Wanasayansi wa kiafrika ndio wanaoikuza Amerika na Ulaya, kwanini wasiikuze Afrika yao?

Nimekuelewa wataalamu kwenye uzi wako wapo from hizo nchi.

Lakini ninahitaji kujua exact number ya wataalamu mashuhuri kutoka kusini mwa jangwa la sahara.
ni wengi mno hao nimetaja wale waliotikisa dunia tu yaani kuna ambao bado wanasoma huko kwa wenzetu na hawana mategemeo ya kurudi na wengine ndio wanafanya kazi za kawaida kwenye mataifa yaliyoendelea ila bado hawajagundua vitu

hivi unafikiri kwanini sasa matangazo ya scholarship kwa waafrika yamekuja mengi?
 
ndo hvyo mkuu kikubwa tusiache kupambana kwakuwa hii hali tunayopitia hata wao walipitia pia enzi zao,tusione aibu kukazania elimu kilimo na viwanda vdg vdg huko kwngne tufnye taratibu
ndio hivyo ila inabidi ili tujitoe kwenye haya matatizo nchi nyingi za africa ziungane ili kuwa na nguvu kama walivyofanya USA kwahiyo kama tz inaonekana jimbo tu bila hivyo bado tutakuwa tunazingirwa na makamasi
 
Hahahahaa hahahahaa
Bora sijatajwa
Lakini kuna Uzi niliwahi ongea kitu kuwa Y? Wasomi wengi wa Africa hawatumikii Nchi zao!.

Kubwa zaidi mfumo mbovu Na sera mbovu za elimu pamoja Na kujuana sanaaa!.

Mf: Mimi nilisoma aerospace engineering
Unadhani kwa huko bongo ningefanyaje nini???????

Pia unakuta mtu una hustle kutoboa halafu uje kuganga Na mshahara wa TGS C?!!!!
.
Waafrika wanaojitambua wapo njeee!
Ukibaki Africa ni kupoteza Muda tu!.
Mleta maada wapo wa TANZANIA wengi NASA lakini wamebadili kila kitu Na hawataki hata kusikia jina TANZANIA!.
 
ndio hivyo ila inabidi ili tujitoe kwenye haya matatizo nchi nyingi za africa ziungane ili kuwa na nguvu kama walivyofanya USA kwahiyo kama tz inaonekana jimbo tu bila hivyo bado tutakuwa tunazingirwa na makamasi
ah ndo hvyo mkuu kama hatujitahidi tutaendelea kuwa watumwa tu sema tunabadilisha tu bwana sasa hivi bwana yetu mchina
 
Wangeuawa zamani tu,tena kama huyo mwenye celtel angeshapigwa risasi.
Hata mack aliyegundua facebook asingefika popote na fb yake wala whatsapp,angepigwa risasi na yeye.
Nata mimi nikiwa scientist sifanyi ujinga huo wa kukaa humu tena hususani Tanzania.
Huyo mrusho satellite angeambiwa aishushe haraka sana la sivyo atapigwa kipigo cha mbwa koko.
 
Mkuu kweli haki ya mungu wallah huu mwezi mtukufu wagunduzi wa instagram,facebook na whatsapp wangekua wanatokea Tanzania wangeshaambiwa wafunge mitandao means hata dunia isingenufaika navyo wala wasingekuwa hata billionares kama zuckerberg.
 
Mkuu kweli haki ya mungu wallah huu mwezi mtukufu wagunduzi wa instagram,facebook na whatsapp wangekua wanatokea Tanzania wangeshaambiwa wafunge mitandao means hata dunia isingenufaika navyo wala wasingekuwa hata billionares kama zuckerberg.
Upo sahihi kiongozi!.
Africa ni laana Na kupotezeana ndoto+bahati Na nyota!.

Kwanza wamekalia uchawi mwingi!.Na imani haba

Kuja siku nilienda kijijini Na Mzungu daaah
Aseeee walisema nitawaleta mikosi
Tena wakafika mbali zaidi Na kusema ety
Nimekuwa Freemason!..

Kisa niliosomaga nao primary wapo kijijini wamechoka me naonekana Bado kijana Na napesa
Nilichoka hoi
 

Sasa mbona huyu kabaki Afrika na bado hakuna maendeleo?
 
Jibu ni rahisi, hakuna haja ya kusema wana tamaa ya pesa ama c.yo wazalendo. Ni kwa sbb hakuna nchi za kiafrika zilizojikita seriously kwenye uendelezaji wa sayansi na teknolojia ama hata R&D.
 
Africa inateswa na siasa mbovu. Kutothamini ujuzi wa mtu siasa mbele. Ndio maana mpk sasa makonda asie na kitu kichwani ni mkuu wa mkoa na anatukana mainjiania na wenye akili, ukae Afrika ufanye nini?

Naonaga vijana wanatengeneza wanavumbua vitu kwenye magereji na mitaani huko nani anawapa sapoti? Zipo wapi karakana za taifa kukuza vipaji?

Mtu akitengeneza kitu badala apewe karakana na uwanja wa majaribio utasikia hairuhusiwi iko kitu maana hakijathibitishwa. Nyumbu nyumbu tu Africa haitaendelea. Kuna tatizo.

Sasa kwa akili za kiongozi wa malaika unategemea ipo siku Afrika itatoka
 
Nchi nyingi za kiafrika wanasiasa ndio tatizo letu. Wanasiasa ni zigo kubwa sana tunalolipia gharama zao za juu za maisha kuliko kundi lolote. Hivi kweli kwa mfano tu Profesa maji marefu analipwa zaidi kuliko daktari bingwa pale muhimbili!!! inaingia akilini mheshimiwa msukuma na mwenzie Sugu wanalipwa zaidi kuliko engineer fulani?
 
Sasa huko Bongo tunazibiwa na kuongozwa na Bashite.

Kwa nini tusisepe tu?
 
Jibu mbona Dogo sana ,angalia mshahara wa mbunge na wa Mwalimu,hapo ndio utapata jibu.

Nchi za afrika husani Tanzania haiungi mkono profession Bali inaunga mkono politics.
 
Mkuu kweli haki ya mungu wallah huu mwezi mtukufu wagunduzi wa instagram,facebook na whatsapp wangekua wanatokea Tanzania wangeshaambiwa wafunge mitandao means hata dunia isingenufaika navyo wala wasingekuwa hata billionares kama zuckerberg.
Wangeingia centrorali kwanza!
 
Africa hatuna kipaumbele cha kukuza taaluma au kua support wana-Sayansi kwenye gunduzi au tafiti zao...

Africa tunakazania zaidi, vibali au uhalali wa kufanya hicho ulichovumbua au unachotakakuvumbua, mengine utajijua mwenyewe...

Africa tunakazania zaidi, unataka kuvumbua au kufanya tafiti fulani wewe kama nani? Na je umepitia Msingi, secondary na chuo? Je vyeti vyote unavyo... mengine utajijua mwenyewe... na je hicho unachotaka kuvumbua au kukifanyia tafiti kuna chochote kitu watapata?

Ndiyo maana wana-Sayansi wengi kutoka Africa wanakimbilia Ulaya...


Cc: mahondaw
 
NAcho sikitika zaidi prof amekufa KIFO ambacho nahisi alikufa huku anajilaumu why alirudi home, is very sad.
 
kwani wangebaki kwenye nchi zao wakayafanya hayo waliyoenda kufanya kwenye mataifa makubwa si ipo siku kazi za mikono yao zingewalipa au tuseme wana tamaa ya pesa?
Africa hakuna masilahi halafu kitu kingine kuna sheria za ovyo sana Africa na hakuna support.
Mfano mzuri. Ni yule jamaa aliyetengeneza helcopter. Unamsikia kwa sasa?
Hata ningekuwa mimi siwezi kubaki Africa hata wangenipa nini. Mshahara wa mzoa taka USA unamzidi meneja wa bank. Hapana aiseeee
 
Africa inayolipa ni siasa tu. Mambo ya taaluma unajitafutia umasikini. Siku hizi tunaangalia masilahi
 
Nani aliyekuambia wanasayansi wa kiafrika ndo walioikuza ulaya na marekani?

Hao waafrika wamekwenda huko washakuta ulaya na marekani zimeendelea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…