Wanaume na wazazi wenye watoto wa kiume, hii imeshawahi kuwatokea?

Hakika, wazazi ndio waalibifu wa kwanza katika saikolojia ya mtoto ktk malezi kabla ya jamii..
Najiona mwenye hatia kila siku kwa mtoto wangu...
 
Siyo Simba dume ata Kuku wa kienyeji Nyumbani tulikua tunafuga kuku wa kinyeji nilikua na Shanghai kukua akitotoa vifaranga anakua ana wapenda watoto wake sana lakini watoto wakishaanza kukua tu nilikua nashangaa anaanza kuwafukuza wasimfate kila watoto wake wakimfata wawe pamoja yeye mama yao wana wadonyoa mpaka mwisho wanazoea kutembea wenyewe mwishoe kila mtu anashika njia yake ya Maisha, Nimejifunza Kuku wakienyeji ana malezi mazuri kwa watoto wake, kipindi cha utoto atawapenda vifaranga vyake na kuvikumbatia ila vikishaanza kukua tu ana vibadilikia kama siyo vifaranga vyake.
 
Hayo ni malezi mabovu tu asikudanganye mtu kwamba sababu ya barehe. Inasingiziwa barehe. Huyo ni rahisi sana kutengeneza njia yake ambayo inaweza kuwa mbaya au vinginevyo. Lakini kwenye mbaya ndio 90%
 
Asila za kurith mbaya sana, hiyo steji kuipita salama kwa kijana ni ngumu kidogo, Mimi wakati nipo Shule ya Msingi baadhi ya Walimu wetu walikua wanajeshi sasa Walimu mmoja Mwanajeshi alinichapa bila kufanya kosa shuleni nilikasilika nikapanga siku nimvizie akiwa anatoka shuleni na mimi nilipe kisasi kwa kumpiga na jiwe kichwani na kukimbia, siku hiyo sikwenda shule nikaenda kwenye kichaka nikiwa na Mawe yangu matatu kwa bahati mbaya alipita na wenzake zoezi likashindikana. Nilipanga nimpige na jiwe la kichwa nikimbie kwenye vichaka na asingeweza kuniona.
 
Na wewe unatakiwa uwakazie lakini kama baba yao yupo vizuri kwenye Malezi.
 
Point yako ni nzuri na kuna cha kujifunza.

Binafsi, siajwahi kuwashtakia watoto matatizo yangu ya kimahusiano na sina changamoto ambazo zimenizidia kiasi cha kutafuta pa kusemea.
 
Daah pole sana.
Kuna wazazi wengine watata kupita kiasi na wanakosea kwenye malezi.
 
Umeshawajaza upumbavu kilichobaki watampiga huyo baba yao. Jipongeze umekuza midume ya kukulinda.
Kwanini hizo lawama napewa mimi?, sijawahi kuwaambia kitu chochote kibaya kuhusu baba yao na hatuna mahusiano yenye magomvi kwamba wanaona mitafaruku nyumbani au matatizo.
 
Asante kwa kushare mpwa.
Ni kipindi kigumu kwa kweli na cha kwenda nacho kwa busara.
 
Umenena
 
Asante, umesema vyema.
Nimelichukua hilo πŸ’―πŸ™
 
Ni kipindi ambacho unatakiwa usali sqna ili uwe na utulivu wa rohoni.
Katika kipindi hiki, watoto wanabadilika kimwili, kihisia na kiroho. Hapa ndipo kipimo cha uzazi na ulezi kinapotokea
Asante, ni kweli kabisa.
Utulivu na msaada wa kiroho unahitajika mno kuvuka kipindi hiki cha malezi.
 
Usimtume tena pombe πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ akiwa mlevi atakuja kusema baba yangu ndiyo alinifundisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…