Wagumu Tunadumu
JF-Expert Member
- Dec 10, 2022
- 7,591
- 23,296
1. Huyo baba Anakidemu nje alafu wadogo wanajua ila hawawezi kusema kwa bimkubwa ila wanachukia sana!
Kinachotokea ni kwamba, mzee hata akiongea anaonekana sio msafi mbele ya macho yao!
wana kitu cha kumlipua mzee akiendelea ku implement pressure kwao. Sasa Hiyo kitu lazima ishushe credibility kwa mzee
2.mzee anaongozwa ha hisia mbaya za makisio dhidi ya watoto wake wa kiume.
Inawezekana ana hisia mbaya zinazosababishwa na barehe ya watoto haswa aki reflect wakat wake wa barehe yeye alikuaje!
Anapata hofu kwamba watakuwa na madem na tabia za kishenzi huko nje!
Haswa wanapoanza kuongeza demand za mahitaji. Kwa watoto wa kiume tunakuwa na hizi tabia tunapoingia kwenye hiyo stage alafu tupate dem
1.fixed fees za shule, yaan hapo mzazi utapigwa mizinga ya michango hadi basi
2.kurudi home mapema ni changamoto kidogo kitu kinachomchochea mzazi kuhisi labda kuna ufiraun mdogoli anaufanya
3.adulthood effects kama kujiskia vibaya akifokewa, akiagizwa kufanya jambo fulani(kama wapo wawili huwa mbaya zaidi) hapo anakuwa anahisi yy ni mkubwa astahili kufanya hicho wakati kuna mdogoli wake.
Hasira za karibu(hizi zinasababishwa na fighting for recognition!) Katka nafsi yake kuna kitu kinamsukuma aoneshe yy ni mkubwa na wazazi mlijue hilo! Hiyo ni hali ya kawaida kabisa na inadumu kwa muda mpaka pale atakapoanza kuhisi yes now i retain my respect..
Mzee apunguze tu mikwara aseeh kwasabb huo umri mtoto anakuwa nje ya dunia ya woga kabisa badala yake anakuwa na heshima tu ya kutambua huyu ni mzazi, but ni very limited si wa kujifanyia kila anachotaka kwangu kwasabab tu kanizaa!!
Mzee anataka kutumia ubabe umri wa kutumia maongezi zaidi!!
Fimbo ya kijana wa miaka ya barehe ni maneno! Amini nakwambia maneno yanamuumiza vibaya sana kuliko viboko vya matakoni!
Ajitahidi kutumia lugha zenye ukali lakini wa heshima(asitweze utoto wa mtoto na akakweza ukubwa wake kam mzazi)
Atumie lugha za michano ya kiume ile!
Sio ngonjera za bi kidude!
Kumbusho tu kw madingi!
Umri wa kuchapa na kufundisha watoto kwa nguvu ni huo mnaowadekeza na kuwaita majina yote ya upenzi kwa watoto(miaka 03-11)
Mtoto akipita huo umri hutakiwi tena kuendekeza ubabe kwa sababu tayar akili yake inaanza kupembua zuri na baya! Tumia maneno mzee
Naomba kuwasilisha
NO REFORMS , NO ELECTION.
NO REFORMS , NO ELECTION.
FREE TUNDU ANTIPAS LISSU
Wee wafundishe watoto wako adab Kwa baba Yao, asilimia kubwa ya malezi ya mtoto anachangia mama, Sasa wewe endelea kuwadekeza kijinga na kimamama,Sawa, basi punguza shobo kwenye uzao wa mwanaume wenzako. Shukrani!
Umezielezea hizo steji vizuri sana. Teenagers wanaacha ku-idolize wazazi, na wanakua na ujuaji sana sana ila pia na wanaanza kuona ubinadamu na mapungufu wa baba zao.Nilichojifunza katika uhusiano kati ya, mtoto wa kiume na, baba yake,
Kuna umri,miaka 0 mpaka 14,baba, anakuwa, ni, shujaa, kwa, mtoto, mtoto anakuwa, anatamani, kuwa, kama, baba, anamuona baba yake ndio hero wake, (kijana, wangu aliiga, na, akapenda kila ninachofanya, weight lifting, martial, art, ufundi umeme na magari, kuangslia series, kuendesha bike, gari kwa, speed, kutembea, u siku sana vichochoroni, bila uoga,) kuna umri 18-30, mtoto wa, kiume atqmchukia dingi yake, harafu, akiwa, na, familia, ndio ataanza kumuelewa, dingi yake for, na mzee akifariki, mtoto wa, kiume ndio ufumbuka na kuelewa logic ya kila kitu alichokuwa anafanya dingi!
Aliwakuza Mixer, Asante kwa kushare experience yako.Kwanza aliwakuzaje...
Kizungu mtoto nae ana haki za kipuuzi puuzi.
Ama kibantu, baba ni baba tu!?
Ama mixer?
Kama kizungu alishakosea, haswa mtoto anapofikia balehe.
Kipindi hiki kuna vi tabia fulani huwa vinajengeka kwetu, kutuna, kakiburi ka hapa na pale.
Mie nimekuwa baba ameshafariki lakini niliweza kujicontrol kwa yale makuzi niliyopewa na mzazi wangu.
Mtoto wa dada yangu, mie nilikuwa namsimamia ila alipokuwa akaanza kakiburi,
Siku moja nikataka kumuadhibu naona analeta za kuleta,
Nikampa nafasi akunje ngumi, kibaya zaidi akakunja basi nilimtwanga kama mtu mzima mwenzangu, mpaka alipopiga kelele ya kufa, ndio nikamuacha na kumueleza yeye ni mtoto tu akae awe na adabu..
Tokea siku hiyo akarudia kwenye kanuni za maisha, muda wa kula ni mmoja na ukifika awepo mezani, uhuru wake mwisho saa 2 kwenda kuswali baada ya hapo anakuwa mtaani, iwe ndani ama nje lakini nyumbani
Hapo baba mtu afanye maamuzi magumu.
Hata hawa wangu shule hawana shida kabisa na huko nje wanasifiwa ni wataratibu.Cha ajabu,sisi magangwe huwa tuna akili za darasani na maishani.Wa sasa hawa tusiwapige sana watavunjika.Sijui ni wa plastics?
NB;Oooh...man! I'm growing old now!
Baba yao ndiyo ana final say na hata wakija kwangu kuomba kitu nawaambia waende kwa baba yao, sina hela 😂 haijalishi ni kidogo au kikubwa kiasi gani, watake wasitake watazungumza na baba yao na kumueleza mahitaji yao.Unajua watoto huwa wanaangalia sana jinsi nyinyi wazazi mnavyo ishi, mkiwa mnaheshimiana wanajua,na mkiwa mnazarauriana pia wanajua, na pia wanajua kati ya baba na mama nani ni final say wanajua, na siku zote watamuheshimu sana yule mwenye final say!!
Safi sana, sauti na uwepo wa baba unaleta tofauti sana kwenye nidhamu ya watoto, wengi wao huwa hawatuogopi sisi mama zao.Kawaida kwa watoto wa kiume kutokua na stori na baba yao hilo nimeliona kwetu nikiwa mdogo na hata sasa nikiwa na familia.
Mzee wetu alikuwa anatupa task za kufanya kama kupanda miti, bustani n.k. wakati wa msosi baada ya chakula tutaulizwa kazi tulizopewa au majukumu ya kusimamia halikadhalika na mimi naenda hivyo hivyo na vijana. Kuna kazi kama kusafisha mabanda ya kuku, kulisha na kupikia mbwa pia kupata ripoti zote kuhusiana na mazingira ya nyumbani.
Kuna kipindi nilisafiri kwa wiki mbili, vidume wakawa full kujiachia utawala wa manyani. Niliporudi nikacheki mazingira nikaona mambo mengi hayapo sawa. Mama yao alikuwa akiwaambia wanamchukulia poa alikuwa akinitonya nikamwambia asubiri nirudi.
Wakati wa chakula cha jioni tukapiga msosi halafu nikawauliza mambo yao ya shule na mengine yanakwendaje. Nikawauliza kama mabanda ya mbwa yamesafishwa, mbwa wameogeshwa wakawa mabubu na wanaangalia chini. Nikawauliza kama kulikuwa na issue yoyote iliyowakwamisha kutimiza majukumu yao wakasema hapana. Sikugombana nao nikawaambia kabla jua halijatoka asubuhi nataka usafi na task zao wazifanye. Aisee walitoka kiunyonge wakaenda kufanya usafi na mambo yote.
Asubuhi nimekuta kila kitu kimefanyika usiku.
Waduwanzi hao, hapo ndipo pakushikilia kamba, akiwachekea tu na elimu ya mtaa hawana watakuwa masela sasa hivi, utasikia namba tu 45 kipaji, 26 sijui nini...Aliwakuza Mixer, Asante kwa kushare experience yako.
Ni kweli hivyo vitabia vipo na baba yao anasimama kwenye nafasi yake kuvirekebisha.
Wanamtii ila ndiyo hivyo upendo kutoka kwao ni kama umekwisha au kama upo hawauonyeshi.
💯 💯 💯Mtoto kumdindia Mzee huwa haipo.
Tulikuwa tukiitwa
Majibu ni"Naam" unakula maagizo "Ndiyo" unapotea.
Hakuna muda wa kujibizana Wala kujitetea Hadi pale unapewa nafasi ujieleze
Sasa Leta Moral codes zako uuone Moto.
Raise them Harder... No Mummy voice out there.
Inshallah na ikawe hivyo 💯Kila kitu ni malezi tuu na maelekezo utakayompatia..... Ninaamini kwa juhudi ninazozifanya basi 98% Hatokuja kuwa "Mpumbavu"
Ulivyokua kijana na kipindi cha balehe (teen age), mahusiano yako na baba yako yalikuwaje?
Nina watoto wa kiume wapo kipindi cha balehe na hawaivi kabisa na baba yao, japo hapo zamani walikua wana ukaribu sana. Ugomvi hauishi, kila kitu kidogo lazima watoto wapate mihemuko au wapate hasira na baba yao naye anakasirika (they trigger each other kupita kiasi). Watoto pia hawana uoga kuongea mbele ya baba kama wakiambiwa kitu na hawana utayari (japo huwa hawavunji heshima au kutukana).
Hii hali ni mpya (kwa miaka kadhaa sasa) tokea waingie kwenye balehe (teen years). Wazazi ambao mmeshalea male teens (vijana wa kume wakiwa kwenye balehe) uzoefu wenu ulikuwaje na je baada ya balehe, ukaribu na mahusiano huwa yanarudi tena kama zamani?
Na wanaume wa JF, vipi na wakati unakua mahusiano yako na wazazi yalikuwaje?
Asanteni na Jumapili njema!
View attachment 3360276
Udikiteta sasa hapo Africa ni Africa tu, Wazungu wao awatumii nguvu kwasababu tamaduni zao ni Binadamu wote ni sawa.Daah ni kweli kabisaa 💯
Hawa wangu huwa wanahoji na vingine wanakua sahihi kutuchallenge ila tunatumia mamlaka kama wazazi tu kuwanyamazisha.
Mkuu aliona hakuna madhara kama wewe una kunywa na hakuna tatizo, Sisi Nyumbani Mzee wetu alikua mlevi sana na anafanya mambo ya haibu kwenye Jamii kwahiyo zile tabia zake za kilevi zilitufanya watoto wake % kubwa hatupendi kunywa pombe tunaogopa kurithi zile tabia zake tulijua tukinywa pombe tutafanya mambo ya hovyo, siyo kwamba tulikua hatunywi tuna kunywa lakini Pombe siyo kipaumbele chetu, ila ile tabia ya Mzee ya kulewa na kufanya mambo ya hovyo kairithi Kaka yetu, kwahiyo Mzazi unaweza kufanya mambo ya hovyo mbele ya watoto na jamii ila watoto wakajifunza kutokufanya tabia hizo mbaya za Mzazi wao, na Mzazi unaweza kuwa na matendo mazuri mbele ya watoto na jamii kwa ujumla lakini watoto wako wakaja kua vituko kwenye Jamii.Nilishawahi kumtuma mwanangu wa kwanza wa kiume kwa shemeji yangu kunifatia wine, akainywa yote njian na akarud kalewa...
Nilipotaka kumuadhibu akasema mbona wewe unakunywaga...
Basi nikamnasa makofi matatu, alafu nikamwambia hayo makofi nimekupiga kwa kosa la kukosa uaminifu,(kuagizwa mzigo wa watu na ukaunywa) sijakudunda kwa ajili ya kunywa pombe.
Watoto wa kiume jau..
Hakika, wazazi ndio waalibifu wa kwanza katika saikolojia ya mtoto ktk malezi kabla ya jamii..Mkuu aliona hakuna madhara kama wewe una kunywa na hakuna tatizo, Sisi Nyumbani Mzee wetu alikua mlevi sana na anafanya mambo ya haibu kwenye Jamii kwahiyo zile tabia zake za kilevi zilitufanya watoto wake % kubwa hatupendi kunywa pombe tunaogopa kurithi zile tabia zake tulijua tukinywa pombe tutafanya mambo ya hovyo, siyo kwamba tulikua hatunywi tuna kunywa lakini Pombe siyo kipaumbele chetu, ila ile tabia ya Mzee ya kulewa na kufanya mambo ya hovyo kairithi Kaka yetu, kwahiyo Mzazi unaweza kufanya mambo ya hovyo mbele ya watoto na jamii ila watoto wakajifunza kutokufanya tabia hizo mbaya za Mzazi wao, na Mzazi unaweza kuwa na matendo mazuri mbele ya watoto na jamii kwa ujumla lakini watoto wako wakaja kua vituko kwenye Jamii.