Wanaume mnaocheza vikoba mnatia aibu

Wanaume mnaocheza vikoba mnatia aibu

Tatizo mnachanganya sana mambo, kuna SACCOS, VICOBA na UPATU.

Huu UPATU ndo umeshamiri na wengi huuita VICOBA.

Mwanaume kushiriki SACCOS na VICOBA hakuna tatizo…Haina tofauti na kuwekeza HISA Bank. Na kwa faida zaidi anaweza kukopa kwa riba nafuu pale anapokwama/Anapohitaji kuwekeza.
 
Hebu nitafute muda nijielekeze vizuri sijui wapi nitasoma vizuri niielewe inafanyikaje
Nitakuelewesha vizuri utaelewa achana na mleta mada hajui umuhimu wa vicoba

Kwenye vicoba akiba yako ndio inakubeba kwa mfano umekwama labda una akiba ya mill 3 unaweza kukopa mill 9 kwenye kicoba chetu unakopeshwa mara 3 ya akiba yako

Na wanaume wengi wanakopewa na wake zao
 
Sisi tuna kikundi cha vikoba, tupo wanaume 17 tu. tuna katiba na kila kitu kinajieleza, mpaka sasa tuna million 203, hatujavunja huu mwaka wa tatu, tunakopeshana kwa riba tunakutana mara1 kwa mwezi, binafsi nakiheshimu sana nikihitaji 5m nakopa nafanya mambo yangu, sijawali sumbuliwa na fees za watoto kila mwaka, kikoba chetu kinazid kukua sababu tunakopa na kurudisha kwa riba, tumewekeza 100 Millions kwenye hati fungani ya serikali ya miaka 25. Kila miezi zita pesa inaingia. Kikoba kinakua tu. Crdb walitushawishi sana wanataka tuwekeze kwao ila tumechomoa. Kila mwanachama ana katiba mkononi.
Kwa mimi mtu akizarau vikoba wala siumizi kichwa.
 
Kila mtu na chake na anachokiamini kwa kuwa cha mtu akimsaidii kitu.

Kama wewe unanunua hisa kila mwezi za mil 100 bado sio sababu yakumdharau bodaboda anayeweka 200,000 kwa mwezi.

Haya ni majungu na umbea wenu kwa mnaohoji maisha ya wanaume wenzenu.

Yeye kuweza kujitunzia na kushindwa bado hayakuhusu.
 
Kuna Ile Moja eti mwanaume hatakiwi kusalimia "mambo''[emoji1751]
Ni kweli. Mwanaume hasalimii mambo. Sijawahi na hakuna mshikaji au mwanaume yoyote amewahi nitumia salami ya hivi

Salamu zetu huwa ni
  • hey
  • mkuu
  • kamanda
  • vp mwamba
  • chief
  • oyaa
  • aje
  • oii
  • arifu
  • bro
Ukianza na lolote hapo uliyemtumia ataelewa umemsalimia.

Kwa mrembo ukianza na "hello" inatosha.

Ila kama unataka sana kutumia mambo, basi sema "mambo vipi"

Hakuna mwanaume anasema "mambo" , hili ni kosa kubwa sana na mwanaume hawezi kumtumia mwanaume mwenzie hivi.
 
Ni kweli. Mwanaume hasalimii mambo. Sijawahi na hakuna mshikaji au mwanaume yoyote amewahi nitumia salami ya hivi

Salamu zetu huwa ni
  • hey
  • mkuu
  • kamanda
  • vp mwamba
  • chief
  • oyaa
  • aje
  • oii
  • arifu
  • bro
Ukianza na lolote hapo uliyemtumia ataelewa umemsalimia.

Kwa mrembo ukianza na "hello" inatosha.

Ila kama unataka sana kutumia mambo, basi sema "mambo vipi"

Hakuna mwanaume anasema "mambo" , hili ni kosa kubwa sana na mwanaume hawezi kumtumia mwanaume mwenzie hivi.
😅😅😅😅Wanamme mna kazi sana
 
Sijawahi kufikiri kama ndugu Deep Pond nawe una fikra kama hizi. Village Community Bank (VICOBA) ina tatizo gani? Au ulimaanisha upatu? Vicoba viko karibu nchi zote za SADC & EAC na imeonyesha mafanikio makubwa. Tatizo kwa hapa nchini utakuta havijasajiliwa na havina utaratibu unaoeleweka. Arusha Club SACCOS ilianziaga chini sana kwa marafiki tu kuanzisha umoja wao ila kwa sasa ipo level nyingine ikijumuisha matajiri wengi wa Arusha. Bado serikali inatakiwa itoe elimu kuhusu mambo ya fedha kwa wananchi. Itawasaidia kina Oscar Oscar na Deep Pond kutambua kuwa VICOBA havina jinsia. Umaskini hautaisha au kupungua kwa fikra kama hizi za Oscar Oscar na Deep Pond.
Acha maneno mengi wewe. Acha Vicoba mara moja.

Elewa maana ya neno Vicoba
 
Back
Top Bottom