Wanaume mliopata wake wa maana wa kuoa, mliwezaje? Au mlijitoa tu ufahamu mkaoa

Mzee alinambia siku flani uende ukahudhurie harusi kule xxxx dah siku ikafika nikaenda kwa kuchelewa na kukuta watu washaanza kula cha mchana basi nikaenda kujoin kwa waliochelewa ghafla namuona binti mrembo anashughulika kwenye ile harusi nikajisemea ndo huyu huyu na kweli tukijaaliwa in shaa Allah mwezi wa kumi tunafunga ndoa
Dua zenu jamani
 
Kaanze kumwelekeza mama yako.
 
Kirahisi hivyo? Tegemea kulia kilio cha mbwa Koko siku za usoni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Panapo uwezekano, Vuta hiyo mama chill nayo ndani.. Ile wazungu huita co-habiting.
Hii ndo imenifanyia kazi.
Mi siamini mapenzi ya kila mtu kukaa kwao tu afu mnaibuka, mnaoana.
Ishini tu wote humo ndani mjuane.
 
Imeandikwa Usimjaribu Bwana Mungu wako.. Lakini tumeruhusiwa kumjaribu kwa sadaka.. Chukua sadaka yako bila kujali ukubwa wake au udogo wake.. Inenee.. Zungumza na Mungu wako kupitia sadaka hiyo bila kuchoka ukimuambia akupe mke bora.. Usichoke na zoezi hilo mpaka utakapoonyeshwa mke wako..

Nilimpata mke wangu kwa njia hii na sijawahi kujutia kumuoa huyu mama.. Hata nikipewa nafasi mia za kuchagua mwanamke wa kuoa tena, nitamchagua huyu niliyepewa na Mungu..
 
yaani atoke aje barabarani uliposimama msimame mpige story??? Ni haki yao kuuliza hivyo maana ni upotevu wa mda
 
Hakuna mwanamke mzuri wala mwanamke wa maana, mke huumbwa na kutengenezwa
 
Ukoma/"leprosy" ni infectious disease......yaani kama ilivo TB,malaria.......sio genetic disease.....haukumtendea halo huyo binti
 
Tabia yako humu inaonyesha sionzuri.
Mtu mzima unamtukana mwanadada unadhani hata uraiani watu hawakusomi tabia . Acha madharau, jenga heshima kwa wanawake. Usipo fanya hivyo harusi utasikia kwa watu .

Kwanza mkali , hujishushi unataka uheshimiwe hela za mawazo sasa nani akubali kukaa namtu hajakua utapitisha miaka yakuoa kwa sababu huna tabia njema nawanawake wanaangalia wanaume wenye tabia njema kwao.

Wanaowasikiliza
Wanaowapenda
Wanaowajali (silazima pesa wanawake wengi wanahela zao sasa wewe unawakia wadada kisa nini .
Wanaooa wanamipaka , heshima upendo na wanasikiliza hawana madharau kwa wake zao.
NA bado hujajipanga kivile hata utambee nasema ukweli kwa respond zako humu kwa wanawake ni mbaya badilika if unataka uoe .

Kama upo serious acha madharau . Wanawake ndio lazima wakupatie uzao generation yako bila wao hutoboi
 
Kama matendo yapi?
Baadhi ya ishara kuu za ukomavu ni kutegemewa, kubadilika, kujitambua, kuheshimu mipaka yako, na uwezo wa kuwa mtulivu katika hali zenye mkazo kama vile kuhamasishwa kufanya majaribio magumu ...
Kukomaa kihisia pia kua na uwezo wa kupambana na hisia zako mf; Hasira, Njaa, Huzuni, kuridhika n.k

Huwezi jitunza ili uangukie kwa mtu wa ajabu, utaonekana wa ajabu. unapojitunza na kua na nidhamu binafsi unatengeneza attraction kwa wanawake wanaotafuta mwanaume bora, wataanza kujikanyaga wenyewe ...

"Kama huna nidhamu binafsi usitarajie kupata nidhamu toka kwa mtu mwingine" SOCRATES
 
Tulijipa ufahamu, tukaoa.


Tukusaidie nini ?
 
Ukoma/"leprosy" ni infectious disease......yaani kama ilivo TB,malaria.......sio genetic disease.....haukumtendea halo huyo binti
Labda mi sijui ni ule ugonjwa mtu anakuwa Hana vidole na wakurithi !! Kama sivo sio ukoma ni ugonjwa mwingine ila ni wakurithi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…