PostGE2025 Wanasheria watinga ICC na kufungua kesi dhidi ya Rais Samia na wakuu wa Vyombo vya Usalama Tanzania

PostGE2025 Wanasheria watinga ICC na kufungua kesi dhidi ya Rais Samia na wakuu wa Vyombo vya Usalama Tanzania

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Tayari Samia Suluhu Hassan anaogopa hata kwenda Zambia, Angola, South Africa anamtuma kaimu rais Emmanuel John Nchimbi
Samia asiwe na hofu ajitayarishe kukabidhi mikoba ya urais kwa kaimu rais Emmanuel Nchimbi kwa kufuata hatua za kikatiba na kulihutubia bunge kuwa anakwenda Uholanzi na hafahamu mchakato utachukua muda gani huko Mahakama hivyo anakabidhi madaraka kwa Nchimbi kama Uhuru Kenyatta alivyofanya wazi

Kimoyo moyo Atatamani huu upepo uondoke na Samuya, Ili alithi mali za marehemu

Kukaimu urais iliwahi kutokea, Samia anajitayarisha kwenda kujitetea akiongozana na Hamza Johari AG Mwanasheria Mkuu kumpambania kwa hoja dhidi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC ili wapone kama Uhuru Kenyatta alivyoweza kuchoropoka kutoka ICC


TOKA MAKTABA :
6 Oktoba 2014


RAIS UHURU KENYATTA - WAHESHIMIWA NACHUKUA HATUA HII YA KIHISTORIA, KUKAIMISHA MADARAKA YA URAIS KWA MH. RUTO ILI NIENDE ICC THE HAGUE UHOLANZI KUJITETEA

View: https://m.youtube.com/shorts/ITgd_NJ_ulY
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ataelekea katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu huko Hague, Uholanzi kuheshimu wito kuhusu madai yake ya kuhusika katika kuandaa ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007. Rais Kenyatta alitoa tangazo hilo katika kikao maalum cha pamoja katika Bunge la Kitaifa la Kenya na Seneti. Pia alimteua naibu wake William Ruto kukaimu kama Rais akiwa hayupo. Hii hapa ripoti ya Chris Ocamringa. Kwa habari zaidi tembelea


View: https://m.youtube.com/watch?v=D8Odn8ne-SQ
 
Utashangaa muswada unapelekwa bungeni kwa hati ya dharura kuiondoa Tanzania kutoka katika hiyo Mahakama ya ICC.
Mkuu muwe mnajielimisha japo kidogo,

Hata kama wakijitoa Leo hii Kuna namna nyingi ya kumfikisha Samuya ICC,hii namna ni mbaya sana kuliko hata hii ya wanasheria kwani
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) linao uwezo wa kupeleka kesi ICC kwa kuwa Hili ndilo lango kuu la ICC kushughulikia viongozi wa nchi zisizo wanachama.
Kwa mfano, kesi ya Sudan kuhusu Rais wa zamani Omar al-Bashir ilipelekwa ICC na Baraza la Usalama, ingawa Sudan haikuwa mwanachama wa ICC.


Kwahiyo uwe mwanachama au lah, ICC wakikutaka wanakudaka tu, Samuya muuaji
 
Yametimia, waTanzania hivi karibuni kupata haki ya kuona kesi ikiendeshwa mubashara ktk mahakama ya ICC Uholanzi. Kutakuwa hakuna intaneti kuzimwa na hivyo ukweli wote ya yaliyotendeka kuwekwa hadharani

1764082128913.jpeg
 
Mkuu muwe mnajielimisha japo kidogo,

Hata kama wakijitoa Leo hii Kuna namna nyingi ya kumfikisha Samuya ICC,hii namna ni mbaya sana kuliko hata hii ya wanasheria kwani
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) linao uwezo wa kupeleka kesi ICC kwa kuwa Hili ndilo lango kuu la ICC kushughulikia viongozi wa nchi zisizo wanachama.
Kwa mfano, kesi ya Sudan kuhusu Rais wa zamani Omar al-Bashir ilipelekwa ICC na Baraza la Usalama, ingawa Sudan haikuwa mwanachama wa ICC.


Kwahiyo uwe mwanachama au lah, ICC wakikutaka wanakudaka tu, Samuya muuaji
Kwa hiyo huko UNSC, China itawatosa maswahiba wao wa CCM?

Vilevile sijasema hivyo kwa vile nawasapoti hawa wahuni.

Jambo la muhimu ni kuendelea kuapply pressure ili waendelee kutenda makosa. Hiko ndiyo kilitokea kule Sudan hadi Wasudan wenyewe wakamuondoa Al Bashir na wakamshitaki kwanza wenyewe wakati huo huo ICC ikiwa na yenyewe inamsubiri.
 
Minaona ili wajinasue niwazushe mapigano ya wenyewe kwa wenyewe Yani wazanzba na wamasai
 
Mambo yameanza kuchangamka!

Yalitokea Oktoba 29 yameweka historia mbaya sana katika taifa la Tanzania taifa ambalo lilikuwa limejaa amani lakini sasa hakuna Haki wala Amani tena!

Acha tusshughulikiwe tu mpaka tukomee maana viongozi wameendkeza matumbo yao
==============
Kesi ya kwanza kuhusu maandamano na vurugu za kabla na baada ya uchaguzi mkuu nchini Tanzania imeripotiwa kuwasilishwa mbele ya Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) mjini The Heague.

Nakala ya Waraka huo yenye Kurasa 82 imefikishwa kwa Naibu Mwendesha Mashitaka wa ICC, Nazhat Shameem Khan, katika Ofisi ya Mwendesha Mashitaka wa ICC.

Miongoni mwa yaliyoanishwa ni pamoja na mauaji ya kiholela, kupotezwa kwa watu, Utekaji na watu kuteswa pamoja na ukandamizaji wa kisiasa.
 
Huyu mtu na watu wake wa karibu wanastahili kufikishwa ICC na wahukumiwe,

Swali: Kesi ya William Rutto na Uhuru Kenyatta iliishia wapi?
Walitumia mabilioni ya Dola kuwalipa fidia Rushwa kwa familia zote zilizoitwa kama mashahidi ICC ndipo ushahidi ukawa umedorola, hata Tanzania tayari wezi au majizi madalali wa siasa Akina Wenye, Steven Nyerere, Abubakar liongo na wenzao wanajipanga kula mapesa ya mama Abdul na Abdul kwa kisingizio cha kwenda kuhonga CNN isitoe video zingine na pia wapelelezi wa ICC ni wizi mpya unakuja, wazee wa fursa wanaenda kuiba pesa za walipa kodi
 
Amiri jeshi mkuu aliyekuwa kila wakati anakumbushia yeye ndiyo mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama Samia Suluhu Hassan

DR. GERSON MSIGWA AWATUPIA MZIGO MZITO WASIOWEZA KUUTUA AMIRI JESHI MKUU NA VYOMBO VYA POLISI, KUHUSU RAIA WALIOULIWA, WALIOPOTEA


View: https://m.youtube.com/watch?v=9tgXI9mnWCw

Dr. Gerson Msigwa msemaji mkuu wa serikali akijibu maswali ya waandishi wa habari na kuusukumizia mzigo wa waliopotea, kufariki au wako mahabusu baada ya 29 Oktoba 2025, basi sehemu sahihi wazazi ,ndugu, jamaa n.k ni kwenda Polisi watapata habari zaidi
 
Samia na wenzie wajitayarishe kwenda kujitetea wao binafsi kwa ushiriki wao katika mauaji ya raia.

AG Hamza Johari awaambie Samia na wenzie ukweli wa jinsi mambo yalivyo magumu, hakuna namna ya kujiokoa wasifike The Hague Uholanzi kujitetea kuwa hawana hatia.

Kesi hizi za the Hague ICC Huwa zinarushwa mubashara live tena hata kwa KiSwahili watapewa wakalimani na wasikilizaji wanaweza kufuatilia mwenendo live / mubashara wa kesi hii ya kihistoria,



Madalali wa Siasa wanaenda mbio wanahaha kupishana kwa Mkoloni Kaburu toka Zanzibar wakimwahidi kuwa watatoa Rishwa CNN isirushe video zaidi na pia watawanunua wapelelezi wa ICC , ili kuvuruga upelekezi
 
DR. GERSON MSIGWA AWATUPIA MZIGO AMIRI JESHI MKUU NA VYOMBO VYA POLISI, KUHUSU WALIOPOTEA


View: https://m.youtube.com/watch?v=9tgXI9mnWCw

Dr. Gerson Msigwa msemaji mkuu wa serikali akijibu maswali ya waandishi wa habari na kuusukumizia mzigo wa waliopotea, kufariki au wako mahabusu baada ya 29 Oktoba 2025, basi sehemu sahihi wazazi ,ndugu, jamaa n.k ni kwenda Polisi watapata habari zaidi

Msigwa kajitoa fahamu zote ameamua kufanya ushetani bila kujua Damu za waliokufa zitamwandama hadi awehuke
 
Walitumia mabilioni ya Dola kuwalipa fidia Rushwa kwa familia zote zilizoitwa kama mashahidi ICC ndipo ushahidi ukawa umedorola, hata Tanzania tayari wezi au majizi madalali wa siasa Akina Wenye, Steven Nyerere, Abubakar liongo na wenzao wanajipanga kula mapesa ya mama Abdul na Abdul kwa kisingizio cha kwenda kuhonga CNN isitoe video zingine na pia wapelelezi wa ICC ni wizi mpya unakuja, wazee wa fursa wanaenda kuiba pesa za walipa kodi
Mkuu unaandika haya ukiwa wapi huku ukiwa umekata tamaa,kiufupi umeujaza ubongo wako mawazo ya rushwa na mawazo hasi juu ya mifumo ya kidunia,

Kaa utulie uone Samuya anavyonyolewa,acha kuuogopesha ubongo wako kwa mambo ambayo hayako hivyo.

Kiufupi Mfumo wa rushwa umekuathiri kiasi cha kufikiri Kila sehemu kunahitaji rushwa.
 
Kwa wale wenye uwezekano wa kwenda kunyea debe huko The Hague ni hawa hapa:

Waziri wa mambo ya ndani ahusiki sanasana ni mkuu wa jeshi la polisi, mkuu wa majeshi, mkurugenzi wa usalama wa taifa na amiri jeshi mkuu hao hawaponi.
 
Back
Top Bottom