na mwenzie anayekwenda kwa jina la Mokiti na wengineo.

Lakini imekuwa heri kwani wamepewa majibu mengi ya kuridhisha japo wamekuwa wabishi tu na kutokutaka kukubali huku wakijitahidi kupambana kuwakaribisha watu(Waislamu) kwa Yesu na kuwashawishi Waokoke.

Mimi nasema hapana, bado hamjatushawishi kutufanya sisi waisilamu tuje kwa Yesu tuokoke na hamtaweza kamwe kwa njia yoyote ile.

Sasa kama kweli mnatuhitaji tuje kwenye Dini yenu, tunaomba mtujibu maswali kwanza tutakayoweka hapa kwa mujibu wa Aya(Maandiko) ndani ya Bibilia ambayo nitaweka hapa na kuulizia Maswali, kwa maana Aya hizo zinanichanganya na pia zinajichanganya.

TUANZE
KWANZA kabisa ukisoma MARKO 15:25 alafu ukaja ukasoma YOHANA 19:14 ni vitu viwili tofauti na vinachanganya. Acha nianze kunukuu hizo aya.

MARKO 15:25 inasema,
Marko 15:25-27 (Basi ilikuwa saa tatu, nao wakamsulibisha.
Palikuwa na anwani ya mashitaka yake iliyoandikwa juu, MFALME WA WAYAHUDI.
Na pamoja naye walisulibisha wanyang'anyi wawili, mmoja mkono wake wa kuume na mmoja mkono wake wa kushoto.)

YOHANA 19:14 inasema,
Yohana 19:14-15 (Nayo ilikuwa Maandalio ya pasaka, yapata saa sita. Akawaambia Wayahudi, Tazama, Mfalme wenu!
Basi wale wakapiga kelele, Mwondoshe! Mwondoshe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Je! Nimsulibishe mfalme wenu! Wakuu wa makuhani wakamjibu, Sisi hatuna mfalme ila Kaisari.)

Kwamujibu wa hizo Aya hapo juu inaonesha Mkanganyiko kwani MARKO 15:25 anasema saa 3 tayari Yesu kashatundikwa msalabani wakati ukisoma YOHANA 19:14 anasema saa 6 yesu ndio kwanza yupo kwa Pilato yani hata Msalabani bado hajafikishwa.

Sasa mbona Yesu wanaonekana wapo tofauti tofauti yani Yesu anayemzungumzia Marko na Yohana ni vitu viwili tofauti. Ndio Mana sisi waisilamu hatuamini kama Yesu alikufa Msalabani.

SWALI
1) NI YESU GANI SAHIHI ALIYEKUFA MSALABANI?

JE NI HUYU ANAYEMZUNGUMZIA MARKO AMBAYE SAA 3 TAYARI YUKO MSALABANI?

AU NI YULE ANAYEMZUNGUMZIA YOHANA AMBAYE SAA 6 BADO WANAMTEMBEZA BARABARANI NA MUDA HUO YUKO KWA PILATO SAFARI YA MSALABANI BADO?

PILI, Ukisoma 2MAMBO YA NYAKATI 22:2 na ukaja ukasoma 2WAFALME 8:26 ni vitu viwili tofauti,. sasa sijui kumeharibiwa au ni vipi na sijui Wakristo wanakwama wapi. Maana naona ubabaishaji kama ni mwingi na najiuliza huwaga hizi Aya hamsomi Makanisani na kuzilinganisha? Nanukuu hizo Aya

2MAMBO YA NYAKATI 22:2
2 Mambo ya Nyakati 22:2 (Ahazia alikuwa na umri wa miaka arobaini na miwili alipoanza kutawala; akatawala mwaka mmoja huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Athalia binti Omri.)

2WAFALME 8:26
2 Wafalme 8:26 (Ahazia alikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili alipoanza kutawala; akatawala mwaka mmoja huko Yerusalemu. Na jina la mamaye aliitwa Athalia binti Omri mfalme wa Israeli.)

Hizo Aya hapo juu, ukisoma utakutana na miaka toafuti ya Ahazia huku ikiongelea kitu kile kile, Aya moja inasema Ahazia ana miaka 42 na Nyingine jnasema Ahazia ana miaka 22.

SWALI:
2)(A) ILI BIBLIA IWE NI UKWELI, AYA IPI IKO SAHIHI KATI YA 2MAMBO YA NYAKATI 22:2 NA 2WAFALME 8:26?

(B) MIAKA SAHIHI YA AHAZIA NI MINGAPI?

Kwa ufupi ni kwamba kuna Maboko Mengi ndani ya Biblia ila nimeanza na hayo kwanza. Hivyo vingine nitauliza kwenye thread itayofuatia, kama mtahitaji niulize.

Haya sasa ninaomba Majibu ndugu zetu Wakristo.
Nawasilisha.
 
Naona huu Uzi hawa Moderators wameamua kuufuta, sijui tatizo nini?
 
Alafu hoja mlizojibu hazikuwa na maana
 
Hapa tunachoangalia ni hii saa 3 aliyoitaja Marko na saa 6 aliyoitaja Yohana basi

Aya haijasema Saa 3 aliyoitaja Marko ilikuwa ni ya asubuhi au usiku. Na pia Aya haijasema saa 6 aliyoitaja Yohana ilikuwa ni ya Alfajiri(asubuhi), mchana au usiku.

Aya imesema ilikuwa saa 3 na ilikuwa saa 6 basi na imeishia hapo, haya mambo ya asubuhi sijui mchana sijui usiku mnayatoa wapi?. Kwa hiyo ukiangalia tofauti ya masaa kutoka saa 3 hadi saa 6 ni masaa 3.

Hivyo basi Marko aliripoti tukio la Yesu kuwa yupo Msalabani tayari saa 3, halafu masaa matatu mbele yani/hadi ilipotimia saa 6 akaja kidume Yohana akasema hapana saa 6 yesu ndio kwanza kapelekwa kwa Pilato.

Sasa nawaza kama saa 6, Yohana anatuambia Yesu alikuwa kwa Pilato. Je Msalabani alifikishwa saa ngapi?

Msituambie sijui habari za saa 3 au saa 6 asubuhi, sijui Mchana, sijui usiku. Kwakuwa aya haisemi hivyo.
 
Japokuwa huu uzi umefutwa kwa sababu binafsi, nimeona acha niupachike hapa.

Na ni kama nilijua tu huu uzi utafutwa ndio mana nikausave Mahali.
 
Kwa Nini kila Uzi wako unalalamika umefutwa ?
Dah! We jamaa ni Muongo sana. Nimewahi kulalamika wapi kila uzi wangu huwa unafutwa? Kitu usichokijua ni kwamba, mimi ndio kwa mara ya kwanza leo nalalamika uzi wangu unafutwa.

Sikawahi kulalamika popote uzi wangu unafutwa zaidi ya leo hapa siku hii ya ijumaa tarehe 07/10/2022.

Kama kuna mahali niliwahi kulalamika mbali na leo lete ushahidi hapa.
 
Malalamiko yako ni uongo kwasababu uzi upo jukwaa la dini.
 
Uzi upo na uchangiaji unaendelea , clik link itakupeleka

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…