Veteran Sailor
JF-Expert Member
- May 28, 2025
- 2,042
- 4,416
Hakika, wazazi ndio waalibifu wa kwanza katika saikolojia ya mtoto ktk malezi kabla ya jamii..Mkuu aliona hakuna madhara kama wewe una kunywa na hakuna tatizo, Sisi Nyumbani Mzee wetu alikua mlevi sana na anafanya mambo ya haibu kwenye Jamii kwahiyo zile tabia zake za kilevi zilitufanya watoto wake % kubwa hatupendi kunywa pombe tunaogopa kurithi zile tabia zake tulijua tukinywa pombe tutafanya mambo ya hovyo, siyo kwamba tulikua hatunywi tuna kunywa lakini Pombe siyo kipaumbele chetu, ila ile tabia ya Mzee ya kulewa na kufanya mambo ya hovyo kairithi Kaka yetu, kwahiyo Mzazi unaweza kufanya mambo ya hovyo mbele ya watoto na jamii ila watoto wakajifunza kutokufanya tabia hizo mbaya za Mzazi wao, na Mzazi unaweza kuwa na matendo mazuri mbele ya watoto na jamii kwa ujumla lakini watoto wako wakaja kua vituko kwenye Jamii.
Najiona mwenye hatia kila siku kwa mtoto wangu...